PENNY NA WEMA WAKUMBANA STUDIO
WEKA TANGAZO
Katika hali isiyotarajiwa, mchumba wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul
‘Diamond’, Wema Sepetu na aliyewahi kuwa mchumba wa msanii huyo, Penniel
Mungilwa ‘Penny’ walikutana studio na kila mmoja akamkwepa mwenzake.
Tukio hilo lilitokea juzikati maeneo ya Posta, jijini Dar katika Studio
za Amaya ambayo ni saluni inayotumika kurekodia vipindi mbalimbali vya
Mkasi vinavyorushwa kupitia Runinga ya EATV.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mwigizaji Aunt Ezekiel alialikwa na
mtangazaji wa kipindi hicho, Salama Jabir kwenda kufanya mahojiano,
akaambatana na shosti wake Wema ndipo ghafla wakakutana na Penny ambaye
naye alialikwa kwa wakati wake.
Chanzo kilizidi kumwaga data kuwa, baada ya Aunt na Wema kufika studio
hapo, Salama aliwakaribisha na wakaanza kurekodi kipindi hicho, lakini
walipokuwa wakiendelea na mahojiano, Penny naye aliwasili bila kujua
kama Wema alikuwepo.
“Penny alipofika alizama ndani na kukutana na Salama ambaye alimwambia
kuwa kuna watu wanatoka ndani muda si mrefu hivyo wakati bado wanaongea,
Wema na Aunt walitoka studio ambapo Penny alikimbilia kwenye gari lake
kukwepa kuonana na Wema ambaye pia alionekana kutotaka kuonana na
Penny,” kilisema chanzo na kuongeza:
“Kwa kuwa Wema naye alimuona kwa mbali Penny, alimtaka Aunt waingie kwenye gari fastafasta na kuondoka eneo hilo.”
Mapaparazi wetu baada ya kuunyaka mchongo huo, walimtafuta Penny ili
kumsikia anazungumziaje ishu hiyo. Alipopatikana, alijibu hivi:
“Mimi sikumkimbia Wema na itambulike kuwa wakati naenda pale sikujua
kama Wema alikuwepo hivyo nilifika na kusubiria muda wangu wa mahojiano
nikiwa ndani ya gari, sikuwa na haja ya kujua Wema yupo ama la.”
Jitihada za kumpata Wema hazikuzaa matunda lakini alipotafutwa Aunt Ezekiel, alitiririka:
“Nilimuona Penny kweli pale studio ingawa mwanzo nilitahamaki maana
sikujua kama naye alikuwa akisubiria tutoke aingie kwenye kipindi ila
Salama alinishtua sana baada ya kusema kabla hatujatoka ndani tusubiri
aandae uwanja wa ngumi, alitania.”
Wema na Penny wanadaiwa kuwa picha haziendi baada ya Wema kumtuhumu
Penny ambaye alikuwa rafiki yake kuwa alimwibia Diamond wake kabla
hawajamwagana na kurejea tena mikononi mwake.
WEKA TANGAZO
0 maoni: