JE UNAKUMBUKA AHADI YAKO KWA MPENZI WAKO?

WEKA TANGAZO
BILA shaka ni wazima wa afya njema na mnaendelea na majukumu yenu kama kawaida. Nawashukuru sana kwa kuchagua kusoma safu hii maana hakuna kitakachopotea, zaidi mtaongeza ujuzi juu ya uhusiano na mapenzi.
Mada ya wiki iliyopita ilikuwa na changamoto sana kwa wasomaji, nilipokea simu, waraka pepe na ujumbe mfupi wa maneno kwa wingi sana kutoka kwa wasomaji mbalimbali wakichangia mada ambayo kimsingi ilizungumzia zaidi wanawake.
Ni kweli ni aibu kuachika ukiwa umeshachumbiwa. Ni vyema wasichana wakachukua somo lile kama dira ya maisha yao katika kuelekea kwenye ndoa. Uchumba ni dalili nzuri, ni wakati wa kutulia na kuonyesha umakini wako ili mwanaume husika asibadilishe mawazo kutokana na mwenendo mbaya utakaouonyesha.
Upande wa wanaume, nao nawashauri waachane na ulaghai, maana kuna wengine wanawachumbia wanawake hata watatu kwa wakati mmoja, wote hao wanavalishwa pete lakini mwishowe anawaacha kwenye mataa.
Siyo jambo zuri. Mapenzi yanahitaji zaidi ukweli. Tusicheze na hisia za wengine. Baada ya mwongozo huo, sasa tuendelee na mada yetu.
Nazungumzia juu ya ahadi ambazo wenzi hutoleana wanapokutana mara ya kwanza. Kwa bahati mbaya sana wengi wanapokutana mara ya kwanza, hutoa ahadi yoyote ilimradi iwe ya kumvutia muhusika amkubali kuwa naye.
Hebu tuzungumze na uwe mkweli katika hili; siku ya kwanza kukutana na mpenzi wako
Inawezekana upo katika uhusiano (ndoa) na mwenzi wako, lakini kila siku mnagombana, unajaribu kuweka mambo sawa, lakini baada ya siku mbili, tatu ugomvi unarudi palepale, umejiuliza tatizo ni nini?
Utafiti usio rasmi unaonesha kwamba,
ugomvi mwingi unaotokea baina ya wapenzi/wanandoa husababishwa na ahadi! Yaani unakuta mtu alipokutana na mpenzi wake mara ya kwanza alimpa ahadi kedekede, kwamba atamfanyia hili na lile au hatafanya hivi na vile, lakini wanapokuwa kwenye uhusiano anajisahau na kufanya kinyume na makubaliano, hapo tatizo linaanza!
Hili ni somo ambalo litakuweka sawa wewe ambaye upo kwenye uhusiano kwa muda mrefu na mwenzi wako, kukuweka sawa na kukufanya ukumbuke makosa yako ili upate nafasi ya kutuliza hali ya hewa katika penzi lenu.
Hata hivyo, itawasaidia zaidi wale ambao bado hawajaingia kwenye uhusiano, kujua madhara ya kuahidi ahadi za uongo.
Hebu tuone mambo ya kuzingatia kabla ya kutoa ahadi kwa mpenzi wako unapokutana naye kwa mara ya kwanza, halafu baadaye tutaona ahadi ‘feki’ zinazotolewa na wenzi wanapokutana kwa mara ya kwanza, halafu zikaleta matatizo baadaye.
KWA NINI AHADI?
Kwani ni lazima unapokutana na mwenzi kwa mara ya kwanza utoe ahadi? Unaahidi nini? Kwani unataka ubunge mpaka uanze kutoa ahadi? Kimsingi kuahidi ni sawa na kuonesha jinsi ambavyo una mashaka ya kukataliwa, ndiyo maana unakimbilia kutoa ahadi.
“Kwa kweli nitabadilisha maisha yako...kwanza sisi kwetu mambo safi...nafanya kazi kwenye ofisi ya mdingi na mimi ndiye director. Kwanza nadhani itabidi nifanye mchakato uanze kazi pale! Hivi elimu yako kiwango gani vile?”
Yote hayo ya nini? Baadhi ya ‘mbumbumbu’ au wapenda ahadi, watakuona wa maana na inawezekana kabisa ukapewa nafasi ya kuwa naye, lakini uliyosema ni ya kweli?
Ataingia kwenye uhusiano akiwa na matarajio makubwa sana kichwani mwake, kumbe si kweli umemwingiza mwenzio ‘chaka!’
ulimuahidi nini? Je, ahadi zako zimetekelezeka? Uhusiano wako ukoje sasa hivi ?
WEKA TANGAZO

0 maoni: