Kila mwanadamu ana mwili tofauti na tunapaswa kufanya mazoezi kulingana na aina ya miili yetu.
Tujifunze njia tofauti za kufanya mazoezi Kulingana na miili wetu.
Je kuna uwezekano wa kuwa unaongeza uzito wako?
Kila mwili wa binadamu umeumbwa tofauti na kwa njia ya kipekee kama alama za vidole.
Hata hivyo tunaweza kutofautisha miili ya wanadamu kwa makundi matatu makubwa.
Tutafanya hivyo kulingana na uzito wa mwili, misuli na mafuta kwenye mwili.
Umuhimu
wa kuelewa ni aina gani ya mazoezi unapaswa kufanya kuambatana na mwili
wako unategemea na ujuzi ambao uko nao kuhusu mwili wako.
Tatizo ni kuwa "kuna mzozo unaojitokeza wakati wa kufanya mazoezi".
Kulingana na Juan Francisco Marco, profesa katika Kituo cha michezo na mafunzo cha Alto Rendimient kule Uhispania.
‘’Unapaswa kuamua iwapo utaboresha sura yako au utafanya mchezo iliongezea.
Kuna aina tatu za miili kulingana na chembe chembe za urithi na maumbile ya mwili wako.
Ectomorph: Watu wenye mwili na kifua chembamba
"Ectomorph"
Huyu
kwa kawaida ni mrefu, mwembamba ana kifua chembamba na hupata wakati
mgumu kuongeza uzito wa misuli yake, alielezea Profesa Marco.
Michezo
ambayo anashiriki ni kama kukimbia ,kuogelea au kuendesha baiskeli
ingawa Profesa Marco alionya ni vyema kufanya mazoezi ya kuongeza nguvu,
kuongeza uzito na kujenga misuli.
Kundi hili linapaswa kuzingatia sana mazoezi ya kila mara ambapo misuli inasonga sana.
Endomorpho: Watu wenye mengi ya mwili
"Endomorph"
Huyu
ni kinyume cha "Ectomorph", kundi hili hufanya mazoezi yakuongeza nguvu
na uzito wa misuli, na hufanya mazoezi mara kwa mara.
Kundi hili lina mafuta mengi ya mwili, huonekana kuwa wanaweza kuwa wanariadha bila hata kujaribu.
Mesomorph: Wanamchezo wa kiasili
"Mesomorph"
Ni wanamchezo wa kiasili, chochote ambacho wanafanya huwa kizuri.
Marco anaelezea. Mazoezi bora kwa aina hii ya mwili ni kujihusisha katika mchezo ambao unaleta pamoja nguvu.
Kutokana
na faida ambazo "Mesomorph" wanazo, Marco anasisitiza kuwa kundi hili
bado linapaswa kuangaliwa kwa makini wanavyokula kwani wanauwezekano wa
kuongeza uzito wa mwili ingawa si sana kama "Endomorph".
0 maoni: