UNYAMA WA KUTISHA: MGANGA WA KIENYEJI AMNYONGA MTOTO WA DARASA LA KWANZA.....AMKATA MIKONO, SEHEMU ZA SIRI NA KUMZIKA CHINI YA KITANDA CHAKE
WEKA TANGAZO
WAKATI jamii ya Watanzania ikipigwa butwaa na ukatili wa kutisha aliofanyiwa mtoto wa miaka minne kwa kufungiwa ndani ya boksi kwa miaka mitatu mjini Morogoro, ukatili mwingine wa kutisha dhidi ya watoto umeripotiwa mkoani Kagera.
WEKA TANGAZO
WAKATI jamii ya Watanzania ikipigwa butwaa na ukatili wa kutisha aliofanyiwa mtoto wa miaka minne kwa kufungiwa ndani ya boksi kwa miaka mitatu mjini Morogoro, ukatili mwingine wa kutisha dhidi ya watoto umeripotiwa mkoani Kagera.
Katika
mkoa huo, mganga wa kienyeji ametiwa mbaroni, akituhumiwa kumuua kwa
kumnyonga, kumkata mikono na kumzika katika nyumba yake.
Mganga
huyo, Mujingwa John (20) amekiri mbele ya jeshi la polisi kuhusika na
mauaji ya mtoto Fausta Geofrey (8), mwanafunzi wa darasa la kwanza
katika Shule ya Msingi Kitunga kata ya Muhutwe, wilayani Muleba.
Anatuhumiwa
kwamba, alimkamata kwa nguvu akienda shule na wenzake, akamuua, kumkata
mikono, nyama ya mgongo, masikio na sehemu za siri kwa lengo la
kuibanika na kutengeneza 'uchawi’ wake, kisha akachimba shimo na kuzika
mwili ndani ya nyumba.
Tukio
hilo lilithibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, George
Mayunga aliyesema mganga huyo alikamatwa na polisi kwa kushirikiana na
wananchi, ambapo alikutwa akibanika viungo alivyovikata kutoka kwa mtoto
huyo.
Aidha,
akiwa polisi, mganga huyo alipewa fursa ya kueleza kilichotokea mbele
ya waandishi wa habari, ambapo alidai alifikia uamuzi wa kumuua mtoto
huyo, kutokana na hali ngumu ya umaskini inayomkabili.
Alisema
baada ya kumkamata mtoto huyo, alimkaba shingo na kumvuta hadi katika
nyumba aliyokuwa akiishi, akamnyonga hadi kufa na baada ya kufa,
alimkata ngozi ya mgongoni, mikono akianzia na mkono wa kushoto aliodai
una bahati, sehemu za siri na masikio.
“Nilimkamata mtoto na kumuua, maana niliona nikikamata mtu mzima atanizidi nguvu na kupiga kelele,” alidai.
Alidai kuwa, “Nilipomaliza
kumuua nilichimba shimo chini ya kitanda changu nikamzika na kutandaza
nyasi juu yake ili isigundulike kama eneo hilo kuna shimo".
Mganga
huyo aliyejitambulisha kuwa ni Msukuma, alidai viungo hivyo ambavyo
hadi polisi wanafika, alikuwa bado akivikausha, angevichanganya na dawa
ambayo angewapatia wateja wake ili iwasaidie kufanikisha mambo yao,
ikiwamo kupata bahati na utajiri na alitarajia kuuza kwa Sh 500 kwa kila
ujazo wa kijiko kimoja cha dawa yake.
Alisema
hiyo ni mara yake ya kwanza kufanya tukio la aina hiyo na kwamba
alihamia Muleba mkoani Kagera miaka miwili iliyopita akitokea Nyanguge
wilaya ya Magu mkoani Mwanza. Alisema alirithi uganga huo kutoka kwa
babu yake mzaa mama na kuwa alianza uganga akiwa na umri wa miaka minane
na hakuwahi kwenda shule.
Ofisa
Mtendaji wa Kijiji cha Bisole katika Kata hiyo wilayani Muleba, Khamis
Hassan, akizungumzia tukio hilo baada ya mauaji hayo, alidai muuaji
alimkata mtoto huyo mikono yake miwili kabla ya kumzika.
Hassan
alisema kuwa tukio hilo ni la Mei 21 mwaka huu asubuhi katika kijiji
hicho, wakati mtoto huyo akiwa na wenzake wakielekea shuleni, ambapo
inadaiwa aliitwa na kukamatwa na mganga huyo, aliyetambulika kwa jina la
Mujingwa John (20).
Alisema
kuwa baada ya taarifa za mtoto huyo kutoonekana kuzagaa, wanakijiji
walikusanyana na kuanza msako, ambapo walikamata kundi la watu waliokuwa
wakiwahofia kuhusika, hasa vijana.
Alisema
baada ya kuwakamata watu hao, waliwaweka sehemu moja na kuwaita
wanafunzi waliokuwa na marehemu, ambapo walimtambua mganga huyo kuwa
ndiye aliyemwita na kumkamata mtoto huyo.
Mtendaji
huyo alidai baada ya mganga huyo kutambuliwa, wananchi na polisi
waliofika eneo hilo, walikwenda naye hadi katika nyumba anayoishi na
kumtaka awaonyeshe alipo mtoto huyo. Alidai baada ya kumbana,
aliwaonesha sehemu alikomzika, ambapo walichukua jembe na kuanza kufukua
mwili wa mtoto huyo, uliokuwa umezikwa ndani ya nyumba aliyoishi mganga
huyo.
Alidai
baada ya mganga huyo kumuua mtoto huyo, alimkata mikono yake miwili na
kisha kuchimba shimo ndani ya nyumba, ambapo baada ya kumzika alifukia
shimo akatandaza nyasi juu yake na kisha kuweka kitanda chenye godoro
alilokuwa akilala.
Alisema
kuwa alipohojiwa ili kujua nani kamtuma kutekeleza unyama huo, mganga
huyo alidai ilitokana na yeye kuoteshwa na mizimu yake, iliyomtaka
kumuua mtoto ili amkate viungo vyake kwa ajili ya kuchanganya na dawa.
Alisema
mikono hiyo alitaka kuibanika kwenye moto ili aichanganye na dawa,
ambayo angewapatia watu wanaohitaji kupata utajiri. Tukio hilo limekuja
siku chache wakati Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, likiendelea na
uchunguzi wa kilichotokea mpaka mtoto mmoja mkoani hapa , akateswa na
mama mlezi kwa kuwekwa katika boksi tangu akiwa na miezi tisa, mpaka
alipotimiza miaka minne.
Credit: Habari leo
Credit: Habari leo
0 maoni: