Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo AFYA. Onyesha machapisho yote

MADHARA SABA KWA WANAUME WAOPENDA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE

0 maoni
Kama nilivyoelezea kwenye mada za wiki kadhaa zilizopita, mchezo huu unatumika sana katika mapenzi ya sasa, watoto wa mjini wana usemi wao kwa kitu kilichovuma kuwa ‘ndiyo habari ya mjini’.

Mchezo huu umekuwa ukipendwa sana na wanaume wengi ambao wengi wao huwa hawatumii kinga na kusababisha wengi kupata magonjwa ya zinaa pamoja na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Lakini mchezo wa kuruka ukuta umekuwa na madhara makubwa sana kwa wanaume wanaoufanya kwa muda mrefu.

Tulipoangalia upande wa wanawake, tuliona sehemu kubwa ya wanaopenda mchezo huu ni wanaume ambao wengine wamebatizwa majina ya ‘basha’, wakimaanisha mwanaume mpenda kuruka ukuta bila kuangalia ni wa mwanaume mwenzake au wa mwanamke.


Kwa vile nia ya kona hii ni kuelimisha madhara ya mtu kupenda kuruka
ukuta ili aache mara moja, tunaendelea kutoa elimu ya bure ili mtu yakimkuta ajue yamempata kwa kiburi chake na kwa kupenda starehe ya kipuuzi.

Madhara anayoyapata mwanaume anayependa mchezo huo ni kama ifuatavyo:

Kwanza: Husababisha kusinyaa au kuweka makovu kwenye njia ya haja ndogo.

Pili: Njia ya haja ndogo kuziba kiasi au kuziba kabisa.

Tatu: Kupata saratani (kansa) ya tezi za figo (prostate gland).

Nne: Kupata magonjwa sugu ya uti wa mgongo.

Tano: Kuharisha.

Sita: Maambukizi ya VVU ambapo mwisho wake ni Upungufu wa Kinga Mwilini (Ukimwi).

Saba: Baadaye mhusika kupata msongo wa mawazo au sonona kwa kujutia tendo hilo.

Nina imani ndugu yangu umeona madhara mabaya sana ya tabia hiyo mbaya. Inawezekana umezoea mchezo huo wa kuwaingilia wenzako na kuona raha lakini tumeona madhara yake, ambayo kwa hakika kama wewe ni mmoja wao, unatakiwa kuacha mara moja kwa vile mwisho wake ni majuto na mateso.

Jiepushe kuiga mambo bila kujua faida na hasara zake pia usimtie mwenzako majaribuni kwa kumlazimisha kuingia kwenye mchezo huo. Wanawake wengi wamekuwa wakilazimishwa na wanaume kuingiliwa kinyume na maumbile kwa kuwatishia kuwaacha kama watakataa.
Swali linakuja, kipi bora, kuharibiwa au kuachana?
Kumbuka baada ya kuharibikiwa, thamani yako hushuka na sifa yako ikiwafikia waharibifu wa watu, basi unageuzwa jamvi la mtaa na hatimaye unakufa kwa msongo wa mawazo au mateso ya ugonjwa utakaupata baada ya kukubali kuingiliwa kinyume na maumbile.

Unaweza kushangaa baada ya kuelezea madhara yanayowapata wanaume nimehamia kwa wanawake. Ukweli mchezo huu umewaathiri sana wanawake ambao wengi wanaujutia.

0 maoni
NI MAZOEZI GANI BORA KWA MWILI WAKO
Kila mwanadamu ana mwili tofauti na tunapaswa kufanya mazoezi kulingana na aina ya miili yetu.
Tujifunze njia tofauti za kufanya mazoezi Kulingana na miili wetu.
Je kuna uwezekano wa kuwa unaongeza uzito wako?
Kila mwili wa binadamu umeumbwa tofauti na kwa njia ya kipekee kama alama za vidole.
Hata hivyo tunaweza kutofautisha miili ya wanadamu kwa makundi matatu makubwa.
Tutafanya hivyo kulingana na uzito wa mwili, misuli na mafuta kwenye mwili.
Umuhimu wa kuelewa ni aina gani ya mazoezi unapaswa kufanya kuambatana na mwili wako unategemea na ujuzi ambao uko nao kuhusu mwili wako.
Tatizo ni kuwa "kuna mzozo unaojitokeza wakati wa kufanya mazoezi".
Kulingana na Juan Francisco Marco, profesa katika Kituo cha michezo na mafunzo cha Alto Rendimient kule Uhispania.
‘’Unapaswa kuamua iwapo utaboresha sura yako au utafanya mchezo iliongezea.
Kuna aina tatu za miili kulingana na chembe chembe za urithi na maumbile ya mwili wako.
Ectomorph: Watu wenye mwili na kifua chembamba
"Ectomorph"
Huyu kwa kawaida ni mrefu, mwembamba ana kifua chembamba na hupata wakati mgumu kuongeza uzito wa misuli yake, alielezea Profesa Marco.
Michezo ambayo anashiriki ni kama kukimbia ,kuogelea au kuendesha baiskeli ingawa Profesa Marco alionya ni vyema kufanya mazoezi ya kuongeza nguvu, kuongeza uzito na kujenga misuli.
Kundi hili linapaswa kuzingatia sana mazoezi ya kila mara ambapo misuli inasonga sana.
Endomorpho: Watu wenye mengi ya mwili
"Endomorph"
Huyu ni kinyume cha "Ectomorph", kundi hili hufanya mazoezi yakuongeza nguvu na uzito wa misuli, na hufanya mazoezi mara kwa mara.
Kundi hili lina mafuta mengi ya mwili, huonekana kuwa wanaweza kuwa wanariadha bila hata kujaribu.
Mesomorph: Wanamchezo wa kiasili
"Mesomorph"
Ni wanamchezo wa kiasili, chochote ambacho wanafanya huwa kizuri.
Marco anaelezea. Mazoezi bora kwa aina hii ya mwili ni kujihusisha katika mchezo ambao unaleta pamoja nguvu.
Kutokana na faida ambazo "Mesomorph" wanazo, Marco anasisitiza kuwa kundi hili bado linapaswa kuangaliwa kwa makini wanavyokula kwani wanauwezekano wa kuongeza uzito wa mwili ingawa si sana kama "Endomorph".

WAKUBWA TU...!!!! WATAFITI WABAINI MTINDO WA MWANAMKE KUWA JUU YA MWANAUME WAKATI WA TENDO LA NDOA NI HATARI KWA WANAUME!

0 maoni

Kwa mujibu wa utafiti huo, mtindo ambao mwanamke anakuwa juu ya mwanaume ndio hatari zaidi na huwa na risk kubwa zaidi ya kusababisha hata kuvunjika kwa uume.
Wanasayansi hao wanasema:
Pindi mwanamke anapokuwa juu, mara zote hucontrol movement na uzito wote wa mwili wake ukitua kwenye uume uliosimama na kushindwa kuzuia pale uume unapokuwa umeingia vibaya kwasababu madhara huwa ni madogo kwa mwanamke bila maumivu lakini ni mabaya kwa mwanaume.


“…Pindi mwanaume anapokuwa akicontrol movement, ana nafasi kubwa ya kuzuia kutokana na uume wake kuwa sehemu mbaya na hali inayopelekea kusikia maumivu na hivyo kupunguza hatari."

Mume wangu anawashwa sehemu zake za siri

0 maoni

Mimi ni dada niliyeolewa na nimebahatika kupata mtoto mmoja katika ndoa yangu na ana miaka 3, ila toka nimjue mume wangu, uwa anawashwa sehemu zake za siri, na tukiwa tumelala usiku utamsikia anajikuna tena kwa nguvu, ni kijaribu kuongea nae twende kwa dokta wa ngozi hataki, anasema nikawaida tu, ila mi ananiboa kitu kimoja anatoka kujikuna harafu anamshika mtoto bila kunawa.

Naombeni ushauri, au kama kuna dawa ya kupaka naweza nikanunua nikajaribu kumpaka, nampenda mume wangu ndo maana najaribu kutafuta njia mbadala

Japan ikotayari kutoa dawa ya Ebola

0 maoni

Serikali ya japan inasema kuwa itatoa dawa kuwatibu wagonjwa wa Ebola
Serikali ya Japan imesema iko tayari kutoa dawa waliotengeneza ya kupambana na homa kali iitwayo T-705 ambayo huenda ikasaidia katika vita vya kupambana na Homa ya EBOLA.
Matumizi ya dawa hiyo hayajaidhinishwa na shirika la afya duniani World Health Organisation, haijabainika iwapo itafaa kutoa afueni kwa wagonjwa wa Ebola au la .
Msemaji wa kampuni inayotengeneza dawa hiyo T-705 iitwayo Toyama Chemicals, anaeleza kuwa dawa hiyo ina uwezo wa kukabiliana na virusi vinavyosababisha homa kali hivyo huenda ikasaidia katika mapambano dhidi ya Ebola.
Serikali ya japan inasema kuwa itatoa dawa kuwatibu wagonjwa wa Ebola
Takao Aoki msemaji wa kampuni ambayo imetengeneza dawa hiyo, alisema kwamba dawa hiyo iliyotengenezwa ili kutibu virusi vya mafua vinavyojitokeza tena baada ya matibabu na vile visivyo vya kawaida ilipitishwa na wizara ya afya ya Japan katika mwezi wa Machi.
Akiongeza alisema kwamba Kampuni hiyo ya Fujifilm inafanya mazungumzo na utawala wa chakula na dawa Marekani juu ya kupimwa uwezo wa dawa hiyo kuhusiana na matibabu ya Ebola.
Kwa sasa hamna dawa wala chanjo yoyote iliyothibitika na kuidhinishwa kutibu Ebola, lakini kutokana na janga la mlipuko wa Ebola huko Afrika magharibi na sasa Jamhuri ya Kidemocrasi ya Congo, Shirika la afya duniani WHO limesema itakubali matumzi ya dawa za majaribio kwa wagonjwa, ilimradi utaratibu na masharti waliyoyaweka yafuatwe na wagonjwa wenyewe wahusishwe katika kutoa idhini .
Majuzi wamarekani wawili waliokuwa wamethibishwa kuugua Ebola walipona baada ya kupewa dawa ya majaribio iitwayo ZMapp.
Daktari aliyepona Ebola baada ya kutibiwa na dawa ya Zmapp.
Yoshihide Suga ambaye ni katibu mkuu baraza la mawaziri aliwaambia wandishi wa habari kwamba Japan inawezapeana dawa hiyo wakati wowote WHO itakapoaagiza.
Aliongezea kusema kwamba Japan inangoja maelezo zaidi ya uamuzi wa WHO kuhusu matumizi ya dawa ambazo hazijajaribiwa lakini katika kesi yoyote ya dharura, Japan inaweza ikajibu maagizo yoyote ya kibinafsi hata kabla ya uamuzi wowote wa WHO.
Mapema mwezi huu WHO ilisema kwamba ni sawa kutumia dawa ambazo hazijajaribiwa kwa wagonjwa wa Ebola kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo.

Kenya katika hatari ya kupata Ebola

0 maoni

Afisa wa shirika la afya duniani aeleza kuhusu janga la Ebola Duniani
Shirika la afya duniani, limetahadharisha kuwa Kenya inaweza kuwa katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa wa Ebola, kutokana na kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo.
Hatari hii inatokana na Kenya kuwa kitovu cha usafiri wa ndege huku wasafiri wengi wanaokwenda Afrika Magharibi wakipitia nchini humo.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa onyo ya afisaa mkuu wa shirika la afya duniani WHO.
Hili ndilo onyo kali zaidi kuhusiana na ugonjwa wa Ebola kutolewa na shirika la WHO kwamba Ebola huenda ikaenea katika kanda ya Afrika Mashariki.
Wataalamu wa afya wanasema kwamba wanajitahidi kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo Afrika Magharibi, ambako zaidi ya watu 1,000 wamefariki.
Canada imesema kwamba itatoa mchango wa dozi 1000 za chanjo ya majaribio ya Ebola kusaidia watu kutoambaukizwa ugonjwa huo.
Kisa cha kwanza cha Ebola,kiliripotiwa nchini Guinea mwezi Februari kabla ya kuenea hadi nchini Sierra Leone na Liberia.
Nigeria ni nchi yenye idadi kuwba ya watu barani Afrika na ndio ya hivi karibuni kuripoti kuwa na thuluthi moja ya vifo kutokana na Ebola.
Kisa cha tatu kiliripotiwa siku ya Jumanne.
Mkurugenzi wa shirika la afya duniani tawi la Kenya, Custodia Mandlhate, amesema kuwa nchi hiyo iko katikahatari kubwa ya kupata Ebola.
Hatua za kuzuia maambukizi na kuweza kutambua wagonjwa zimeshika kasi mjini Nairobi katika siku za hivi karibuni.
Serikali hata bhivyo imesema kuwa haitasitisha safari za ndege kutoka katika nchi nne zilizokumbwa na ugonjwa huo Afrika Magharibi.
"Hatushauri, safari za ndege kusitishwa kwa sababu ya mipaka yetu ambayo watu wanaingia na kutoka pasipo vikwazo vingi, '' alisema waziri wa afya James Macharia.
Kenya hupokea zaidi bya safari 70 za ndegekuoka Afrika Magharibi.
Shirika la kikanda la Ecowas, limesema kuwa mmoja wa maafisa wake Jatto Asihu Abdulqudir, mwenye umri wa miaka 36, alifariki kutokana na Ebola nchini Nigeria.

#UTAFITI : KULALA ZAIDI YA MASAA SABA NI HATARI KWA AFYA YAKO . SOMA HAPA KUJUA ZAIDI

0 maoni

Wakati ambapo tafiti za awali zilionesha kuwa kulala muda mrefu kunaweza kusaidia zaidi kuweka sawa afya zetu, tafiti mpya zimeonesha kuwa kulala zaidi ya masaa saba ni hatari sana kwa afya ya binadamu.

Utafiti uliofanywa na Shawn Youngstedt, Professor wa chuo kikuu cha Arizona State umebaini kuwa kulala zaidi ya masaa saba au chini ya masaa saba ni hatari kwa mwili wa binadamu.

Akiongea na Wall Street Journal, professor Shawn Youngstedt amesema kuwa alifanya utafiti kwa watu 9,000 na kubaini kuwa watu wenye umri kati ya miaka 50 hadi 64 waliolala chini ya masaa sita usiku au waliolala zaidi ya masaa nane wana matatizo ya kumbukumbu na uwezo mdogo wa kufanya maamuzi.

“The lowest mortality and morbidity is with seven hours,' says .But eight hours or more has consistently been shown to be hazardous,Just last month a study of almost 9,000 people found those aged 50 to 64 who slept for less than six hours a night - or more than eight - had worse memories and decision-making abilities.”

 Kwa hiyo tunashauriwa kulala kwa muda wa masaa saba tu usiku, sio chini ya hapo na sio zaidi ya hapo.

NJIA 10 TENA RAHISI TU ZA KUPUNGUZA UNENE,SOMA ZAIDI HAPA

0 maoni

UTANGULIZI. 

Ugali kwa samaki; mboga ya majani ya matango kwa nyanya. Usiweke chumvi kwenye hiyo mboga mbichi ya majani.




Ni makala muhimu sana. Wastani wa maisha ya Mtanzania ( na Waafrika wengi) hata wale waliosoma au wanaojiweza kiuchumi ni miaka 40-50. Kati ya sababu kuu zinazopunguza uhai wetu ni afya, unene na kutojua kujiangalia vyema afya zetu. 

1-ULAJI 
Ipo mifumo miwili ya kula. Chakula unachokula na namna unavyokila. 

Unavyokula. 
-Kuna kula vyakula vidogo vidogo vyenye madini, vitamini, mafuta nk mara nyingi kwa siku; au kula milo michache (mmoja au miwili) mikubwa ili kujaza tumbo. Ulaji mdogo mdogo husaidia afya na kuingia mwilini vyema kuliko ulaji mkubwa wa mara chache. 


Tumbo lina musuli zinazofanya kazi kama mashine au mnyama. Gari likijaa sana hupata taabu kwenda. Punda hivyo hivyo. Ulaji mdogo mdogo unaosambazwa mara kadhaa kwa siku ni bora maana mwili unachambua kila kitu kwa wepesi na haraka. Unapokula milo michache mikubwa unapalilia zaidi mafuta mwili. 
 
(PENDEKEZO la kwanza. 
Asubuhi, kunywa maji kwanza, matunda, kisha ndiyo chai na vitu vingine kama mkate au maandazi) 
· Wapo wanaodai kwamba wanakula matunda na mboga. 
Tatizo ni kwamba mipangilio yao huwa ya makosa. Mathalan wengi hula matunda baada ya chakula. 


Vimeng’enya chakula (enzymes) tumboni hufanya kazi namna tofauti. Mathalan vile vinavyonyambua matunda ni tofauti na vinavyomeng’enya vitu vigumu zaidi kama nyama au wanga. Matunda hunyambuliwa haraka zaidi kuliko vyakula vingine. 


Hivyo ni bora kula matunda dakika10-20 kabla ya chakula. Ukila baadaye matunda hugeuzwa aina fulani ya pombe (fermented food) inayoelea tu juu ya chakula na kubakia kitu kingine badala ya kuingizwa haraka ndani ya damu kupitia utumbo mdogo, uwengu, moyo, ini, nk. 

Tatizo jingine ni kupika sana mboga hadi zikapoteza nguvu. 
-Mseto wa vyakula pia ni muhimu. Kwa mfano vyakula vyenye uchachu (“acid”) na vile vinavyomumunyuka haraka (“alkaline”) havitakiwi viliwe pamoja. Mfano ni matunda. 
 

Matunda chachu kama machungwa, mananasi na maembe yatakiwa yawe pamoja; na yale laini zaidi: ndizi mbivu, matikiti maji, mapapai, matufaha, nk yaende kivyake, maana yana mfumo tofauti, wa kumeng’enywa. 




Hali hiyo pia iko katika nyama. Nyama nyeupe (ndege na samaki) tofauti na nyama nyekundu (ng’ombe, kondoo, nk) ziliwe tofauti. 

Chakula unachokula 
Watanzania/Waafrika hatuna tabia ya kula mboga mboga mbichi. Tunafuata ladha na mazoea kuliko thamani.


Bara letu lina mboga na vyakula bora kuliko bara lolote duniani lakini sisi tunakufa mapema na kwa utapia mlo kuliko wale wanaotoka nchi kame. Ulaya nzima imejazana mboga mboga zinazoagizwa toka Afrika. 


Kenya na Tanzania zinauza mboga za maharagwe mabichi (green beans), matunda toka Afrika Kusini na Ivory Coast; nk. Waafrika tunapenda kujaza matumbo. Unene umekithiri hata wale walio matajiri waliosoma bado wanakufa kwa kisukari shauri ya kutokula mboga mbichi. 

Ulaji wa mboga mbichi ni upi ?. 
Ni mathalani ulaji wa salad. Tanzania tunaita kachumbari. Lakini si lazima iwe kachumbari ya nyanya, vitunguu na chumvi tu. Waweza kuchanganya matango, nyanya kwa maparachichi; au vitunguu saumu, giligilani na karote. 


Huu mseto wa mboga mbichi ni mzuri ukienda na chakula chenye nyama za minofu na wanga (ugali, wali, ndizi za kupika nk). Ulaji wa wanga asubuhi, mchana na jioni kila siku huchangia sana katika unene. 
 
(PENDEKEZO LA 2. 
Ugali kwa samaki; mboga ya majani ya matango kwa nyanya. Usiweke chumvi kwenye hiyo mboga mbichi ya majani.) 

2-UNYWAJI MAJI 
Waafrika hatunywi maji, hasa wanawake. Wanaokunywa maji zaidi ni wacheza michezo. Wengi wetu hunywa zaidi soda (vinywaji baridi kama Cocacola, Pepsi, Mirinda ,Tangawizi na gesi za kisasa kama Red Bull) zilizojaa gesi inayoleta vidonda tumboni; na chai. Kuliko maji. 


Na maji haya hutakiwa dakika 10-20 kabla ya chakula au nusu saa kuendelea baada ya chakula. Ukila chakula huku unasakatia maji huimanisha mtu una kiu. Ulaji chakula na unywaji maji ni vitu viwili tofauti. 
 
Ila utawaona watu wanakula huku wakibugia maji. Unapokula chakula huku unabugia maji unapunguza nguvu za chakula, unajaza tumbo maji na kuchelewesha mmeng’enyo wa chakula (digestion). 
Chakula kisipomeng’enywa vizuri kinaketi tu tumboni. 


Matokeo wengi wetu tuna matumbo makubwa. Kama hufanyi mazoezi lile tumbo linakwenda pembeni (chini ya mbavu) hasa kwa watu wa makamo linaleta maradhi kama kisukari, kiungulia, kuvimbiwa, uyabisi wa tumbo, nk. Kizungu huitwa “love handles.”.



3-SUALA LA UMENG’ENYAJI 
Chakula huanza kumeng’enywa au kusagwa (kwa lugha iliyozoeleka) mdomoni. Mate yako mdomoni ni chanzo cha uchambuaji chakula. Unapobugia chakula bila kutafuna sawasawa unasababisha mambo mawili. Moja chakula kutochambuliwa vizuri, pili chakula kwenda kukaa tu tumboni, au kama kikipita hakisaidii lolote mwilini. 
 
Utafunaji wa taratibu husaidia umeng’enyaji. Chakula kinapofika tumboni hukaa pale dakika ishirini. Hapo huchanganywa na asidi (ya manjano iitwayo Hydrochloric) inayokibadilisha tayari kupelekwa utumbo mkubwa, kupitia kongosho. 


Kule uchafu utapelekwa chini na rutuba kusafirishwa na utumbo mdogo kuelekea katika uwengu, moyo. Moyo utadunda chakula kilichoshageuzwa damu kuelekea mwilini kufanya kazi na akiba hubakishwa katika ini. 



Sasa kama usipotafuna vizuri, ukila huku unakunywa sana maji au vinywaji vingine chakula hakimeng’enywi vizuri. Ndiyo maana unawaona watu wengine wanakula sana lakini hawana afya. Wanaugua ovyo ovyo, wanatoka jasho ovyo, wanajamba ovyo, wana matumbo makubwa, wanavimbiwa, wanakaa siku nyingi bila kwenda choo (inatakiwa mtu kwenda haja kubwa mara moja au mbili kwa siku) nk. 
4-ULAJI WA VYAKULA VYA MAFUTA 
Mafuta ni suala muhimu sana mwilini. Ila ulaji wake shurti uwe wa mpangilio. Yaani unaowiana. 

Lazima mtu uwe na wastani mzuri wa vyakula vya nguvu, yaani “wanga” (ugali, ndizi, wali, viazi mbalimbali, mikate, mahindi, nk), ujenzi yaani “protini” (mboga na nyama), “madini” (mbegu mbegu mbichi si za kukaanga sana na chumvi) na “vitamini” (matunda, maziwa, mayai, nk). 
 
Waafrika tunapenda nyama. Nyama ni muhimu sana maana ina madini aina ya chuma (nyama nyekundu) protini,nguvu na mafuta. Ila mafuta yaliyoko katika nyama mara nyingi si mazuri shauri hayatoki, huganda. 


Chukua nyama ya kuku na samaki ambayo huwa na ngozi. Wengi wetu hupenda sana kula ile ngozi ya wanyama hawa kwa kuwa tamu. Lakini haya ni mafuta mabaya. 
Mafuta ya samaki lakini ni mazuri. Samaki anayo mafuta ya Omega-3 ambayo husaidia mwili na kinga maradhi mwilini. 
Tunapokula nyama choma au ya kukaanga, lazima tule pia mboga za majani (mbichi) na si vizuri kula nyama kila siku. Kama huwezi kukaa bila nyama kila siku, fanya mazoezi ya mwili. 

PENDEKEZO LA 3. 
Kula mbegu mbegu za korosho, karanga (ziwe mbichi badala ya kukaanga na chumvi) kati kati ya siku. Haya ni mafuta yenye rutuba mwilini kuliko nyama za mafuta. 

5-MAZOEZI YA MWILI NA VIUNGO. 
Mazoezi ni mfalme wa kupunguza unene. 
Ukiwauliza wengi watakuambia wanafanya kazi ngumu za sulubu (wanachuruzikwa jasho) kwa hiyo hayo ni mazoezi. Ila kazi na mazoezi ni vitu viwili tofauti. Ingekuwa kufanya kazi ni mazoezi basi kusingekuwa na wastani mfupi wa maisha kwa maskini hasa sisi Waafrika.


Wengine watadai kwamba walipokuwa wadogo shuleni walifanya mazoezi sasa wamekuwa watu wazima (miaka 40 kuendelea) kwamba eti mazoezi ni suala la ujana; kumbe kadri unavyokuwa ki umri ndivyo kadri unavyotakiwa kufanya mazoezi na kujitazama zaidi kiafya. 
 
Watazame Wachina na Wajapani wanavyoishi maisha marefu. 
Mazoezi ni shughuli inayokufanya kwanza uheme (mapafu na moyo kwenda kasi), viungo na mifupa kujinyoosha (stretching), kutoka jasho na usafishaji wa damu. 


Mazoezi yanayosaidia haya ni pamoja na kutembea kasi, kukimbia, kuogelea, michezo mbalimbali ya riadha (kama mpira wa miguu, nyavu, kikapu, mikono, nk); michezo ya kupigana na kujilinda yaani masho ati(karate, kung fu, judo, capoeira, krav maga, jiu jitsu, systema, kickboxing, thai boxing, kempo, kalari payatu, aikido, nk) 


Ni muhimu mwanadamu ufanye mazoezi makali ya viungo mara mbili tatu kwa juma. Si vizuri kufanya kila siku kwani musuli na mishipa inahitaji kupumzika na kukua. 
Kama unapenda kuinua vyuma lazima uwe na mwalimu wa kukuelekeza; na si vizuri kufanya kila siku. Wastani wa mara mbili tatu kwa juma inatosha kabisa. 


6-UPO UFANYAJI MAZOEZI WA AINA MBILI 
Mazoezi ya nguvu ya kuhema niliyotaja hapo juu (cardio-vascular) na yale laini ya kujinyoosha yaani ambayo hutumia zaidi nguvu za ndani na pumzi. Haya ya pili ni kama Yoga (India), Tai Chi Chuan (China) na aina mpya mazoezi iliyoanza Majuu miaka ya karibuni yaani Pilates (hutamkwa hivyo hivyo ilivyoandikwa Pilates). Haya laini yanawafaa zaidi watu wazima na nchini China na Japan mathalan utawakuta wazee wa miaka 80 hadi 90 bado wanayafanya. Husaidia moyo, damu na akili. 
 
Michezo na mazoezi ya mwili ni njia kuu ya kupunguza unene, kurefusha maisha, kuchangamsha ubongo, kupunguza ulevi, uvutaji sigara, dawa za kulevya, tabia mbaya za uvivu, ugomvi, nk. Mataifa yenye watu wanaofanya mazoezi kama Japan, Brazili, India, China nk huwa na wachapa kazi wengi na wananchi wanaoipenda jamii yao. 
7-KULA SANA CHUMVI SI VIZURI 
Ulaji chumvi mwingi hutokana na suala la ladha. Kisayansi vyakula vyote vina chumvi asilia sema tu tumezoea kuongezea madini hii iitwayo Sodium. Sodium inachangia sana kufupisha maisha.


Huifanya mishipa ya damu ichoke; ni kama bomba lolote la maji ukilitazama baadaye hugeuka rangi kutokana na yale maji kupita pale kila siku. 
 
Kwa wale tunaoishi nchi za joto na kutoka sana jasho kula chumvi ni muhimu. Ila tatizo letu ni kwamba hatunywi maji ya kutosha. Mtu ukiwa na kiu unakunywa soda au kinywaji cha sukari; inakuwa kama unaendelea kuutesa mwili. 


Kwa vipi? Mishipa inayopitisha damu mwilini badala ya kusaidiwa kwa maji inawekewa kazi zaidi ya kusafisha sukari na chumvi. Ndiyo maana vifo vingi vinatokea mapema; wastani wetu wa maisha haupiti miaka 50.


Utafiti uliofanywa chuo kikuu cha California, Marekani mwanzoni mwa 2010, umethitibisha kwamba vifo vingi duniani husababishwa na maradhi ya moyo na saratani ambavyo hutokana na uvutaji sigara, unene, ulevi na ulaji sana wa chumvi na sukari. Tukipunguza ulaji wa chumvi tunasaidia pia kupunguza maradhi ya moyo, utafiti unasema. 
 

8-TAFITI ZA VYUO KADHAA ULIMWNGUNI KUHUSIANA NA AFYA.

-Jarida la Kimarekani la sayansi lilieleza mwaka jana kwamba utapunguza ugonjwa wa moyo (ambao husababishwa na unene , wasiwasi na purukshani) kwa asilia mia 42 kama utakula matunda na mboga za majani peke yake kila siku, juu ya msosi wa kawaida. 


PENDEKEZO LA KULA- Na 4. 

Kula mlo wako. Baada ya saa mbili au tatu, sakatia tunda au matunda; baada ya mlo mwingine, kula sahani ya mseto wa mboga mbichi kama karote na matango. Utaona tofauti ya afya, ngozi, wajihi, kinyesi, usingizi, nk. Kidesturi tumezoea kunywa chai au soda za sukari sukari na gesi kati kati nya milo badala ya matunda na mboga mbichi za majani). 

-Utafiti uliofanywa na wanasayansi chuo kikuu cha South Carolina mwanzo wa mwaka 2010 kuhusu faida za kuogelea. 


Zoezi la kuogelea lina faida zaidi ya kukimbia au kutembea kwa vile huchanganya mazoezi makali na pumzi, kusaidia mapafu na moyo. Utafiti ulithibitisha kuogelea hupunguza hatari za kifo kwa asili mia hamsini. 


-Utafiti wa jarida la chuo cha uganga Ulaya umeeleza (desemba 2009) kwamba kulala nusu saa kila mchana (“nap”) husaidia kupunguza ugonjwa wa moyo kwa asilimia 37. 


-Uchunguzi wa chuo cha michezo cha Hispania mwanzoni mwa 2010 umethibitisha kwamba ukikimbia mara tatu kwa juma (jogging) unaongeza nyege mwilini kwa asili mia 75. Hasa kwa watu wa makamo mnaoanza kupoteza nguvu za urijali. 


-Uchunguzi chuo kikuu cha Leeds, Uingereza mwanzoni mwa 2010 umeonyesha unapotembea kwa miguu, ukikwepa barabara kubwa zisisokuwa na mioshi ya magari (pollution) unapunguza matatizo ya maradhi ya hewa chafu kama pumu, mapafu na appendix. 
-Uchunguzi wa chuo kikuu cha Texas mwaka 2010 umegundua kwamba kula tunda la divai nyekundu mara kwa mara husaidia kupunguza kupata ugonjwa wa kisukari. 


-Hapo hapo tunaelezwa kwamba watu weusi na bara la Asia wanakumbwa zaidi na ugonjwa wa kisukari kutokana na vinywaji vya sukari sukari na gesi (fizzy drinks). Ukinywa kiasi cha miligramu 300 za vinywaji hivi (Cocacola, Red Bull, Fanta, nk) kwa siku unajitahadharisha kupata kisukari. 
9-KUFUNGA 
Neno kufunga linatambuliwa rasmi kuhusiana na Waislamu (mwezi Ramadhani) au Wakristo (Lenti nk). Ufungaji huo una masharti mengine ya kidini tofauti na haya ya kiafya. 


Mathalani wafungaji hawa hula chakula kingi usiku; ukihesabu wanafunga wastani wa saa 12 tu. Kawaida ukitaka virusi na takataka nyingine mwilini zitoweke, au viungo vipumzike wahitaji saa 20 kuendelea. 


Ufungaji ninaouongelea ni ufungaji wa kutokula kabisa kwa saa 24, 36 hadi 48 kuendele 
 
Ufungaji ni nini?
Kama mashine yeyote mwili wa mwanadamu unahitaji kupumzika na kujisafisha. Hata tukiwa tumelala bado viungo mbalimbali mwilini vinafanya kazi. Kwa hiyo faida ya kwanza kabisa ya kufunga ni kuupumzisha mwili kama mfanyakazi yeyote anapokwenda likizo. 


Faida ya pili ya kufunga ni kusafisha mwili kutokana na uchafu ambao haukutoka (kinyesi hakitoi mabaki yote toka utumbo mkubwa), dawa na takataka za mazingira tunayoyavutia hewa, virusi au kuyanywa katika maji na vyakula mbalimbali na pia uchafu wa hisia, yaani hasira, huzuni, nk. 
Kuna ufungaji wa aina mbalimbali. 


1-Kufunga kwa kunywa maji tu, saa 24 kuendelea… 
2-Kufunga kwa kutokunywa maji au kula chochote, saa 24 kuendelea.
3-Kufunga kwa kula tu matunda au mboga zilizopondwa kama karote, matango nk, saa 24 kuendelea.



Ufungaji huu unatakiwa ufanywe kwa mpangilio. Kitu muhimu si tu kufunga bali NAMNA unavyofungua. Ukianza kula tena, unaanza taratibu. Kawaida ni vizuri kuanza na maji, kikombe au bilauri ya kwanza taratibu. Subiri tena nusu saa, bilauri nyingine, halafu hadi ya tatu, halafu ndiyo matunda yasiyo ya chachu, na kadhalika. Kuanza kufungua kwa kunywa chai ya maziwa, uji au vyakula vingine vya wanga hakusadii sana mfungo huu. 
Maana lengo lake ni kusafisha mwili. 

PENDEKEZO LA 5.
Kwa wenye imani za kidini. Unaweza pia kufunga hivi ukawa pia unasali au kuvaa mavazi yanayokufanya mtu wa amani. Ukifanya hivi unajitakasa kimwili na kiroho. Si lazima ungojee ile miezi ya kufunga na wengine. 

10-USINGAJI 
Usingaji au masaji ni njia nzuri sana ya kupunguza unene. Ikiwa unaangalia namna unavyokula, unafanya mazoezi na kusingwa mara moja au mbili kwa mwezi unaupalilia mwili vizuri. Nini faida ya usingaji? Kusinga husaidia ngozi, mishipa ya damu na sura nzima ya mwili na taswira yako mwanadamu. 

Wengi wetu tunaposikia neno kusinga tunafikiria usingaji wa mapenzi. Hivi ni vitu viwili tofauti kwani usingaji wa mapenzi unaimanisha mahusiano ya kihisia. 
 
Kifupi mwanadamu unatakiwa uwe unautunza na kuungalia mwili wako kama nyumba au hekalu lako. Wengi wetu tunaoga, tunajipaka marashi, tunasuka, tunanyoa nywele au ndevu; lakini miili yetu kiundani inaoza taratibu.

Kama alivyosema mpiganaji, msanii, mwanafalsafa, mwigizaji, mwandishi mashuhuri marehemu Bruce Lee katika shairi lake Mazingira Yako Kimya (toka kitabu “Msanii wa Maisha”, Turtle Publishing, 2001):

Dawa za nywele zinazosababisha uvimbe wa kizazi.

0 maoni
saluni a3038
Na Hudugu Ng'amilo
Dawa za kulainisha nywele (relaxer) zimekuwa zinapendwa na wanawake wengi wa Afrika kwa kuwa zina uwezo wa kulainisha nywele na kumfanya apendeze na awe wa kuvutia.
Hata hivyo, wataalamu wa afya wanadai kuwa dawa hizo zinasababisha uvimbe kwenye kizazi kutokana na kemikali za dawa hizo ambazo huingia mwilini kupitia majeraha au ngozi wakati wa kupaka.
Daktari wa Manispaa ya Ilala, Laurent Chipata alifanya utafiti na kubaini kuwa dawa za nywele na vipodozi zina kemikali ambazo husababisha uzalishwaji wa vichocheo kwa kiasi kikubwa na kusababisha uvimbe kwenye kizazi uitwao fibroids au leimyoma.
"Kemikali hizi hupenya kwenye ngozi na wakati mwingine hata kwa harufu tu, husababisha kuzalishwa kwa wingi wa vichocheo aina ya estrogen ambavyo huchangia kuota kwa uvimbe wa fibroids," anasema.
Dk Chipata anasema kukua kwa uvimbe kwenye kizazi hutokea katika kipindi ambacho mama yupo kwenye uzazi yaani kabla hajakoma hedhi.
Utafiti wa Dk Chipata ulifanywa nchini na kujumuisha wanawake wa kada tofauti tofauti wanaotumia dawa za nywele na wale wasiotumia na ukubwa wa tatizo hili ulibainika.
"Zipo kemikali tofauti tofauti zinazosababisha uvinbe kwenye kizazi, zipo za kwenye dawa za kilimo kama DDT na za kwenye mafuta ya ngozi kama vile mercury na hydroquionone," anasema.
Dk Chipata anasema madhara yanayopatikana katika kemikali za vipodozi ni makubwa siyo tu kwenye kizazi bali nyingine husababisha saratani au kufeli kwa figo. Anatoa mfano wa kemikali ya zebaki (mercury).
"Dawa za nywele zina madhara si lazima zipenye kwenye ngozi baada ya mtu kupata jeraha la kuungua bali zinaweza kupenya zenyewe kwenye ngozi kutokana na mfumo wa ngozi," anasema.
Anashauri kuwa ni vyema watu wakasoma kipodozi kimetengenezwa kwa nini kabla ya kukitumia na kuongeza kuwa ni salama zaidi kubaki na ngozi au nywele halisi badala ya kujibadilisha.
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekataza vipodozi vyenye kemikali kama biothionol, hexachlorophene, mercury, vinyl chloride, zirconium na bidhaa zenye aerosol, chloroquionone, steroids, methylene na chloroform.
Utafiti mwingine uliofanywa mwaka 2012 na Dk Lauren Wise na wenzake nchini Marekani na kuchapishwa kwenye jarida la afya la nchini Marekani ulibaini kuwa vipodozi vingi vina kemikali zenye vichocheo vya estrogen ambavyo kwa kawaida huchochea kasi ya kuota kwa uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke na wakati mwingine kwenye mji wa mimba. Kitaalamu uvimbe au vivimbe hivi hujulikana kama fibroids au myoma.Dk Wise anasema aliwafanyia uchunguzi wanawake wanaotumia dawa za kulainisha nywele na kuangali umri walioanza kutumia dawa hizo, mara ngapi, waliungua kiasi gani na walikaa na dawa hizo kichwani kwa kipindi gani.
Aliwafuatilia wanawake 23,580 wanaotumia dawa za kulainisha nywele na baada ya kipindi fulani walipimwa. Kati yao, 7146 waligundulika kuwa na uvimbe kwenye kizazi baada ya kupimwa kwa mionzi na wengine kufanyiwa upasuaji.
Kwa nini relaxer ni hatari kwa wanawake?
Dk Wise anasema mchanganyiko ulio kenye dawa za nywele hasa zilizoandikwa "Lye Relaxer" ni sodium hydroxide wakati makopo ya dawa yaliyoandikwa "No Lye Relaxer" yana calcium hydroxide na guanidine carbonate.
Bidhaa za kulainishwa nywele zilizoandikwa 'no lye relaxer' zinadaiwa kusababisha majeraha kwa kiasi kidogo ukilinganisha na zile zilizoandikwa "Lye Relaxer".
Uvimbe kwenye kizazi ni nini?
Ukuta wa nyumba ya uzazi umejengwa kwa misuli ya tishu. Kwa kawaida uvimbe huu huanza kidogo kidogo na hukua hadi kufikia ukubwa wa tikiti maji. Fibroids kubwa huweza kukua na kutanua nyumba ya uzazi na kuwa sawa na ujauzito wa miezi sita au saba.
Mwanamke huweza kuwa na uvimbe mmoja mkubwa au vivimbe vingi ndani ya kizazi.
Daktari Bigwa wa magonjwa ya uzazi wa Kitengo cha Upasuaji cha Chuo Kikuu Sayansi ya Tiba Muhimbili, Henry Mwakyoma anauelezea fibroids ni uvimbe ambao upo katika umbile la misuli myembamba na laini linalokua siku hadi siku.
"Sababu inayopewa kipaumbele zaidi ni wingi wa vichocheo vya estrogen ambavyo vipo katika miili ya wanawake," anasema.
Dk Mwakyoma anafafanua kuwa, vichocheo hivi ndivyo hufanya kazi katika mwili wa mwanamke na kumsababishia kupata siku zake za hedhi.
"Ndiyo maana wengi wanaopata uvimbe huu, huwa ni wanawake walio katika umri mkubwa au ambao tayari wamevunja ungo, kwani ndiyo ambao huzalisha vichocheo vya estrogeni," anabainisha mtaalamu huyo."Dalili hutegemeana na eneo ulipokaa uvimbe na ukubwa wake. Wengi hugundulika wakati wa kujifungua au endapo mwanamke atapata uvimbe katikati ya kizazi, basi huweza kutokwa damu kwa wingi," anasema.
Anaongeza: "Hata hivyo, asilimia 35 hadi 50 ya wanawake wanaougua maradhi haya huonyesha dalili wakati wa kujifungua,"
Dalili nyingine ni mwanamke kutokwa damu zake za hedhi kwa wingi na kwa siku nyingi. Damu za hedhi huweza kuwa nyingi au kidogo sana zikiambatana na maumivu makali.
Anasema wakati mwingine mwanamke huweza kuhisi ana ujauzito kwani uvimbe huu huwa mkubwa na huchezacheza kana kwamba ni kiumbe.
"Nina mifano hai, wapo wanawake waliowahi kuhisi wana ujauzito, wakakosa kabisa siku zao za hedhi, wakaona dalili zote za mimba na kumbe walikuwa na uvimbe wa fibroids," anasema.
Msemaji wa TFDA, Gaudensia Simwanza anasema wamekuwa wakifanya ukaguzi mara kwa mara kuzuia uuzwaji wake.
Isitoshe akasema: "Elimu inatolewa kwa wananchi pia ili kuwafahamisha kuhusu madhara ya vipodozi hivyo kwa sababu wanunuzi wasipokuwepo basi hata biashara haitakuwepo."
Pamoja na hayo, adhabu hutolewa ya kuwanyang'anya na kuwapeleka mahakamani wenye maduka makubwa wakiziuza.CHANZO MWANANCHI.

Usafi na Kinywa na utunzaji wa meno

0 maoni
Usafi na Kinywa na utunzaji wa meno
Assalamu aleykum wasikiliziaji wapenzi na karibuni katika kipindi kingine cha Ijuwe Afya yako. Kipindi ambacho hujadili masuala mbalimbali yanayohusu afya na tiba kwa lengo la kupata maarifa ya kuzitunza vyema afya na siha zetu. Katika kipindi cheti cha leo tutazungumzia usafi wa kinywa na umuhumu wake na jinsi utunzaji wa sehemu hiyo ya mwili unavyoathiri afya ya mtu kwa ujumla.  Karibuni.
&&&&&&&&
Afya ya kinywa ina umuhimu mkubwa zaidi ya unavyoweza kufikiria na kwa ujumla inaweza kutoa ufahamu kuhusiana na jinsi afya yako ya mwili ilivyo. Kuelezewa uhusiano uliopo kati ya afya ya kinywa na afya ya mwili mzima kunasaidia kufahamu umuhimu wa kutunza kinywa na hasa meno na fizi. Kama zilizo sehemu nyingine za mwili, kinywa nacho kimejaa bakteria ambao wengi wao hawana madhara. Kwa kawaida mfumo wa kulinda mwili na utunzaji mzuri wa kinywa kama vile kupiga mswaki na kutumia uzi kuondoa uchafu katika meno kunaweza kudhibiti bakteria walioko kinywani wabakie katika hali ya kawaida na kutodhuru kinywa. Lakini bila kutunza vyema kinywa, bakteria hao wanaweza kusababisha maambukizo na kusababisha meno kuoza na maradhi ya fizi.
Afya ya kinywa inajumuisha siha na namna ya utunzaji wa sehemu zote za mdomo hasa meno na fizi. Mbali na kinywa kutuwezesha ipasavyo kula, kuzungumza na hata kuwa na muonekano mzuri wa uso, meno na fizi zinapaswa zisiwe zimedhurika na kuwa na matatizo kama vile meno kuoza, magonjwa ya fizi, kung'oka meno na mdomo kunuka. Kuoza meno na meno kuwa na matundu ni matatizo ya kinywa yanayoshuhudiwa sana miongoni mwa watu. Sababu zinazoweza kuzuia matatizo hayo ya meno ni kudumisha usafi wa kinywa, kupata fluoride ya kutosha na kutokula kwa wingi vyakula vinavyoweza kudhuru meno na kusababisha matundu.
Afya ya meno na kinywa kwa ujumla inahusiana na afya ya mwili mzima kwa njia tofauti. Kwanza kabisa uwezo wa kutafuna chakula na kukimeza ni muhimu ili mwili uweze kupata virutubisho muhimu vya kujenga mwili. Halikahalika kuwa na kinywa chenye matatizo kunaweza kuathiri namna mtu anavyozungumza na hata kujiamini kwake. Matatizo ya meno yanaweza kumsababishia mtu gharama kubwa ya matibabu na ukarabati wa meno.
Sababu zinazoweza kuathiri afya ya kinywa
Uimara wa meno na fizi unatofautiana kati ya mtu na mtu, na umbo la taya, mdomo, meno na hata kiasi cha mate. Hayo yote ni mambo muhimu yanayoweza kuainisha kwa nini baadhi ya watu meno yao yanaoza zaidi kuliko wengine. Baadhi ya meno yanaweza kuwa na vishimo na nyufa zinazoweza kuruhusu bakteri na tindikali kupenya kwa urahisi na baadhi ya wakati umbo la taya huweza kuzuia meno yasisafishike vizuri na kuondoa vyema uchafu kinywani. Kiwango na namna mate yalivyo pia huweza kuathiri uozaji wa meno. Kwa mfano matundu na nyufa huwa haziko sana katika meno ya mbele ambako kuna mate mengi ikilinganishwa na meno ya nyuma. Bakteria wote walioko kinywani wanaweza kubadilisha wanga kuwa tindikali lakini aina ya streptococci na Lactobacili wana uwezo mkubwa wa kutengeneza tindikali. Kuwepo kinywani vijidudu vya aina hii huongeza uwezekano wa meno kuoza. Baadhi ya watu wana kiasi kikubwa cha bakteria wanaosababisha meno kuoza kuliko watu wengine na hii ni kutokana na kuzembea katika kutunza na kuimarishwa usafi wa kinywa.
Wataalamu wanatwambia kuwa, usafi wa kinywa na matumizi ya dawa za meno zenye fluoride hupunguza kasi ya meno kuoza. Usafi wa meno ni pamoja na kupiga mswaki kila siku kwa kutumia dawa za meno zenye flouride, kutumia uzi wa meno kusafisha eneo lililo kati ya meno, kuchokonea meno kwa kijiti ili kundoa mabaki ya chakula na kufanyiwa uchunguzi wa meno mara kwa mara. Flouride huzuia kupungua madini katika molekuli za meno, kuongeza madini hayo kwenye meno na kuimarisha meno ili yasiathiriwe na tindikali. Matumizi ya fluoride kwa kiwango kinachotakiwa huzuia na kudhibiti matundu kwenye meno. Flouride inaweza kupatikana kutoka katika maji ya kunywa na baadhi ya vinywaji vilivyoongezwa mada hiyo. Pia mada hiyo hutiwa katika dawa za mswaki, geli na dawa za kusafishia kinywa. Katika baadhi ya nchi mada ya fluoride huongezwa hata katika chumvi na maziwa. Kiwango cha flouride katika maji ya kunywa na vyakula kinapaswa kuzingatiwa kwa mujibu wa mahitaji ya mwili. Suala hili ni muhimu kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 6 ambao meno yao bado yanakua. Kutumiwa sana au kwa kiwango kikubwa mada hiyo husababisha matatizo katika enamel au mfupa wa jino hali inayojulikana kinaalamu kama kama fluorosis.
Vyakula na athari yake katika kuoza meno
Ijapokuwa katika nchi nyingi kuoza meno kumekuwa kukiambatanishwa na matumizi ya fluoride na utunzaji wa kinywa, aina ya vyakula anavyokula mtu pia ni jambo muhimu linalochangia meno kuoza. Jinsi chakula chenyewe kilivyo kwa mfano kama kinanata na kung'ang'ania kwenye meno pia husababisha meno kuoza. Vyakula vinavyong'ang'ania kwenye meno kama vile bisikuti na crips huongeza uwezekano wa kuoza meno kwani hubakia juu ya meno kwa muda mrefu zaidi kuliko vyakula vingine. Pia vyakula vyenye sukari zinazoyeyuka kwa haraka husafishwa kwa wepesi kinywani na mate, na kila vyakula vyenye wanga vinavyokaa muda mrefu kinywani na kuzunguka meno, ndivyo bakteria wanavyopata fursa zaidi ya kutengeneza tindikali na kuondoa madini katika meno. Kila tunapokula vyakula vyenye wanga, bakteria walioko kwenye kinywa huanza kutengeneza asidi suala linalopelekea meno kuoza. Mwenendo huu huendelea hadi baada ya dakika 10 hadi 20 baada ya kula au kunywa. Katika kipindi tusichokula au kunywa mate huzimua tindikali na kusaidia kurejesha madini katika meno. Iwapo vyakula au vinywaji vitaliwa mara kwa mara na kinywa kisipate muda wa kurejesha madini kwenye meno, hapo ndipo meno huanza kuoza. Kwa ajili hiyo tunashauriwa kutokula na kunywa wakati wote na pia kupunguza kula vyakula vyenye wanga na sukari kwa uchache tusile vyakula hivyo zaidi ya mara 6 kwa siku. Pia tunashauriwa kuhakikisha kuwa tunapiga mswaki meno kwa kutumia dawa za meno zenye fluoride, kwa uchache mara mbili kwa siku.
Mmomonyoko wa meno
Mmomonyoko wa meno ni kuharibika tishu ngumu ya juu ya meno kutokana na acidi bila kuathiriwa na bakteria wanaosababisha meno kuoza. Kuna vyakula na vinywaji vingi vyenye tindikali katika lishe zetu na kuna uwezekano suala hilo likatuathiri. Kwa mfano kupendelea sana kula vyakula au kunywa vinywaji vyenye tindikali husababisha mmomonyoko wa meno. Tatizo hilo lisiposhughulikiwa huweza kuathiri ufanisi wa kinywa na hutofautiana baina ya watu. Ili kuepukana na tatizo hilo tunashauriwa kujiepusha kupenda sana kunywa vinywaji au kula vyakula vyenye acidi na kupiga mswaki kwa uchache mara mbili kwa siku kwa kutumia dawa ya mswaki yenye fluoride. Pia tunashauriwa kutopiga mswaki mara tu baada ya kunywa au kula chakula chenye acidi kwani kufanya hivyo huweza kuyafanya meno yaharibike kutokana na kusugua meno wakati tindikali ikiwemo kinywani. Pia ni bora tujizoeshe kutafuna chingamu au ubani mara tu baada ya kula vyakula vyenye acidi ili kufanya mate yatengenezwe ambayo husaidia kuondoa acidi mdomoni.
&&&&&&&
Naam wasikilizaji wapenzi, mada hii kuhusu usafi wa kinywa na meno ndio kwanza imeanza, na tutaendelea kuijadili pia katika kipindi kijacho. Hadi wakati huo, daima tuimarishe afya zetu!