Picha Chafu Za Wema Sepetu Na Diamond Platnumz Zatinga Bungeni..!!
WEKA TANGAZO
WEKA TANGAZO
Sakata
la mastaa wakiwemo Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond’ kupiga picha
chafu kisha kuzitundika mitandaoni limetinga bungeni baada ya juzikati
baadhi ya wabunge kulishupalia.
Hilo
liliibuka Suzi mjengoni katika kipindi cha maswali na majibu ambapo
Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Saidi Mtanda alitaka kujua hatua
zilizochukuliwa na serikali katika kukabiliana na tabia za watu maarufu
kupiga picha zisizo na maadili kisha kuziweka mtandaoni.
Katika
kujibu swali hilo, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Juma Nkamia alisema: “Tunajitahidi kuhakikisha wanaofanya hivyo
wanachukuliwa hatua stahili ili kukabiliana na matendo hayo ambayo ni
kinyume na maadili.”
Katika
kuonesha kutoridhika na majibu ya waziri, Mheshimiwa Mtanda alipopewa
nafasi aulize swali la nyongeza alisema: “Mheshimwa spika nahisi swali
langu halijajibiwa ipasavyo. Nilichotaka kujua ni hatua ambazo
zimechukuliwa kwa baadhi ya watu mastaa kama vile Wema na Diamond ambao
hupiga picha zao zisizofaa kisha kuziweka mtandaoni.”
Kufuatia
swali hilo, Nkamia alisimama na kujibu kwamba, serikali imeweka
mikakati na njia sahihi za kukabiliana na tabia hiyo na kwamba wale
ambao watabainika watachukuliwa hatua zinazostahili.
Licha
ya majibu hayo, bado wabunge walionesha kutoridhika, hali ambayo Spika
Anne Makinda aliiona na yeye akaongezea “Waheshimiwa wanataka kujua na
za hivi karibuni zilizovuja mtandaoni” ambapo jibu la Nkamia lilikuwa:
“Mheshimiwa
kuhusu hizi picha za juzi zilizosambaa mtandaoni, tunazifuatilia kujua
zimeanzia wapi na taarifa zake zikoje kwani hata mimi bado sijaziona ila
tutachukua hatua tutakapobaini zilikotokea.”
-swahilitz
0 maoni: