DUDE, TINO MBARONI NCHINI KENYA . BOFYA HAPA KUJUA CHANZO NI NINI
WEKA TANGAZO
ASANII nyota
wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ na Hisan Muya ‘Tino’ hivi
karibuni walitiwa mbaroni katika mji wa Kilifi ulio mbele ya Mombasa
nchini Kenya baada ya kukutwa wakipiga picha za filamu yao bila kuwa na
kibali.
Hata hivyo, waigizaji hao baadaye waliachiwa, ingawa hali ilikuwa ngumu
kidogo kwa Tino, ambaye polisi wa Kenya walidai hakuwa Mtanzania, bali
ni raia wa Somalia.
Dude alithibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema liliwatokea kutokana
na mazoea ya huku nyumbani ambako hufanya shughuli zao za kupiga picha
za filamu zao bila kuhitaji kibali.
“Yaani tumepata aibu ya mwaka, kwani tulienda kushuti bila kuomba kibali
kutokana na mazoea ya huku kwetu Bongo, tulipekuliwa sisi na gari letu,
baada ya hapo kibali kikaletwa nikaachiwa lakini Tino waliendelea
kumshikilia wakisema ni Msomali mpaka mkuu wa shirikisho la filamu
Mombasa alipokuja kuokoa jahazi, ukweli Kenya hakufai,”alisema Dude.
WEKA TANGAZO
0 maoni: