BAADA YA OMMY DIMPOZ KUWATUKANA MADIRECTER WA BONGO ADAMU JUMA AFUNGUKA MAZITO . SOMA HAPA KUJUA ALICHOKISEMA AJ
WEKA TANGAZO
Kauli
ya Ommy Dimpoz aliyoitoa siku mbili zilizopita akishauri wadau
wajitokeze na kuwekeza zaidi katika kununua vifaavya kisasa ili wasanii
wasipate sababu ya kwenda kushoot video zao nje, imewafanya madirector
nao kutoa yao ya moyoni.
Kauli
ya Ommy Dimpoz imetokana na maswali ambayo watu wengi wamekua wakihoji
kwanini wasanii wengi sasa hivi wanaamua kwenda kushoot video zao nje na
kwa gharama kubwa ili hali inaaminika hapa nyumbani bado kuna maeneo
mengi na mazuri ya kufanyia video ambayo hayajatumika.
Baada
ya Nisher kuzungumza na kuwatupia lawama wasanii kuwa wanawadharau
madirector wa bongo, Adam Juma wa Visual Lab na yeye ametoa ya moyoni
kuhusu kauli hiyo ya Dimpoz, kupitia Instagram ameandika:
“Hahahahahahhahahahahahaha
vifaaa tutanunua inshallah, ila sasa nasisi tutaanza kutangaza bei
mnazotilipa! Sijawahi kulipwa zaidi ya mil 3.5 na msanii yoyote tanzania
km yupo aje ntampa video 10 buree. @rehemavisuallab @nisherbybee
@jerrymushalastudios @hefemi @meckykaloka #
niggarstalkingshit#mnanitibuasasa#noneducatedniggasoncrack#.”
Director Jerry Mushalla na yeye alicomment kwenye post ya Adam:
“Most
Musicians like to blog and talk too much.. But when it comes to actual
payments they don’t pay… @adamjumanxl I wish directors woote mngekuwa Na
msimamo Wa pamoja @hefemi @nisherbybee @abas_adam @travellah”.
Na hiki ndicho Nisher alichokisema wiki hii kuhusu swala hilo:
“Mi
sipati logic wasanii wanavyosema wanaweza kulipa sijui milioni za hela
wapi…mi napigiwa simu na wasanii wakubwa lakini kila anaekupigia anasema
mi sina hela lakini mi naweza kukugharamia chochote unachotaka tushoot
video.
Unaanzaje
na kauli halafu na wakati mi nasoma kwenye Internet kwamba umelipa
sijui kiasi gani gani gani kwenye video flani flani, nafikiri video ya
Ben Pol juzi tu ambayo tuliifanya ‘Unanichora’ labda ndio video
niliyopata hela nyingi kwa kiasi flani kwa sababu video iligharimu
karibu milioni 10 hivi. Mi nadhani tunachukuliana poa na kudhariana
kiukweli.
Kwa
Mfano ukinilipa milioni 5 au 10, una uhakika kwamba hela hiyo hiyo
itatumika kusambaza kazi yako[…] kufanya kila kitu. Vyombo vipo cranes
nini, cranes zenyewe za kukodi kwa siku laki 5, camera zipo za kukodi
Red Camera unaambiwa labda dola 800 kwa siku, nani atakupa hiyo hela?
Hivi vitu vinakatisha tamaa wasanii hawatukubali wanatuona kama
hatujui.”
Hiki ndicho alichokisema Ommy Dimpoz wiki hii na kuwafanya madirector nao kuamua kufunguka:
“Biashara
ya video ishaingia ushindani, kwahiyo kuna haja ya kuwekeza kwenye
vifaa, m i nauhakika hapa mtu ana mavifaa kibao unaenda kushoot Lushoto
huko noma, wazungu wenyewe watauliza umeshoot wapi. Tuna maeneo kibao
Zanzibar wapi wapi wapi ya kushutia, sio kwamba hatuna maeneo, maeneo
tunayo lakini hatujawa na
vile
vitu. Kwahiyo ndo maana hata mtu pia unafikiria ah sijui nishoot
Zanzibar, lakini unawaza kumchukua labda GodFather au nani kumleta huku
Tanzania ndio mziki.
Halafu
mtu utakapoleta vifaa hivyo nauhakika hautaishia kwenye video tu, kuna
matangazo, utakodi utafanyaje…Watu lazima waelewe kitu kimoja kwamba
hakuna mtu anaependa kujitia gharama kama kuna uwezo wa kuepuka gharama,
sio ufahari mi nina vitu vingi vya kufanya sio kwamba nataka tu
nikalipe dola elfu 30 kushoot video wakati nina uwezo wa kuokoa hiyo
hela labda kulipa dola elfu 15 au elfu 10.
Wadau
wanatusikia sie ndio wasanii wenyewe tunasema kwamba muziki unalipa
mnaona sasa hivi vijana wenu wanapata shilingi mbili tatu, hizo shilingi
mbili tatu mtagawana nao vipi kuliko kwenda kuwapa watu wengine huko
nje ya nchi.”
WEKA TANGAZO
0 maoni: