CAR:Waasi wataka nchi kugawanywa
WEKA TANGAZO
Twitter
Google+
Tuma kwa rafiki yako
Chapisha
WEKA TANGAZO
Waasi katika Jamhuri ya Afrika
ya Kati CAR wamekataa makubaliano ya kusitsisha vita na kutaka taifa
hilo ligawanywe kati ya Waislamu na Wakristo.
Afisa mkuu wa waasi wa kundi la kiislamu la
Seleka ameiambia BBC kwamba wapiganaji wake watapuuza makubaliano hayo
yalioafikiwa siku ya jumatano kwa kuwa yalifanywa bila wao kuhusishwa.
Joseph Zoundeiko amewalaumu Wakristo
wa Kusini mwa taifa hilo kwa kushindwa kuleta amani na kusema kuwa
taifa hilo ni sharti ligawanywe mara mbili.
Mapigano ya miezi kadhaa kati ya makundi ya
Wakristo na yale ya Waislamu katika taifa hilo yamesababisha mauaji ya
maelfu ya watu huku mamilioni wakiwachwa bila makao.
Kundi la waasi wa Seleka lilivunjwa rasmi mwaka uliopita.
lakini kundi la Human Rights Watch linasema kuwa
wapiganaji hao wameelekea katika maeneo ya mashambani na kwamba
wameanza kuzishambulia jamii za Wakristo.
Wakristo na wamelipiza kisasi na hivyobasi kusababisha maafa zaidi kutoa pande zote mbili.
0 maoni: