Suarez amng'ata Chiellini
WEKA TANGAZO
Chiellini aliangushwa chini na
uchungu wa meno ya Suarez na alionekana akimkimbilia refarii akimvulia
shati ilikuonesha alama ya meno begani lakini refarii akapuzilia mbali .
Chiellini ameiambia runinga moja ya Italia kuwa Suarez alijiangusha chini likuficha uovu huo wa kutisha na kusingizia kuwa alikuwa amepigwa kumbo.
Suarez alionekana akigaaga uwanjani baada ya tukio hilo.
Japo refarii Marco Rodriguez hakuona tukio hilo la kutamausha Chiellini amesikika akisema kuwa ni jambo la kuhuzunisha kuwa refarii huyo alipuzilia mbali maombi yake ya kutaka hatua ichukuliwe dhidi ya mshambulizi huyo ambaye aliadhibiwa kwa tukio lengine kama hilo akiichezea Liverpool misimu miwili iliyopita nchini Uingereza.
Suarez alilazimika kukaa nje kwa mechi 10 baada ya kumngata kiungo wa Chelsea Branislav Ivanovic aprili 2013.
Awali Suarez aliadhibiwa na shirikisho la soka
la Uholanzi lilimuadhibu Suarez kwa marufuku ya mechi saba baada ya
kumngata mchezaji wa PSV Eindhoven Otman Bakka wakati huo akiwa
nahodha wa Ajax Amsterdam.
WEKA TANGAZO
Mshambulizi wa Uruguay Luis Suarez amekumbwa na kashfa mpya baada ya kuonekana kumngata Giorgio Chiellini wa Italia.
Suarez alionekana akiminya bega la Chiellini
muda mchache kabla ya Diego Godin kufunga bao la ushindi la Uruguay
dhidi ya Italia.Chiellini ameiambia runinga moja ya Italia kuwa Suarez alijiangusha chini likuficha uovu huo wa kutisha na kusingizia kuwa alikuwa amepigwa kumbo.
Japo refarii Marco Rodriguez hakuona tukio hilo la kutamausha Chiellini amesikika akisema kuwa ni jambo la kuhuzunisha kuwa refarii huyo alipuzilia mbali maombi yake ya kutaka hatua ichukuliwe dhidi ya mshambulizi huyo ambaye aliadhibiwa kwa tukio lengine kama hilo akiichezea Liverpool misimu miwili iliyopita nchini Uingereza.
Suarez alilazimika kukaa nje kwa mechi 10 baada ya kumngata kiungo wa Chelsea Branislav Ivanovic aprili 2013.
Mwaka wa 2010 Suarez aliunawa mkwaju ambao
ulikuwa unaingia wavuni na kuinyima Ghana nafasi ya kuingia kwenye nusu
fainali ya kombe la dunia .
0 maoni: