MSANII BABA LEVO ADAIWA KUMSHUSHIA KIPIGO SHEMEJI YAKE . SOMA HAPA KUJUA KISA CHA KUMSHUSHIA KIPIGO

WEKA TANGAZO

STAA wa Bongo Fleva, Trey Revocatus ‘Baba Levo’ amedaiwa kumshushia kipigo shemeji yake aliyefahamika kwa jina la Pili Kimenya, mkazi wa Kisangani, Kigoma.
Kwa mujibu wa chanzo, Baba Levo alikwenda kwenye mazishi ya kaka yake ambaye alikuwa mchumba wa Pili, Patrick Revocatus, baada ya kuzika alimtuhumu shemeji yake huyo kuwa amemuibia marehemu cheni na aliposema hajachukua, jamaa akampa kipigo.
Aliulizwa Baba Levo kuhusiana na tukio hilo alisema:“Hamna mimi sikumpiga, wao na mama yake ndiyo walikuja kufanya fujo msibani nikawafungulia mashtaka polisi. Mwanamke huyo alimharibia marehemu kwa kumvutisha madawa ya kulevya.”
WEKA TANGAZO

0 maoni: