SHTUKA MREMBO: MAMBO MUHIMU YA KUFANYA BAADA YA KUTENDWA NA UMPENDAE...!
WEKA TANGAZO
Mweleze ukweli
KATIKA MAISHA YA KIMAPENZI HAKUNA KITU
KINACHOUMA KAMA KUSALITIWA, TENA KUSALITIWA KUNAKOUMA ZAIDI NI PALE
UNAPOBAINI MPENZI WAKO KAMPA PENZI MTU UNAYEMJUA HALAFU UKIJILINGANISHA
WEWE NA HUYO ALIYEPEWA UNASHINDWA KUELEWA KILICHOMSHAWISHI MPENZI WAKO
KUMPA PENZI HUYO MTU...
Niseme tu kwamba wapo wachache
waliotulia ila asilimia kubwa ya walio kwenye uhusiano ni wasaliti hata
tafiti zimethibitisha hilo. Kama hali yenyewe iko hivyo, cha kujiuliza
ni kwamba unapobaini mpenzi wako kakusaliti ni kipi unachotakiwa
kufanya? Je, ni kuamua kunywa sumu kama ambavyo wamekuwa wakifanya
wengine? Sidhani kama huo ni uamuzi sahihi.
Yafuatayo baadhi ya mambo ambayo unapaswa kuyafanya baada ya kubaini kuwa mpenzi wako amekusaliti.
Kubaliana na kilichotokea
Kama keshakusaliti ni tukio ambao
limeshatokea na haliwezi kufutika. Kubali kuwa umetendwa, huzunika
lakini mwisho liache lipite ili uweze kujipanga upya.
Usijilaumu
Wapo ambao wakishasalitiwa hujuta kukubali kuingia kwenye uhusiano na
watu waliowatenda. Utamsikia mtu akisema “najuta kumkubalia awe mpenzi
wangu”. Kujilaumu kwa namna hiyo hukutakiwi kwani kutakufanya uzidi
kunyong’onyea.
Jitoe
Jifanye kama vile aliyesalitiwa siyo wewe bali ni rafiki yako kisha
jiulize ungemshaurije? Ushauri ambao ungempa basi uchukue kisha uufanyie
kazi.
Pima ulivyoathirika
Je, kitendo cha mpenzi wako kukusaliti
kimekukosesha imani juu yake? Kama ni hivyo, unadhani una sababu ya
kuendelea kuwa naye au unahisi madhara aliyokupatia huwezi kumvumilia?
Kwa vyovyote utakavyoamua ni lazima
umweleze ukweli juu namna alivyokuumiza kwa usaliti wake. Hata kama
utampa nafasi nyingine lazima ajue jinsi alivyokuumiza ili iwe
changamoto kwake.
Chunguza kwa nini kakusaliti
Usiliache likapita hivi hivi, unatakiwa kujua sababu ya yeye kukusaliti.
Je, kuna ambacho anakikosa kwako au ni tamaa zake tu? Jibu
utakalolipata litakusaidia katika maisha yako ya kimapenzi.
Usikubali akulainishe
Huenda huyo mpenzi wako ni msanii na anaweza kukulainisha kwa maneno
ambayo yanaweza kukufanya ukalichukulia tukio hilo kiurahisi. Kuwa na
msimamo na eleza hisia zako kwa uwazi.
Amua kusuka au kunyoa
Likishatokea hilo jaribu kuzungumza na moyo wako. Uamuzi wa kuendelea
kuwa naye au kumuacha uuchukue bila shinikizo. Hata kama kakuumiza, kama
unadhani unaweza kumpa nafasi nyingine mpe ili usije ukajuta baadaye
kwa kumkosa lakini kama unaona moyo wako unamkataa, muache.
WEKA TANGAZO
0 maoni: