Afutiwa kosa la kutorosha pesa Syria
WEKA TANGAZO
WEKA TANGAZO
Mahakama nchini Syria imefutilia
mbali kesi ya mwanamke aliyeshitakiwa kwa madai ya kutorosha pesa
kwenda Syria kwa kuzificha katika nguo ya ndani.
Ila rafiki yake amepatikana na hatia ya kosa la kufadhili ugaidi.
Mwanamke huyo kwa jina Nawal Msaad
alituhumiwa kwa kutorosha pauni 15,800 ndani ya nguo zake za ndani
kuingia nchini Syria, amefutiwa makosa baada ya kukosekana ushahidi.
Nawal Msaad, mwenye umri wa miaka 27, kutoka
London, alisimamishwa katika uwanja wa ndege wa Heathrow alipokuwa
anajaribu kupanda ndege kwuelekea mjini Istalbul nchini Uturuki.
Pesa hizo inadiwa alidhamiria kumpwa mwanamke raia wa Uingereza,nchini Syria.
Mwenzake Amal El-Wahabi, mwenye umri sawa na
wake, alituhumiwa kwa kosa la kujaribu kuingiza pesa Syria kimagendo kwa
lengo la kufadhili ugaidi.
Viongozi wa mashitaka wanasema kuwa mumewe El-Wahabi alijiunga na wapiganaji wa kiisilamu nchini Syria.
Bi Msaad, alikuwa mwanafunzi katika chuo kikuu
cha Metropolitan mjini London akisema kuwa alikuwa amehadaiwa na
mwenzake El-Wahabi.
Alisema alificha pesa hizo ili zisiibwe lakini akasema aliziingiza katika nguo yake ya ndani tu kwa sababau hiyo.
Mahakama ilimpata na hatia El-Wahabi kwa
kumshawishi rafiki yake kubeba pesa hizo ili kumkabidhi mumewe aliye
vitani nchini Syria.
Alipoachiliwa na mahakama aliangua kilio na
kuondoka kwa haraka mahakamani huku mwenzake akipatikana na hatia na
huenda akafungwa jela kwa miaka 14.
0 maoni: