MWANAMKE ANG'ATWA MIDOMO NA MPENZI WAKE WAKATI WAKINYONYANA DENDA
WEKA TANGAZO
WEKA TANGAZO
Huffington
Post limeripoti habari kutoka Uingereza ya kusikitisha ya kijana Rhys
Culley kumng’ata vibaya midomo mpenzi wake Chanttelle Ward mwenye umri
wa miaka 18 wakati anamkiss baada ya kuwa na ugomvi unaohusisha na wivu
wa mapenzi.
Kijana
huyo wa miaka 23 alikuwa na wasiwasi baada ya kuhisi kuwa mpenzi wake
alikuwa anachat na mwanaume kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook
akimsaliti.
Akisimulia
mkasa huo mbele ya jopo la majaji, Chanttelle ameeleza kuwa baada ya
kutoka kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa ya mama yake msichana huyo
walielekea nyumbani kwao ambapo Rhys alianzisha mzozo akimtuhumu kuwa
anamsaliti kupitia Facebook.
Kijana huyo alichukua simu ya
Chanttelle kwa makubaliano ya kuangalia jumbe alizokuwa anatuma Facebook
lakini hakukuta mawasiliano kati ya msichana huyo na mwanaume aliyekuwa
anamhisi. Moja kwa moja akaanza kupaza sauti kwa hasira akidai kuwa
amezifuta.
Hasira
za kijana huyo zilimuogopesha akaona ni bora ampigie simu mama yake
lakini alinyang’anywa simu. Rhys alifunga mlango na kuendelea
kumshambulia kwa maneno.
Chanttelle
anaeleza kuwa mgogoro huo ulipofikia hatua ya kupoa hivi, kijana huyo
alimkiss huku akimuuliza kama kweli ana mpenda na hapo ndipo kila kitu
kilibadilika.
“Aliweka mdomo wake wote kuzungumguka lips zangu na kuvuta, nilidhani lips zote zimetoka. Damu zilisambaa kila sehemu.” Msichana huyo alieleza.
Polisi walipofika walikuta wote
wametapakaa damu usoni, wakamkamata kijana huyo na kumkimbiza Chanttelle
hospitali huku akiwa na mikwaruzo katika sehemu mbalimbali za mwili.
Mwanaume
huyo alipopewa nafasi ya kujitetea mahakamani hapo, alieleza kuwa
hakuwa na nia mbaya ya kumuumiza mrembo wake ambaye anadai alikuwa na
bahati kuwa naye.
Rhys alikutwa na hatia. Alirudishwa rumande na anasubiri hukumu yake mwezi ujao.
0 maoni: