Japan ikotayari kutoa dawa ya Ebola
WEKA TANGAZO
WEKA TANGAZO

Serikali ya japan inasema kuwa itatoa dawa kuwatibu wagonjwa wa Ebola
Serikali ya Japan imesema iko
tayari kutoa dawa waliotengeneza ya kupambana na homa kali iitwayo T-705
ambayo huenda ikasaidia katika vita vya kupambana na Homa ya EBOLA.
Matumizi ya dawa hiyo hayajaidhinishwa na
shirika la afya duniani World Health Organisation, haijabainika iwapo
itafaa kutoa afueni kwa wagonjwa wa Ebola au la .
Msemaji wa kampuni inayotengeneza
dawa hiyo T-705 iitwayo Toyama Chemicals, anaeleza kuwa dawa hiyo ina
uwezo wa kukabiliana na virusi vinavyosababisha homa kali hivyo huenda
ikasaidia katika mapambano dhidi ya Ebola.

Serikali ya japan inasema kuwa itatoa dawa kuwatibu wagonjwa wa Ebola
Takao Aoki msemaji wa kampuni ambayo
imetengeneza dawa hiyo, alisema kwamba dawa hiyo iliyotengenezwa ili
kutibu virusi vya mafua vinavyojitokeza tena baada ya matibabu na vile
visivyo vya kawaida ilipitishwa na wizara ya afya ya Japan katika mwezi
wa Machi.
Akiongeza alisema kwamba Kampuni hiyo ya
Fujifilm inafanya mazungumzo na utawala wa chakula na dawa Marekani juu
ya kupimwa uwezo wa dawa hiyo kuhusiana na matibabu ya Ebola.
Kwa sasa hamna dawa wala chanjo yoyote
iliyothibitika na kuidhinishwa kutibu Ebola, lakini kutokana na janga la
mlipuko wa Ebola huko Afrika magharibi na sasa Jamhuri ya Kidemocrasi
ya Congo, Shirika la afya duniani WHO limesema itakubali matumzi ya dawa
za majaribio kwa wagonjwa, ilimradi utaratibu na masharti waliyoyaweka
yafuatwe na wagonjwa wenyewe wahusishwe katika kutoa idhini .
Majuzi wamarekani wawili waliokuwa wamethibishwa kuugua Ebola walipona baada ya kupewa dawa ya majaribio iitwayo ZMapp.

Daktari aliyepona Ebola baada ya kutibiwa na dawa ya Zmapp.
Yoshihide Suga ambaye ni katibu mkuu baraza la
mawaziri aliwaambia wandishi wa habari kwamba Japan inawezapeana dawa
hiyo wakati wowote WHO itakapoaagiza.
Aliongezea kusema kwamba Japan inangoja maelezo
zaidi ya uamuzi wa WHO kuhusu matumizi ya dawa ambazo hazijajaribiwa
lakini katika kesi yoyote ya dharura, Japan inaweza ikajibu maagizo
yoyote ya kibinafsi hata kabla ya uamuzi wowote wa WHO.
Mapema mwezi huu WHO ilisema kwamba ni sawa
kutumia dawa ambazo hazijajaribiwa kwa wagonjwa wa Ebola kutokana na
mlipuko wa ugonjwa huo.
0 maoni: