Genge
la wezi wa kompyuta limefanikiwa kuiba takriban dola bilioni moja
kutoka kwenye akaunti za wateja wa mabenki 100 katika mataifa 30.
Kampuni
inayosimamia usalama wa programu ya kompyuta inayohakikisha data ya
wateja iko salama Kaspersky Lab imesema katika ripoti yake maalum.
Ripoti
hiyo inaelezea mbinu mpya ya wezi wa Kompyuta wanaotumia mbinu mpya ya
kudakua nambari za akaunti za wateja za siri kabla ya kuingia na kupora
pesa .
Kaspersky imesema kuwa wizi huo ulianza mwaka wa 2013 na
bado unaendelea hata leo kwani mabenki yote yalioathirika hayana uwezo
wa kuwazuia wezi hao .
Hadi kufikia sasa ripoti hiyo inadai kuwa takriban dola bilioni moja zimeporwa kutoka kwenye akaunti za wateza.
Genge hilo la wezi, lililoanzia shughuili yake nchini Urusi, Ukraine na pia Uchina ndilo linalolaumiwa kwa wizi huo.
Kampuni
hiyo ya Kaspersky inasema inafanya juhudi za kuzima wizi huo kwa
ushirikiano na polisi wa kimataifa Interpol na polisi wa bara ulya
Europol . Kwa mujibu wa ripoti hiyo mabenki katika mataifa 30
yakiwemo, Russia, Marekani , Ujerumani , Uchina, Ukraine na Canada
yameathirika pakubwa.
Wezi walitumia programme ya kipekee
Kamanda wa kikosi cha polisi wa
kimataifa Interpol bwana Sanjay Virmani, amesema kuwa wezi wataendelea
kutumia upungufu wa miundo msingi katika sekta ya uchumi wa mataifa
husika hadi pale kutaibuka umoja wa kuzuia mapengo.
Kaspersky hata hivyo inasema kuwa genge hilo linalenga mabenki bila ya kuwaibia watu binafsi.
genge
hilo kwa jina Carbanak, linatumia mbinu ya kuambukiza virusi kwenye
mashine za benki ikiwemo kamera za CCTV ilikunakili kila kitu
kinachoandakiwa kwenye kompyuta.
Kutokana na uweledi wao genge
hilo lilituma pesa kwenye account zao huku wengine wakiamrisha mmitambo
ya kutoa pesa ATM kumimina pesa bila kikomo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo kila tukio la wizi lilihusisha takriban dola milioni kumi.
0 maoni: