JUA VYAKULA BORA NA FAIDA ZAKE MWILINI

WEKA TANGAZO

Makala haya tumerudia kutokana na sababu maalum na inaangalia vyakula muhimu na umuhimu wake katika ustawi wa afya zetu. Kumbuka chakula ni uhai, lakini pia chaweza kuwa sumu kama hakiliwi ipasavyo.
Vitunguu saumu.
KITUNGUU SAUMU
Hiki ni kiungo cha mboga, licha ya kuonekana kama ni kiungo cha kuongezea ladha ya chakula, lakini ni miongoni mwa vyakula vyenye faida kubwa katika afya zetu. Kitunguu saumu husaidia kuyeyusha damu mwilini hivyo kumuepusha mlaji na ugonjwa wa moyo pamoja na presha. Kitunguu hiki pia hutoa kinga kwenye ini na huondoa maumivu ya viungo. Kula angalau kitunguu kimoja mara moja kwa wiki.

Mdalasini.
MDALASINI
Hiki nacho ni kiungo cha kuongezea ladha na rangi kwenye chakula, lakini nacho kina faida zaidi ya hiyo. Mdalasini ambayo inapatikana kwa wingi katika masoko mbalimbali nchini, hufaa  kutumiwa na wagonjwa wa kisukari, kwani hurekebisha kiwango cha sukari mwilini kwa kiwango cha hadi pointi 50. Inapendekezwa kutumiwa angalau nusu kijiko cha chai kila siku mara mbili.

Matango.
TANGO
Watu wengi hulipuuza tango na wengine hawajawahi kula kabisa kwa sababu siyo tamu mdomoni, hata linapochanganywa kwenye kachumbari huepukwa. Hii yote inatokana na kutokujua umuhimu wa tunda hili. Inaelezwa kuwa tango linapoliwa husaidia kusaga chakula tumboni hivyo kumuwezesha mlaji kupata choo laini. Halikadhalika, tango linaweza kutumika katika kuboresha ngozi ya uso kwa kupaka, kwani huondoa vipele na kuifanya ngozi kuwa nyororo. Ni zuri linapoliwa na maganda yake na unaweza kula kiasi utakacho.

Asali.
ASALI
Kama kuna chakula kitamu na kizuri duniani, basi ni asali. Hiki ni chakula cha asili ambacho kimekuwepo enzi na enzi na kimesifiwa hata katika vitabu vya Mungu. Asali ina uwezo wa kudhibiti sumu mwilini, ina uwezo wa kumfanya mtu mnene kupungua uzito na mtu mwembamba kuongezeka uzito hadi kufikia uzito wa kawaida.

Asali huupa nguvu mwili haraka, huifanya ngozi kuwa nyororo, huzuia asidi, husafisha damu na ina uwezo wa kuua vijidudu mwilini.
Lamba asali kijiko kimoja cha chai asubuhi kabla hujala kitu chochote. Kwa kuwa asali ni tamu lamba mara 3, wagonjwa wa kisukari wanashauriwa kuila kwa tahadhari.

Tende.
TENDE
Tende ambayo ni maarufu sana katika nchi za Arabuni na ukanda wa mwambao wa Tanzania ni miongoni mwa vyakula vyenye faida kubwa mwilini. Sifa ya kwanza ya tende ni uwezo wake wa kuupa nguvu moyo dhaifu na kuupa nguvu mwili (energizer). Wale wenye matatizo ya moyo kukosa nguvu tende zitawasaidia. Tende nayo ni mlo tosha unaopaswa kuwepo katika orodha ya milo yetu ya kila siku.
WEKA TANGAZO

0 maoni: