TOFAUTI ZA UTAMU WA PENZI

WEKA TANGAZO Ni kweli kabisa kuwa penzi kati ya mwanaume na mwanamke hupitia mabadiliko mbalimbali kwani mtu hukutana na vitu mbalimbali na mawazo mbalimbali yanayoweza kumpa sababu ya yeye kubadilika. Katika ulimwengu wa sasa ambapo mtu akifikia umri wa miaka 25 tayari amekwishakuwa na wapenzi zaidi ya 3 ni vigumu kabisa mtu kushindwa kuanza kulinganisha utamu wa penzi alilopata huko nyuma kabla yako na lile unalompa sasa.Katika ulinganishaji huo lazima kuna vitu Fulani utakavyopungukiwa kama vile sura, rangi ya ngozi yako,urefu au ufupi kwa mwili wako, ukubwa wa uume au uke wako,uwezo wako wa kifedha,uongeaji wako,hasira zako ,utamu wako katika tendo la ndoa na vitu vinginevyo. Iwapo unaamini kuwa hilo ni jambo la kweli basi lazima uamini pia kuwa penzi lako litapimwa kwa kadri siku zinavyoenda.

Ndugu mpendwa napenda nikuambie kuwa pamoja na ukweli kuwa mpenzi wako ulienae sasa au yule utakayempata tayari ameshakuwa na wapenzi wasiopungua watatu basi inakupasa uamini kuwa sio atakuwa analinganisha utamu wa penzi lako na wapenzi waliotangulia bali pia atakuwa anaangalia kama wewe pia una dalili za kuweza kumuumiza kama alivyoumizwa na wapenzi waliotangulia.Hivyo ni muhimu sana katika mwenendo wako ujitahidi usisababishe maumivu katika moyo wa mpenzi wako.Jambo lolote lile linaloleta huzuni au kumkosesha raha mwenzio linaweza kuonekana kama tishio.

Katokana na hali halisi ya uanadamu tumeumbwa na tabia ya kujilinda na maumivu au kukwepa watu ambao ambao wanaweza kutuumiza ni muhimu uepuke mambo ambayo yanwaweza kuonekana kama tishio kwa mpenzi wako.Kutokan na umuhimu wa mtu kujilinda bila wewe kujua mwenzio atakuwa makini kuangalia maneno ,mwenendo na matendo yako kuangalia kama una mbegu yenye uwezo wa kuzaa maumivu yatakayoumiza moyo wake.
Kama vile utamu wa vyakula na matunda vilivyo na utofauti kadhalika ili uweze kumfurahisha na kutunza penzi lako ni muhimu uwe na uwezo wa kuleta utamu katika maeneo mbalimbali ya uhusiano wenu.Kwa maneno mengine ni muhimu utumie akili yako kujua maeneo yanayoleta utamu mwingi zaidi kwa mpenzi wako na kufanya kazi hiyo na bila kuacha maeneo mengine yaletayo utamu wa kiasi kidogo.

Ili uweze kufanikiwa katika hilo kwanza lazima utambue kuwa kila mmoja wetu anapendelea vitu tofauti tofauti kama vile kuna wengine hawawezi kula chakula bila pilipili kadhalika kuna watu wengine ambao hawawezi kuendeleza uhusiano unaokuwa na mapungufu fulani. Kwa mfano huo wa pilipili ningependa kusisitiza kuwa inakupasa uwe makini sana katika vitu ambavyo wewe unapendelea lakini mwenzio hapendelei kwani hapo ukishindwa kutimiza haja za mwenzio unaweka uhusiano wako hatarini.Pamoja na kusema hayo pia ni muhimu ukumbuke kuwa upo uwezekano wa kutokea mabadiliko katika vitu ambavyo unapendelea au mwenzio anapendelea.Usipokuwa makini utashindwa kwenda sambamba na madiliko yanayotoke na baadae ukaanza kuona penzi linapungua siku hadi siku na unapomuuliza mpenzi wako utashangaa kuona anakuwa mkali.Kwanini anakuwa mkali? Anakuwa mkali kwani anauona uzembe wako katika kufuatilia mabadiliko ya utamu wa penzi lenu na kwa kuwa hukuwa makini anaona kama vile ulikuwa humjali kwa makusudi kabisa kumbe sivyo.Jambo hili nimeliona katika mahusiano yangu mimi mwenyewe.KWkuwa nimekuwa muwazi sana wapenzi wangu wengi  wamekuwa hawajazoea hali hiyo na kushidwa kunifurahisha katika maeneo kadha na badala ya wapenzi hao kuona ni nafasi ya wao kujifunza mambo mapya wakaniona kuwa ni wa ajabu na mkali jambo ambalo sio la kweli.
    Nakumbuka kuwa na uhusiano na dada mmoja mwenye umri wa miaka 24 na dada huyo aliniambia wazi kuwa hajawahi kuachwa na mwanaume yeyote yule kati ya wanaume sita walionitangulia(wakati naazisha ushusiano nae alikuwa hajvunja na kuzika uhusiano aliokuwa na handsome Fulani).Siku moja dada huyo  baada ya kufanya kosa fulani  na kuadhibiwa aliniuliza anifanyie nini ili  nijue ananipenda na mimi nikamwambia ninachohitaji sana ili nijione ananipenda ni heshima.KWA wengi hilo linaonekana jambo rahisi sana lakini ukiliangalia undani wake ni refu na pan asana.Kwa kweli dada huyo alijitahidi sana kuonyesha mapenzi kwangu kwani alidiriki kutoroka kwao na kumhonga mlinzi ili aje kuwa name hadi alfajiri na kwa hilo tu nilimpenda sana.Pamoja na juhidi zake nyingi sana alishindwa kuwa mkweli na muwazi jambo ambalo lilipelekea mimi kuamua kumuacha kwani tayari huko nyuma nilikuwa nimeumizwa vibaya sana na mtu wa aina hiyo.La kushangaza dada huyo alikataa kwa kusema hataki kuachwa na mara kadhaa alikuja nyumbani kwangu na nilipokuwa sipokei simu zake wakati ananisubiri nyumbani alianza kulia hadi majirani wakaingilia kati.NI kweli unaweza kumpenda sana mpenzi wako lakini usipokuwa makini unaweza kuharibu uhusiano huo  wewe mwenyewe.

Umuhimu wa kujali tofauti za utamu unaongezeka zaidi kutokana na mambo mengi tofauti tunayokutana nayo katika mitandao na tamthilia .Katika maeneo hayo niliyotaja upo uwezekano wa mtu kujiona sio mzuri wa kutosha au hana uwezo wa kipesa wa kutosha au hapendwi kikamilifu. Hisia zinazojitokeza wakati wa kuangalia tamthilia au kuona mambo fulani  kwenye mtandao zina nguvu za kumbadilisha mtu na tabia zake au mwenendo wake.

Changamoto kwako ni kwamba jitahidi kuleta utamu wa kutosha katika maeneo mengi zaidi ya uhusiano wako ili umpe sababu za kufurahia kuwa nawe kama mpenzi.

Tahadhari kwako, uonapo mpenzi wako hataki kufanya mabadiliko mazuri unayomweleza kuwa ni muhimu kwako jua kuwa hana penzi la kweli kwako. Pamoja na hilo pale kuwa mpenzi wako anatamani mambo yanayohitaji uwezo mkubwa wa kifedha kuliko uwezo wenu na hajali uboreshaji wa penzi bila kuhusisha pesa basi tambua kuwa mwenzio ni mpenzi wa fedha na sio mpenzi wako.

Nimuhimu katika uhusiano wa kimapenzi kuwepo kwa mfumo unaoleta utamu tofauti tofauti. Hali ya kupata vitu au mambo tofauti huleta uchangamfu na mshikamano ambao husaidia katika kukuza penzi kati ya watu wawili wanaopendana.

WEKA TANGAZO

0 maoni: