Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HABARI. Onyesha machapisho yote

Obasanjo atimuliwa chamani PDP

0 maoni
Obasanjo atimuliwa chamani
Aliyekuwa rais wa Nigeria Olusegun Obasanjo ametimuliwa kutoka chama tawala cha PDP.
Bwana Obasanjo amepinga vikali kuahirishwa kwa uchaguzi nchini Nigeria hadi mwezi machi.
Rais huyo wa zamani amekuwa mstari wa mbele kumkosoa rais wa sasa Goodluck Jonathan, ambaye anawania muhula wa pili kwa tiketi ya chama cha PDP.
Rais Jonathan anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mgombea wa upinzani bwana Muhammadu Buhari.
Wakuu wa jeshi la Nigeria
Muda mchache kabla ya kutimuliwa chamani, Obasanjo aliwaambia waandishi wa Habari kuwa alikuwa akitarajia kutimuliwa chamani japo ujumbe ulimfikia mapema kabla ya ya tangazo.
Alipasua kadi yake ya uanachama hadharani jambo lililowaaudhi wandani wa rais kwani ilikuwa inaonesha mgawanyiko katika chama huku uchaguzi mkuu ukisogea.
Obasanjo amesema kuwa hatojiunga na chama chochote .
"Nitasalia raiya wa kawaida ,mimi ni Mnigeria.
Niko tayari kuchangia maendeleo ya taifa kwa ushirikiano wa mtu yeyote bila ya kujali msimamo wa kisiasa.
Hakuna haja ya watu kupanga njama ya kunibumburusha Chamani Chukuwa kadi yenu ya uanachama ,siihitaji'' alisema bwana Obasanjo.
Rais wa sasa Goodluck Jonathan amemlaumu Obasanjo kwa kuipigia debe chama kikuu cha upinzani All Progressives Congress (APC) na mpinzani wake mkuu Buhari.
Juma lililopita Obasanjo aliiambia gazeti la London Financial Times kuwa anaomba kuwa rais Goodluck hatofikia kiwango cha kusema ''asipopata ushindi hakuna atakayeipata''
Rais Jonathan amemkashifu vikali kwa matamshi hayo akisema kuwa Obasanjo anachochea upinzani dhidi ya uongozi wake.
Jeshi la Nigeria limemlaani Olusegun Obasanjo na kusema kuwa ameliabisha jeshi kwa kuashiria kuwa walikuwa na njama ya kuongeza muda wa rais Jonathan.
Bwana Obasanjo ambaye aliyekuwa jenerali wa jeshi na rais chini ya utawala wa kijeshi aliwaudhi wengialipodai kuwa kuhairishwa kwa,
uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ilikuwa ni njama ya rais wa sasa Goodluck Jonathan kutumia jeshi kujiongezea muda wake ofisini.
Obasanjo alipasua kadi yake ya uanachama wa chama tawala PDP hadharani akisema anakihama chama hicho.

Wezi wa kompyuta wameiba dola bilioni 1

0 maoni
Wezi wa kompyuta wameiba dola bilioni 1
Genge la wezi wa kompyuta limefanikiwa kuiba takriban dola bilioni moja kutoka kwenye akaunti za wateja wa mabenki 100 katika mataifa 30.
Kampuni inayosimamia usalama wa programu ya kompyuta inayohakikisha data ya wateja iko salama Kaspersky Lab imesema katika ripoti yake maalum.
Ripoti hiyo inaelezea mbinu mpya ya wezi wa Kompyuta wanaotumia mbinu mpya ya kudakua nambari za akaunti za wateja za siri kabla ya kuingia na kupora pesa .
Kaspersky imesema kuwa wizi huo ulianza mwaka wa 2013 na bado unaendelea hata leo kwani mabenki yote yalioathirika hayana uwezo wa kuwazuia wezi hao .
Hadi kufikia sasa ripoti hiyo inadai kuwa takriban dola bilioni moja zimeporwa kutoka kwenye akaunti za wateza.
Genge hilo la wezi, lililoanzia shughuili yake nchini Urusi, Ukraine na pia Uchina ndilo linalolaumiwa kwa wizi huo.
Kampuni hiyo ya Kaspersky inasema inafanya juhudi za kuzima wizi huo kwa ushirikiano na polisi wa kimataifa Interpol na polisi wa bara ulya Europol .
Kwa mujibu wa ripoti hiyo mabenki katika mataifa 30 yakiwemo, Russia, Marekani , Ujerumani , Uchina, Ukraine na Canada yameathirika pakubwa.
Wezi walitumia programme ya kipekee
Kamanda wa kikosi cha polisi wa kimataifa Interpol bwana Sanjay Virmani, amesema kuwa wezi wataendelea kutumia upungufu wa miundo msingi katika sekta ya uchumi wa mataifa husika hadi pale kutaibuka umoja wa kuzuia mapengo.
Kaspersky hata hivyo inasema kuwa genge hilo linalenga mabenki bila ya kuwaibia watu binafsi.
genge hilo kwa jina Carbanak, linatumia mbinu ya kuambukiza virusi kwenye mashine za benki ikiwemo kamera za CCTV ilikunakili kila kitu kinachoandakiwa kwenye kompyuta.
Kutokana na uweledi wao genge hilo lilituma pesa kwenye account zao huku wengine wakiamrisha mmitambo ya kutoa pesa ATM kumimina pesa bila kikomo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo kila tukio la wizi lilihusisha takriban dola milioni kumi.

HATUJAKAMATA MTU - POLISI

0 maoni
Jeshi la Polisi nchini, limesema majambazi waliokuwa wamejificha katika mapango ya Amboni nje kidogo ya jiji la Tanga wamekimbia.
Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa jeshi hilo, Kamishna Paul Chagonja, akizungumza jana alisema majambazi hao wamekimbia baada ya kuzidiwa nguvu na askari wa jeshi lake wanaoshirikiana na Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Nini unataka kuliambia jeshi la polisi?

Misri:Viongozi wakataza unenguaji viuno

0 maoni

Densi ya kunengua viuno na tumbo ya 'Belly Dance nchini Misri
Bodi ya kidini ya misri, imetoa fatwa kukataza uonyeshaji wa kipindi kilichoanzishwa kwenye televesheni nchini humo kuonyesha densi ya jadi ya wanawake wa misri ya kunengua viuno almaarufu 'belly dance'.
Ngoma hiyo inayofanana na chakacha ya waswahili imechezwa tangu zama za kale na imenakiliwa hata katika enzi za ma-pharoah katika nchi hiyo ya Misri.
Ni densi ambayo isingekosekana kwenye sherehe muhimu. Harusi au burudani nyenginezo.
Maelfu ya watalii wanaoitembelea Misri hupenda kwenda kuona inavyochezwa lakini mnamo siku za hivi karibuni wasichana kutoka sehemu nyingi duniani hasa ulaya na hata uchina wameripotiwa kwenda Misri kujifundisha jinsi ya kucheza densi hiyo.
Ni ajabu kuwa sasa imekuwa maarufu katika mataifa ya kigeni kuliko Misri kwenyewe ambako haichezwi ovyo ovyo hadharani.
Misri ni nchi ya waislamu wengi hivyo burudani zina miiko yake- densi kama hizo hazichezwi hadharani hasa kwenye mikusanyiko ya umma ya mchanganyiko wa wake kwa waume.
Hivi wale wanaozishabikia ni wachache kiasi kuwa sasa kuna hofu kuwa huenda utamaduni au ustadi huo wa belly dancing unakufa polepole Misri.
Pengine ni kwa kutambua hilo ndio waandalizi wa vipindi wakaona bora walete shindano la ngoma hiyo kwenye televisheni ya kitaifa kuhifadhi na kuipa umaarufu kama kitu cha asili ya Misri.
Lakini bila shaka hilo haliswihi machoni pa bodi ya kidini nchini humo na wametoa amri kipindi hicho kiondolewe mara moja .
Bodi hiyo Dar al-Ifta imesema kuonyesha watu wakinengua viono kwenye televisheni kutazorotesha maadili ya jamii na kutapelekea mwenye itikadi kali kupata visababu vya kuipaka matope Misri ili kutia doa imani ya kiislamu ya taifa hilo.
Kutokana na kauli hiyo sasa kipindi kilichoikuwa kipeperushwe hewani juzi usiku kimeahirishwa.
Ni makala moja tu ya kipindi hiyo ndiyo iliyooneshwa - Mojawapo wa waliokuwa majaji wa kupendekeza washindi kwenye kipindi hicho ni mchezaji maarufu wa densi hiyo aitwae Dina na wengi wa washindani katika mchuano huo wa belly dancing wala si raia wa Misri .

Boko Haram wazuia watu kuzika maiti

0 maoni

Wapiganaji wa Boko Haram wamesababisha maafa Kaskazini ya Nigeria ngome yao ya vita
Taarifa za kutisha zimeibuka kutoka mjini Bama moja ya miji ambayo ilitekwa na wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram Kaskazini Mashariki ya Nigeria
Seneta mmoja wa eneo hilo,Ahmed Zanna, aliambia BBC kwamba wakazi hawaruhusiwi kuwazika jamaa wao waliouawa na wapiganaji hao.
Inaarifiwa miili imetapakaa katika barabara za mji huo ambao Boko Haram imeuteka.
Kundi hilo linasemekana kuuteka mji huo huku wapiganaji wa kundi hilo wakishika doria katika barabara zake.
Maelfu ya watu wametoroka huku idadi kubwa ya wengine wakiuawa.
Seneta huyo ameitaka serikali ya Nigeria kupeleka wanajeshi mjini Maiduguri ambao ni mji mkuu wa jimbo hilo ili kuulinda dhidi ya wapiganaji hao.
Mnamo siku ya Jumatano serikali ya jimbo hilo ilikanusha madai kuwa jimbo hilo limetekwa na wapiganaji hao.
Maafisa wakuu wanakisia kuwa watu 26,000 wameachwa bila makao kutfuatia mapigano katika mji wa Bama.
Bwana Zanna anasema kuwa barabara za mji huo zimejaa miili ya watu na Boko Harama imewakata wakazi kuwazika jamaa wao. ''Kwa hivyo hali ni mbaya na inaendelea kuzorota,'' asema bwana zANNA
Boko Haram wameteka miji kadhaa Kaskazini Mashariki ya Nigeria, katika miezi ya hivi karibuni na kusababisha hofu kuwa huenda wakaufikia mji mkuu Maiduguri.
Bwana Zanna amesema kuwa itakuwa janga kubwa ikiwa Boko Haram wataushambulia mji wa Maidiguri ambao una watu zaidi ya milioni mbili.

Japan ikotayari kutoa dawa ya Ebola

0 maoni

Serikali ya japan inasema kuwa itatoa dawa kuwatibu wagonjwa wa Ebola
Serikali ya Japan imesema iko tayari kutoa dawa waliotengeneza ya kupambana na homa kali iitwayo T-705 ambayo huenda ikasaidia katika vita vya kupambana na Homa ya EBOLA.
Matumizi ya dawa hiyo hayajaidhinishwa na shirika la afya duniani World Health Organisation, haijabainika iwapo itafaa kutoa afueni kwa wagonjwa wa Ebola au la .
Msemaji wa kampuni inayotengeneza dawa hiyo T-705 iitwayo Toyama Chemicals, anaeleza kuwa dawa hiyo ina uwezo wa kukabiliana na virusi vinavyosababisha homa kali hivyo huenda ikasaidia katika mapambano dhidi ya Ebola.
Serikali ya japan inasema kuwa itatoa dawa kuwatibu wagonjwa wa Ebola
Takao Aoki msemaji wa kampuni ambayo imetengeneza dawa hiyo, alisema kwamba dawa hiyo iliyotengenezwa ili kutibu virusi vya mafua vinavyojitokeza tena baada ya matibabu na vile visivyo vya kawaida ilipitishwa na wizara ya afya ya Japan katika mwezi wa Machi.
Akiongeza alisema kwamba Kampuni hiyo ya Fujifilm inafanya mazungumzo na utawala wa chakula na dawa Marekani juu ya kupimwa uwezo wa dawa hiyo kuhusiana na matibabu ya Ebola.
Kwa sasa hamna dawa wala chanjo yoyote iliyothibitika na kuidhinishwa kutibu Ebola, lakini kutokana na janga la mlipuko wa Ebola huko Afrika magharibi na sasa Jamhuri ya Kidemocrasi ya Congo, Shirika la afya duniani WHO limesema itakubali matumzi ya dawa za majaribio kwa wagonjwa, ilimradi utaratibu na masharti waliyoyaweka yafuatwe na wagonjwa wenyewe wahusishwe katika kutoa idhini .
Majuzi wamarekani wawili waliokuwa wamethibishwa kuugua Ebola walipona baada ya kupewa dawa ya majaribio iitwayo ZMapp.
Daktari aliyepona Ebola baada ya kutibiwa na dawa ya Zmapp.
Yoshihide Suga ambaye ni katibu mkuu baraza la mawaziri aliwaambia wandishi wa habari kwamba Japan inawezapeana dawa hiyo wakati wowote WHO itakapoaagiza.
Aliongezea kusema kwamba Japan inangoja maelezo zaidi ya uamuzi wa WHO kuhusu matumizi ya dawa ambazo hazijajaribiwa lakini katika kesi yoyote ya dharura, Japan inaweza ikajibu maagizo yoyote ya kibinafsi hata kabla ya uamuzi wowote wa WHO.
Mapema mwezi huu WHO ilisema kwamba ni sawa kutumia dawa ambazo hazijajaribiwa kwa wagonjwa wa Ebola kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo.

Hofu ya Ebola Tanzania, mmoja ahofiwa

0 maoni
Mhudumu wa afya akiwa katika hali ya tahadhari ya Ebola huko Afrika Magharibi
Kuna taarifa ya kuwepo kwa mtu mmoja anayehisiwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa Wizara ya Afya ya Tanzania Nsachris Mwamaja mtu huyo ana asili ya Afrika Magharibi ambaye ni mkazi wa mji wa Dar es Salaam ambaye alifika katika hosptali moja akiwa na homa kali ikiwa ni dalili mojawapo ya ugojwa huo .
Bwana Mwamaja amesema mgonjwa huyo ambaye ni mtoto wa makamo tayari ameshatengwa na yupo chini ya uangalizi wa karibu madaktari katika hosptali Temeke ambayo ni ndio iliyotengwa kwa ajili ya watakaohisiwa kuwa na ugonjwa huo.
Amesema sababu nyingine ya kuhisiwa kwa mtu huyo kuwa huenda ameambukizwa virusi vya ugonjwa huo ni kwa vile hivi karibuni alitokea nchini Benin.
Hii ni mara ya kwanza ya kuwepo kwa taarifa za mtu kuhisiwa kuwa na virusi vya Ebola nchini Tanzania.
Taarifa hizi zinakuja baada ya hapo awali serikali ya nchi hiyo kukanusha taarifa iliyotolewa na gazeti moja la udaku kuwa kuna mgonjwa mmoja wa Ebola aliyegundulika nchini Tanzania.

Mtoto wa Simba amlilia mamake

0 maoni
Simba huyo aliwaelekeza walinzi hadi katika mzoga wa mamake
Mtoto wa simba aliwaongoza askari wa kulinda wanyama kwenda ulipo mwili wa mama yake ambaye alikuwa ameuawa katika mbuga moja ya kuhifadhi wanyama nchini India, kitendo ambacho maafisa wa wanyama pori wanakilelezea kuwa si cha kawaida.
Askari wa wanyama pori ambaye alimwona mtoto wa Simba akijificha vichakani, alimfuata na kugundua mwili wa Simba aliyeuawa katika kilima jirani.
Mtoto huyo wa simba aliulinda mwili wa mama yake hadi pale mlinzi wa wanyama pori aliporudi na maafisa wa wanyama pori na polisi kuondoa mzoga huo.
Uchunguzi uliofanyiwa mwili wa simba huyo ulibainisha kuwa alikufa katika mapigano na wanyama wengine huenda aliuawa na kundi la nyati.
Naibu mhifadhi wa Misitu katika eneo la Gir, Anshuman Sharma, amesema tabia ya simba huyo mtoto ni nadra kutokea na ni cha aina yake, kitu ambacho hajawahi kushuhudia katika miaka yake mingi ya kufuatilia tabia za simba.
Gir katika jimbo la Gujarat ni mahali wanapopatikana kwa wingi simba wa Asia na kwa mujibu wa sense ya wanyama iliyofanyika mwaka 2010, kuna simba 411 katika mbuga hiyo.
"Jumamosi mchana, nilikuwa nafanya doria katika hifadhi ya Tulsi-Shyam nilipomwona mtoto wa simba akichificha katika vichaka,"mlinzi wa msitu Rana Mori ameiambia BBC.
''Watoto wa Simba huambatana na mama zao''
Watoto wadogo wa simba nadra kuwakuta peke yao , kwa ujumla wanafuatana na mama zao na Bwana Mori anasema alianza kumtafuta mama ya simba huyo mtoto.
"Nilimfuatilia mtoto wa simba ambaye aliniongoza hadi kwenye mwili wa mama yake uliokuwa umelala katika kilima kidogo. Simba huyo jike aliitwa Rupa [likiwa na maana ya Mzuri].Kwanza alionekana kama aliyelala usingizi, lakini wakati hatikisiki, nilimsukuma na fimbo yangu. Ndipo nilipogundua kwamba simba huyo jike alikuwa amekufa," amesema.
Wakati Bwana Mori aliporejea na kundi la maafisa kuondoa mzoga huo, walimkuta mtoto huyo wa simba akiwa amekaa kando ya mwili wa mama yake.
Simba huyo jike ambaye alikuwa na umri wa miaka kumi na moja , alivunjika mbavu na kupata majereha ya ndani na kufa kutokana na kuvuja damu nyingi.
Mtaalam wa Simba Yadvendra Dev Jhala wa taasisi ya Wanyama Pori ya India ameiambia BBC kuwa hajawahi kusikia tukio kama hilo linalomhusu mtoto wa simba.
''Simba na walinzi wao''
Lakini amesema katika eneo la Gir hakuna mgogoro kati ya simba na binadamu na "kwa ujumla Simba wanawafahamu vizuri walinzi wao binafisi ".
Bwana Sharma anasema wanafahamika kwa tabia yao ya maisha ya kijamii: "Si kama Mbwa, hawatoi kucha au kutikisa mikia, lakini wanawatambua walinzi wanaowaona kila siku.."
Maafisa wa wanayama pori wanasema kwa ujumla watoto wa simba ni wategemezi mno wa mama zao kwa ajili ya maisha yao hadi wanapofikia umri wa miaka miwili na nusu hadi mitatu.
Mtoto huyo wa simba mwenye umri wa miezi 15, kwa sasa yuko chini ya uangalizi wa maafisa wa misitu.
"Mama yake, Rupa, alionekana kuwa mpweke na aliwinda peke yake,Lakini kwa sasa simba huyo jike ametoweka, tunatarajia mtoto huyo wa simba atajiunga na kundi lingine, au simba mwingine jike huenda akaanza kumtunza," amesema Bwana Sharma.

Kenya katika hatari ya kupata Ebola

0 maoni

Afisa wa shirika la afya duniani aeleza kuhusu janga la Ebola Duniani
Shirika la afya duniani, limetahadharisha kuwa Kenya inaweza kuwa katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa wa Ebola, kutokana na kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo.
Hatari hii inatokana na Kenya kuwa kitovu cha usafiri wa ndege huku wasafiri wengi wanaokwenda Afrika Magharibi wakipitia nchini humo.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa onyo ya afisaa mkuu wa shirika la afya duniani WHO.
Hili ndilo onyo kali zaidi kuhusiana na ugonjwa wa Ebola kutolewa na shirika la WHO kwamba Ebola huenda ikaenea katika kanda ya Afrika Mashariki.
Wataalamu wa afya wanasema kwamba wanajitahidi kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo Afrika Magharibi, ambako zaidi ya watu 1,000 wamefariki.
Canada imesema kwamba itatoa mchango wa dozi 1000 za chanjo ya majaribio ya Ebola kusaidia watu kutoambaukizwa ugonjwa huo.
Kisa cha kwanza cha Ebola,kiliripotiwa nchini Guinea mwezi Februari kabla ya kuenea hadi nchini Sierra Leone na Liberia.
Nigeria ni nchi yenye idadi kuwba ya watu barani Afrika na ndio ya hivi karibuni kuripoti kuwa na thuluthi moja ya vifo kutokana na Ebola.
Kisa cha tatu kiliripotiwa siku ya Jumanne.
Mkurugenzi wa shirika la afya duniani tawi la Kenya, Custodia Mandlhate, amesema kuwa nchi hiyo iko katikahatari kubwa ya kupata Ebola.
Hatua za kuzuia maambukizi na kuweza kutambua wagonjwa zimeshika kasi mjini Nairobi katika siku za hivi karibuni.
Serikali hata bhivyo imesema kuwa haitasitisha safari za ndege kutoka katika nchi nne zilizokumbwa na ugonjwa huo Afrika Magharibi.
"Hatushauri, safari za ndege kusitishwa kwa sababu ya mipaka yetu ambayo watu wanaingia na kutoka pasipo vikwazo vingi, '' alisema waziri wa afya James Macharia.
Kenya hupokea zaidi bya safari 70 za ndegekuoka Afrika Magharibi.
Shirika la kikanda la Ecowas, limesema kuwa mmoja wa maafisa wake Jatto Asihu Abdulqudir, mwenye umri wa miaka 36, alifariki kutokana na Ebola nchini Nigeria.

Afutiwa kosa la kutorosha pesa Syria

0 maoni

Nawal aliambia mahakama kua alishauriwa kubeba pesa hizo na rafiki yake bila kumweleza zilikokuwa zinakwenda
Mahakama nchini Syria imefutilia mbali kesi ya mwanamke aliyeshitakiwa kwa madai ya kutorosha pesa kwenda Syria kwa kuzificha katika nguo ya ndani.
Ila rafiki yake amepatikana na hatia ya kosa la kufadhili ugaidi.                                                                                                                                                              
Mwanamke huyo kwa jina Nawal Msaad alituhumiwa kwa kutorosha pauni 15,800 ndani ya nguo zake za ndani kuingia nchini Syria, amefutiwa makosa baada ya kukosekana ushahidi.
Nawal Msaad, mwenye umri wa miaka 27, kutoka London, alisimamishwa katika uwanja wa ndege wa Heathrow alipokuwa anajaribu kupanda ndege kwuelekea mjini Istalbul nchini Uturuki.
Pesa hizo inadiwa alidhamiria kumpwa mwanamke raia wa Uingereza,nchini Syria.
Mwenzake Amal El-Wahabi, mwenye umri sawa na wake, alituhumiwa kwa kosa la kujaribu kuingiza pesa Syria kimagendo kwa lengo la kufadhili ugaidi.
Viongozi wa mashitaka wanasema kuwa mumewe El-Wahabi alijiunga na wapiganaji wa kiisilamu nchini Syria.
Bi Msaad, alikuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Metropolitan mjini London akisema kuwa alikuwa amehadaiwa na mwenzake El-Wahabi.
Alisema alificha pesa hizo ili zisiibwe lakini akasema aliziingiza katika nguo yake ya ndani tu kwa sababau hiyo.
Mahakama ilimpata na hatia El-Wahabi kwa kumshawishi rafiki yake kubeba pesa hizo ili kumkabidhi mumewe aliye vitani nchini Syria.
Alipoachiliwa na mahakama aliangua kilio na kuondoka kwa haraka mahakamani huku mwenzake akipatikana na hatia na huenda akafungwa jela kwa miaka 14.

CAR:Waasi wataka nchi kugawanywa

0 maoni


  • Google+
  • Chapisha


  • kundi la wapiganaji nchini CAR
    Waasi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR wamekataa makubaliano ya kusitsisha vita na kutaka taifa hilo ligawanywe kati ya Waislamu na Wakristo.
    Afisa mkuu wa waasi wa kundi la kiislamu la Seleka ameiambia BBC kwamba wapiganaji wake watapuuza makubaliano hayo yalioafikiwa siku ya jumatano kwa kuwa yalifanywa bila wao kuhusishwa.
    Joseph Zoundeiko amewalaumu Wakristo wa Kusini mwa taifa hilo kwa kushindwa kuleta amani na kusema kuwa taifa hilo ni sharti ligawanywe mara mbili.
    Mapigano ya miezi kadhaa kati ya makundi ya Wakristo na yale ya Waislamu katika taifa hilo yamesababisha mauaji ya maelfu ya watu huku mamilioni wakiwachwa bila makao.
    Kundi la waasi wa Seleka lilivunjwa rasmi mwaka uliopita.
    lakini kundi la Human Rights Watch linasema kuwa wapiganaji hao wameelekea katika maeneo ya mashambani na kwamba wameanza kuzishambulia jamii za Wakristo.
    Wakristo na wamelipiza kisasi na hivyobasi kusababisha maafa zaidi kutoa pande zote mbili.

    Juhudi za kutafuta amani Gaza zachacha

    0 maoni

    Wapalestina zaidi ya 800 wameuawa na Waisraeli 35
    Israeli imeendelea kuivirumishia makombora Gaza kucha kutwa ,huku kikao cha mawaziri wa baraza la Usalama kikitarajiwa huko Marekani kujadili mapendekezo mapya ya wito wa kusitishwa mapigano kwa misingi ya kibinadamu.
    Afisa wa ngazi ya juu wa umoja wa mataifa aliyeko Gaza Bob Turner, ameiambia BBC kuwa wapalestina laki moja unusu , ambao ni asilimia 8 ya idadi ya watu wa Gaza sasa wamekimbilia hifadhi kwenye shule za Umoja wa mataifa.
    Idadi ya raia wa Palestina waliouawa imezidi mia nane, huku mashambulio hayo ya Israel ya angani majini na ardhini yakiingia siku ya kumi na nane.
    Wanajeshi 32 na raia watatu wa Israel wameuawa katika muda huo.
    Katika ukingo wa magharibi, na Jerusalem mashariki raia wawili wa Palestina wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa wakati waandamanaji waliokuwa na hasira kuhusu mashambulio huko Gaza walipokabiliana na vikosi vya Israel.
    Maandamano yaendelea Gaza kupinga mashambulizi ya Israeli
    Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon anasema ameshtushwa na kushambuliwa kwa shule ya Umoja huo iliyopo huko Beit Hanoun, ambako mamia ya watu walifika kutafuta hifadhi.
    Hata hivyo Bwana Moon na waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani John Kerry wanaendeleza juhudi za kutafuta makubaliano ya kusitisha vita.
    Kerry alikuwa Cairo kukutana na waziri wa maswala ya kigeni wa Misri Sameh Shoukry na Ban Ki-moon ambapo wanajaribu kuishinikiza Hamas kukubali mwito wa kusitisha mapigano bila ya kuishinikiza Isareli kuondoa vikosi vyake katika ukanda wa Gaza.
    Wapalestina wakabiliana na polisi Gaza kupinga uvamizi wa Israeli
    Israeli iliishambulia Gaza Julai tarehe 8 ikitafuta mbinu za kuzima mashambulizi ya makombora ya Hamas yanayotokea Gaza.
    Mapema leo maandamano makubwa yalifanyika katika ukingo wa Magharibi mwa Palestina karibu na mpaka wake na Israel kupinga mashambulio yanayofanywa na Israel.
    Waandamanaji hao wakiwa na hasira walipambana na vikosi vya usalama vya Israel.
    Hata hivyo mapambano makubwa dhidi ya vikosi vya usalama ilikuwa katika eneo la Qalandia katika mpaka wa Ramallah and Jerusalem.

    DUDE, TINO MBARONI NCHINI KENYA . BOFYA HAPA KUJUA CHANZO NI NINI

    0 maoni


    ASANII nyota wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ na Hisan Muya ‘Tino’ hivi karibuni walitiwa mbaroni katika mji wa Kilifi ulio mbele ya Mombasa nchini Kenya baada ya kukutwa wakipiga picha za filamu yao bila kuwa na kibali.
    Msanii nyota wa filamu Bongo, Hisan Muya ‘Tino’.
    Hata hivyo, waigizaji hao baadaye waliachiwa, ingawa hali ilikuwa ngumu kidogo kwa Tino, ambaye polisi wa Kenya walidai hakuwa Mtanzania, bali ni raia wa Somalia.
    Dude alithibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema liliwatokea kutokana na mazoea ya huku nyumbani ambako hufanya shughuli zao za kupiga picha za filamu zao bila kuhitaji kibali.
    Msanii nyota wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’.
    “Yaani tumepata aibu ya mwaka, kwani tulienda kushuti bila kuomba kibali kutokana na mazoea ya huku kwetu Bongo, tulipekuliwa sisi na gari letu, baada ya hapo kibali kikaletwa nikaachiwa lakini Tino waliendelea kumshikilia wakisema ni Msomali mpaka mkuu wa shirikisho la filamu Mombasa alipokuja kuokoa jahazi, ukweli Kenya hakufai,”alisema Dude.

    Mwanamke aliyeasi dini akamatwa tena

    0 maoni
    Taarifa kutoka nchini Sudan zinasema kuwa mwanamke aliyeachiliwa hapo jana kwa kosa la kuasi dini amekamatwa tena.
    Mwanamke huyo Meriam Ibrahim, alikuwa amehukumiwa kifo kwa kosa la kuolewa na mwanamume mkristo na kukana dini ya kiisilamu alikamatwa akiwa na familia yake katika uwanja wa ndege mjini Khartoum.
    Watu waliomkata walikuwa wamevalia mavazi ya kiraia ingawa wanaaminika kuwa wanajeshi wa serikali.
    Duru zinasema kuwa Meriam Ibrahim aliyejifungulia jela alikuwa anajiandaa kuondoka nchini Sudan pamoja na familia yake.
    Haijulikani kwa nini alikamatwa na karibu watu arobaini waliokuwa wamavalia mavazi ya kiraia siku moja tu baada ya kuachiliwa kuambatana na uamuzi wa mahakama ya rufaa.
    Meriam alikamatwa kwa mara ya kwanza mwezi Februari na kujifungulia mtoto wake msichana jela baada ya kuhukumiwa.
    Alikamatwa mara ya kwanza mwezi Februari na kujifungulia mtoto wake msichana jela punde baada ya kuhukumiwa.
    Familia yake imepelekwa katika makao makuu ya idara ya ujasusi.
    Kabla ya kuzuiliwa kwaketena, jamii ya kimataifa yalipongeza uamuzi wa kuachiliwa kwake na kumuondolea hukumu ya kifo chake.

    Binti Aliyeng'atwa Mwili Mzima na Bosi Wake Atoa Siri Nzito

    0 maoni
    Stori: Haruni Sanchawa
    NYUMAya pazia! Yule msichana Yusta Lucas (20) mwenyeji wa Mkoa wa Tabora ambaye alifika jijini Dar kufanya kazi ya u-hausigeli na kufanyiwa ukatili wa kutisha na bosi wake kisha habari zake kuandikwa, ametoa siri nzito, Uwazi limemegewa.
    Akizungumza kwa uchungu na gazeti hili akiwa wodini kwenye Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu Kinondoni, Mwananyamala jijini Dar, Yusta ambaye amefanya kazi kwa tajiri yake huyo kwa miaka mitatu alisema:
    “Kwanza nataka watu wajue kuwa mwajiri wangu ni binamu yangu, alinileta hapa Dar kwa ajili  ya kumsaidia kazi za ndani pamoja na kumlelea mwanaye.
    “Kipigo hasa kilianza mwanzoni mwa mwaka huu ikiwa ni pamoja na kuning’ata kwa meno mwili mzima, ndiyo maana mwili wangu wote unaonekana una mabakamabaka.
    “Mateso yangu majirani walikuwa wakiyajua kutokana na kilio changu lakini walikuwa wanashindwa kunisaidia kwa sababu ya ushirikiano mdogo.
    “Kwanza nashangaa sana kwa adhabu yake ya kuning’ata meno mpaka damu zinabaki kwake. Je, kama nina virusi vya Ukimwi si na yeye anavipata?
    “Sijajua alikuwa anapata wapi ujasiri wa kuning’ata meno. Kwa kweli nimeteseka kwa muda mrefu sana. Mungu ndiye anajua, lakini nawashukuru sana majirani walioliona hilo na kuamua kuchukua hatua.”
    KUHUSU MAISHA YA TAJIRI WAKE
    Aidha, Yusta alianika mienendo mitano ya bosi wake huyo na kusema imekuwa ikimshangaza sana.
    MWENENDO WA KWANZA
    “Mimi katika kuishi kwangu pale sijawahi kumwona jirani yeyote amekuja ndani kusalimia wala yeye kwenda kwa jirani kufanya hivyo jambo ambalo si la kawaida.”
    MWENENDO WA PILI
    “Yeye (bosi wake) hana mume. Lakini tangu nimeishi pale kwa miaka mitatu sijawahi kumwona mwanaume ameingia ndani ya nyumba achilia mbali wanawake wenzake, hata mgeni. Kifupi yeye ni yeye kwa pale nyumbani kama ana marafiki labda wanakutana mbali.”
    MWENENDO WA TATU
    “Muda wake wa kurudi nyumbani siku zote ni usiku mnene, amewahi sana ni saa mbili usiku. Kwa hiyo, muda mwingi mimi ndiyo huwa nyumbani.”
    MWENENDO WA NNE
    “Anajiweza, sijui kwa nini aliamua kunifanyia hivi. Maana mtu ana gari, anaendesha mwenyewe na anasema ana hela, ndiyo maana namshangaa kuniadhibu kwa kuning’ata kwa meno.”
    MWENENDO WA TANO
    “Sikumbuki lini nimewahi kumwona akicheka. Muda mwingi anaonekana amekasirika tu kiasi kwamba nimekuwa nikimwogopa siku zote.”
    OMBI KWA SERIKALI
    Yusta alisema kufuatia matatizo makubwa yaliyompata ameiomba  serikali imsaidie  aweze  kurudi nyumbani kwao Tabora.
    SHUKURANI KWA MAJIRANI
    Yusta alitoa shukurani kwa majirani  waliojitokeza kuokoa maisha yake ambapo alisema kama wasingekuwa wao hajui ingekuwaje.
    MANENO YA MUUGUZI
    Kwa upande wa hospitali hiyo, muuguzi  kiongozi  wa zamu siku hiyo, Mahija Swalehe alikemea tabia za waajiri wa wafanyakazi wa ndani kuwatesa na kuiomba serikali kuliangalia suala hilo kwa jicho la tatu ili kukomesha vitendo hivyo.
    TUJIKUMBUSHE
    Yusta alikumbwa na masaibu hayo kwa muda mrefu hadi hivi karibuni majirani wakiwa na polisi walipovamia nyumba hiyo na kumkamata bosi wake kisha kumpeleka Kituo cha Polisi cha Oysteraby, Dar ambako anashikiliwa na yeye kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala kwa matibu baada ya kukutwa na majeraha.
    Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Camillius Wambura amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa ametiwa mbaroni.
    -lucypatickm

    PICHA VURUGU ZA WAMACHINGA MWANZA MABOMU YA MACHOZI YARINDIMA ZAIDI YA SAA 3, BIASHARA ZAFUNGWA KABISA.

    0 maoni














    Mkuu wa jeshi aponea kifo Somalia

    0 maoni
    Jenerali Dahir anaendesha moja ya magari yenye uwezo mkubwa wa kudhibiti mashambulizi
    Mkuu wa jeshi la Somalia ameponea chupuchupu kuuawa mjini Mogadishu.
    Hili ndilo shambulio la punde zaidi katika msururu wa mashambulio dhidi ya viongozi wa serikali na rasilimali za serikali nchini humo.
    Gari lake Jenerali Dahir Aden Elmim lilirushiwa bomu katika barabara kuu karibu na afisi za wizara ya ulinzi mjini Mogadishu.
    Aliponea kwa sababu yeye huendesha mojawepo ya magari machache yaliyo na uwezo wa kudhibiti shambulio la risasi, ambayo yametengewa viongozi wakuu wa serikali hiyo.
    Hakuna yeyote aliyedai kuhusika na shambulio hilo kufikia sasa japo inafahamika kuwa kundi la Al shabaab limekuwa likifanya mashambulio ya mara kwa mara mjini Mogadishu.
    Mwishoni mwa juma, watu 15 waliuawa katika shambulio lililolenga jengo la bunge la Somalia. Wengine wengi walijeruhiwa wakiwemo wabunge 3.

    Mwanamke aliyehukumiwa kifo Sudan ajifungua

    0 maoni
    Meriam Yehya Ibrahim Ishag aliadhibiwa kwa makosa mawili, zinaa na kuasi dini
    Mwanamke aliyeasi dini nchini Sudan na kupata adhabu ya kifo amejifungua mtoto mvulana akiwa jela mjini Khartoum kwa mujibu wa wakili wake.
    Meriam Yehya Ibrahim Ishag, aliolewa na mwanamume mkristo jambo lililopelekea mwanamke huyo kuhukumiwa kifo mapema mwezi huu baada ya kukataa kusilimu tena.
    Ataruhusiwa kumnyonyesha mtoto wake kwa miaka miwili kabla ya hukumu kutekelezwa.
    Meriam aliyezaliwa na wazazi waisilamu, alihukumiwa na mahakama ya ya kiisilamu.
    'Mijeledi miamoja'
    Bi Ibrahim alihukumiwa kifo kwa kosa la zinaa kwa sababu ameolewa na mwanamume mkristo wa kutoka Sudan Kusini na kwamba ndoa yao haikubaliki chini ya sheria ya kiisilamu ambayo inasema kuwa mwanamke musilamu hawezi kuolewa na mwanamume mkristo.
    Kwa kosa hilo, jaji alimuhukumu adhabu ya mijeledi miamoja, adhabub ambayo itatelezwa pindi mama huyo atakapopata nafuu kutokana na kujifungua.
    Bi Ibrahim alilelewa kwa njia ya kikristo , dini ya mamake kwa sababu babake aliyekuwa muisilamu hakuwepo katika maisha yake tangu utotoni.
    Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Amnesty International, alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la Zinaa mwezi Agosti mwaka 2013, na mahakama ikamuongezea kosa la kuasi dini Februari 2014 aliposema kuwa yeye ni mkristo wala sio muisilamu.
    Sudan ina idadi kubwa ya waisilamu ambao wanafuata sheria za kiisilamu.

    Tanzania yasema M23 walitoka Rwanda

    0 maoni
    Tanzania kwa mara ya Kwanza imesema inayo uhakika kuwa waasi wa M23 walioondolewa nchini Jamuhuri ya Kongo ni ni raia Rwanda.Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Benard Membe ameliambia Bunge la Tanzania kuwa anao uhakika kuwa waasi M23 walitokea nchini Rwanda.
    Hii ni Mara kwanza kwa Tanzania kukiri hadharani kuwa inao uhakika kuwa waasi hao ni raia wa Rwanda.
    Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimepeleka majeshi Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo kwa kushirikiana na yale ya umoja wa Mataifa yaliwaondoa waasi hao DRC
    Benard Membe Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania
    Matamshi hayo ya Waziri huyo aliyatoa wakati alipokuwa akiwasilisha hotuba ya Bajeti ya Wizara yake ambapo pia alikiri kuwa bado uhusiano wa Tanzania na Rwanda sio mzuri.
    Hata hivyo upande wa Upinzani mlishambulia Waziri huyo wa Mambo ya nje Benard Membe wakidai kwamba Waziri huyo anachochea kuvurugika kwa uhusiano wa Watanzania na Rwanda kwa kuhisi kuwa M23 ni Wanyarwanda nahata kutaka achukuliwe adhabu kali.
    Mbali na tuhuma hizo Waziri Membe alizidi kusisitiza kuwa waasi wa M23 ni raia wa Rwanda akisema hiyo ni ripoti ya Umoja wa Mataifa.
    Mbali na waziri baadhi ya wabunge wanamuunga mkono waziri Membe kuwa waasi wa M23 ni raia wa Rwanda wao.
    Matamshi haya Waziri wa Tanzania kuhusu M23 bado haijulikana ni kwa namna gani utaathiri uhusiano wa Tanzania na Rwanda kama utakuwepo huenda ukajulikana hapo baadae.

    UNYAMA WA KUTISHA: MGANGA WA KIENYEJI AMNYONGA MTOTO WA DARASA LA KWANZA.....AMKATA MIKONO, SEHEMU ZA SIRI NA KUMZIKA CHINI YA KITANDA CHAKE

    0 maoni

    WAKATI jamii ya Watanzania ikipigwa butwaa na ukatili wa kutisha aliofanyiwa mtoto wa miaka minne kwa kufungiwa ndani ya boksi kwa miaka mitatu mjini Morogoro, ukatili mwingine wa kutisha dhidi ya watoto umeripotiwa mkoani Kagera.
    Katika mkoa huo, mganga wa kienyeji ametiwa mbaroni, akituhumiwa kumuua kwa kumnyonga, kumkata mikono na kumzika katika nyumba yake.
    Mganga huyo, Mujingwa John (20) amekiri mbele ya jeshi la polisi kuhusika na mauaji ya mtoto Fausta Geofrey (8), mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kitunga kata ya Muhutwe, wilayani Muleba.
    Anatuhumiwa kwamba, alimkamata kwa nguvu akienda shule na wenzake, akamuua, kumkata mikono, nyama ya mgongo, masikio na sehemu za siri kwa lengo la kuibanika na kutengeneza 'uchawi’ wake, kisha akachimba shimo na kuzika mwili ndani ya nyumba.
    Tukio hilo lilithibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, George Mayunga aliyesema mganga huyo alikamatwa na polisi kwa kushirikiana na wananchi, ambapo alikutwa akibanika viungo alivyovikata kutoka kwa mtoto huyo.
    Aidha, akiwa polisi, mganga huyo alipewa fursa ya kueleza kilichotokea mbele ya waandishi wa habari, ambapo alidai alifikia uamuzi wa kumuua mtoto huyo, kutokana na hali ngumu ya umaskini inayomkabili.
    Alisema baada ya kumkamata mtoto huyo, alimkaba shingo na kumvuta hadi katika nyumba aliyokuwa akiishi, akamnyonga hadi kufa na baada ya kufa, alimkata ngozi ya mgongoni, mikono akianzia na mkono wa kushoto aliodai una bahati, sehemu za siri na masikio.
    “Nilimkamata mtoto na kumuua, maana niliona nikikamata mtu mzima atanizidi nguvu na kupiga kelele,” alidai.
    Alidai kuwa, “Nilipomaliza kumuua nilichimba shimo chini ya kitanda changu nikamzika na kutandaza nyasi juu yake ili isigundulike kama eneo hilo kuna shimo".
    Mganga huyo aliyejitambulisha kuwa ni Msukuma, alidai viungo hivyo ambavyo hadi polisi wanafika, alikuwa bado akivikausha, angevichanganya na dawa ambayo angewapatia wateja wake ili iwasaidie kufanikisha mambo yao, ikiwamo kupata bahati na utajiri na alitarajia kuuza kwa Sh 500 kwa kila ujazo wa kijiko kimoja cha dawa yake.
    Alisema hiyo ni mara yake ya kwanza kufanya tukio la aina hiyo na kwamba alihamia Muleba mkoani Kagera miaka miwili iliyopita akitokea Nyanguge wilaya ya Magu mkoani Mwanza. Alisema alirithi uganga huo kutoka kwa babu yake mzaa mama na kuwa alianza uganga akiwa na umri wa miaka minane na hakuwahi kwenda shule.
    Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Bisole katika Kata hiyo wilayani Muleba, Khamis Hassan, akizungumzia tukio hilo baada ya mauaji hayo, alidai muuaji alimkata mtoto huyo mikono yake miwili kabla ya kumzika.
    Hassan alisema kuwa tukio hilo ni la Mei 21 mwaka huu asubuhi katika kijiji hicho, wakati mtoto huyo akiwa na wenzake wakielekea shuleni, ambapo inadaiwa aliitwa na kukamatwa na mganga huyo, aliyetambulika kwa jina la Mujingwa John (20).
    Alisema kuwa baada ya taarifa za mtoto huyo kutoonekana kuzagaa, wanakijiji walikusanyana na kuanza msako, ambapo walikamata kundi la watu waliokuwa wakiwahofia kuhusika, hasa vijana.
    Alisema baada ya kuwakamata watu hao, waliwaweka sehemu moja na kuwaita wanafunzi waliokuwa na marehemu, ambapo walimtambua mganga huyo kuwa ndiye aliyemwita na kumkamata mtoto huyo.
    Mtendaji huyo alidai baada ya mganga huyo kutambuliwa, wananchi na polisi waliofika eneo hilo, walikwenda naye hadi katika nyumba anayoishi na kumtaka awaonyeshe alipo mtoto huyo. Alidai baada ya kumbana, aliwaonesha sehemu alikomzika, ambapo walichukua jembe na kuanza kufukua mwili wa mtoto huyo, uliokuwa umezikwa ndani ya nyumba aliyoishi mganga huyo.
    Alidai baada ya mganga huyo kumuua mtoto huyo, alimkata mikono yake miwili na kisha kuchimba shimo ndani ya nyumba, ambapo baada ya kumzika alifukia shimo akatandaza nyasi juu yake na kisha kuweka kitanda chenye godoro alilokuwa akilala.
    Alisema kuwa alipohojiwa ili kujua nani kamtuma kutekeleza unyama huo, mganga huyo alidai ilitokana na yeye kuoteshwa na mizimu yake, iliyomtaka kumuua mtoto ili amkate viungo vyake kwa ajili ya kuchanganya na dawa.
    Alisema mikono hiyo alitaka kuibanika kwenye moto ili aichanganye na dawa, ambayo angewapatia watu wanaohitaji kupata utajiri. Tukio hilo limekuja siku chache wakati Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, likiendelea na uchunguzi wa kilichotokea mpaka mtoto mmoja mkoani hapa , akateswa na mama mlezi kwa kuwekwa katika boksi tangu akiwa na miezi tisa, mpaka alipotimiza miaka minne.

    Credit: Habari leo