ASILIMIA 26.5 YA WANAWAKE HUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE
WEKA TANGAZO
Wakati idadi ya wanawake wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi
ikiongezeka, asilimia 26.5 ya wanawake Tanzania wamebainika kuwa
wanafanya mapenzi kinyume na maumbile.
Mfumo wa uzazi unaharibika
Watafiti
wanabainisha kuwa kitendo hicho licha ya ukweli hakifai kwa vile
kinaharibu mfumo wa uzazi, kina athari kubwa mno kwa mwanadamu, mojawapo
ni ikiwemo uwezekano mkubwa wa wahusika kuambukizana virusi vya Ukimwi
kwa vile hakuna vilainishi, hivyo kusababisha michubuko ambayo ndio njia
kuu ya kuambukiza vijidudu hivyo.
Mtafiti Mwanasayansi, Irene Mremi kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa
Magonjwa ya Binadamu nchini Tanzania (NIMR) alitoa ripoti hiyo hivi
karibuni hapa jijini Dar Es Salaam.
Mremi akiwa na jopo la watafiti kutoka NIMR anasema kuwa wanawake hao
wamesema chanzo kikubwa kinacho wapelekea kufanya ngono kinyume na
maumbile ni kujipatia kipato zaidi na Kuogopa kupata Mimba.
Vilevile
alizitaja sababu nyingine za wanawake kufanya mapenzi kwa njia hiyo ni
kulinda usichana wao na baadhi ya mila na tamaduni za baadhi ya
makabila.
Sampuli za utafiti
Utafiti huo ulikusanya sampuli kutoka katika mikoa ya Dar es salaam, hasa maeneo ya Kinondoni, Tanga, Makete na Siha.
Mremi anasema “Utafiti wetu uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika
kuanzia miaka 15 na kuendelea na kada tofauti katika jamii kama
wanafunzi, wafanyakazi, wahudumu wa bar, wauguzi, makahaba na akina mama
wa nyumbani
Katika maeneo hayo watu 903 walijitokeza wakiwepo pia wanaume ambao walihusishwa katika utafiti huo.
Imani potofu kwa wanaume
Wanaume waliohojiwa wamesema wanafanya kwa ajili ya kupata raha tu na
imani ya kuwa huko hakuna maaambukizi ya VVU, kitu ambacho ni uongo,
kwani huko ndiko kwenye kuchangia ukimwi kwa haraka zaidi kuliko sehemu
nyingine yoyote.
WEKA TANGAZO
0 maoni: