WANAWAKE WANAVYOSABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
WEKA TANGAZO
WEKA TANGAZO
JE WAJUA WANAWAKE WANAVYOSABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
Kesi ya wanaume kupungukiwa nguvu
za kiume zimezidi kushika kasi, kiasi cha kufanya dawa za kuongeza nguvu
hizo kuwa maarufu na zenye mahitaji makubwa katika jamii.
Waganga wa kienyeji wamekuwa
wakitumia dawa hizo kama tiba ya msingi ya kuwavutia wateja kwenye
biashara zao. Hii inaonesha kuwa tatizo hili ni kubwa miongoni mwa
wanaume wengi katika jamii yetu.
Hata hivyo, utafiti unaonesha
kwamba wengi kati ya wanaume waliowahi kutumia dawa za asili na zile za
hospitali kuondokana na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume
hawakufanikiwa kupata tiba ya kudumu, matokeo yake wamegeuzwa kuwa
watumwa wa kila wanapotaka kushiriki tendo lazima wabwie ‘kolezo’ la
kuwasaidia kuamsha hisia zao.
Kwa wanaume, ukosefu wa nguvu ni
jambo linalouma na kuondoa kabisa ujasiri. Wengi kati yao wako tayari
kutumia pesa na uwezo wao wote kuhakikisha kuwa heshima ya tendo la ndoa
ikuwa katika miliki yao daima.
Lakini, watafiti wa masuala ya
mapenzi nikiwemo mimi, tumegundua kuwa wengi kati ya hao wanaolalamika
kupungukiwa nguvu za kiume, hawafahamu chanzo cha matatizo na namna
wanavyoweza kuepukana na kasoro hizo.
Ushahidi uliopatikana kwa
waathirika wa tatizo hili, unaonesha kuwa wanaume wanapokabili upungufu
wa nguvu za kiume huishia kujuta na kujilaumu wenyewe bila kutazama
upande wa pili wa washirika wao, namaanisha wanawake.
Zipo kesi za wanaume kujiua au
kujinyofoa sehemu zao za siri kwa sababu ya kushindwa katika tendo la
ndoa. Hali hii inatoa picha kwamba wanaume wengi hujitwika mzigo wa
lawama wenyewe.
Dokta Bianca P. Acevedo kutoka
Chuo Kikuu cha California, Santa Barbara anasema, wanawake huchangia kwa
kiasi kikubwa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, jambo ambalo nami
nalithibitisha kwa ushahidi wa kitaalamu ufuatao:
1: KAULI
Miongoni mwa mambo ambayo mwanaume
hataki kuyasikia yakitoka kwenye kinywa cha mwanamke ni kuambiwa HAWEZI
TENDO LA NDOA. Mwanamke akimwambia mwanaume wakati au baada ya tendo
kuwa hawezi, atakuwa amemsababishia tatizo kubwa la kisaikolojia ambalo
litampelekea kupotea nguvu za kiume taratibu.
Msaada unaohitajika kwa mwanamke
anayekutana na mwanaume dhaifu kwenye tendo si kumwambia hawezi, bali ni
kumtia moyo na kumsaidia kuweza. Wanawake wamewasababishia waume zao
upungufu wa nguvu za kiume kwa kuwaambia maneno kama haya: “Yaani siku
hizi sijui umekuwaje, yaani huwezi kazi kabisa!”
2 : UJUZI
Wanawake wengi hasa waliopo kwenye
ndoa, wanapuuza ujuzi kwenye tendo la ndoa. Hawajishughulishi kumsaidia
mwanaume ‘kuwika’, si wabunifu na watundu, jambo hili humfanya mwanaume
kushiriki tendo kwa kutegemea kupanda kwa hisia zake mwenyewe, hivyo
anapokuwa amechoka au ana mawazo, hawezi kusisimka kwa vile hapati
ushirikiano toka kwa mwenzake.
Pamoja na wengi kutokuwa wajuzi,
lakini wapo wengine ambao ni watundu mno kwenye sita kwa sita kiasi cha
kumfanya mwanaume ajione kama mgeni wa mchezo huo.
Kimtazamo, wanaume hupenda sana
ushindi wakati wa ‘kazi’, lakini pale wanapogeuzwa ‘chekechea’ hupunguza
uwezo wa kujiamini na kuruhusu hofu kuongezeka mawazoni mwao, hivyo
kuwasababishia tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Inashauriwa kwamba, mwanamke
anapokuwa na uelewa mkubwa wa masuala ya mapenzi hasa wakati wa tendo,
asioneshe kiwango kikubwa kwa haraka bali amchukulie mwenzake kama
mwanafunzi, asiwe na maneno kama: “Leo nakuja kukupa vitu adimu kuliko
vya juzi, hakuna kulala kasi mtindo mmoja.” Kauli hizi huwaogopesha
wanaume na kuwafanya wapungukiwe na nguvu.
USAFI
Mwanamke anapokuwa si msafi,
huweza kumsababishia mwanaume matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume.
Sote tunafahamu umuhimu wa usafi wa mwili na kero za uchafu wakati wa
tendo, hivyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa mchafu atamfanya mwanaume
apoteze msisimko na uwezo wa tendo la ndoa. Unadhifu wa mavazi na mwili
ni muhimu sana katika mapenzi.
GUBU
Jambo lingine linaloweza
kumsababishia mwanaume upungufu wa nguvu za kiume ni gubu au karaha za
maneno ya uchokozi yasiyokuwa na kichwa wala miguu. Uchokonozi wa mambo,
ugomvi, usaliti na hali ya kutokuwa na staha ni mambo yanayosababisha
tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Mwanamke anapokuwa mwingi wa
maneno ya kashfa, dharau na matusi huweza kumfanya mume amchukie na
kutopenda kushiriki naye tendo. Uchunguzi unaonesha kwamba wanawake
walioolewa wenye tabia hii, huwafanya waume zao wawe na msisimko wa
kimapenzi kwa wanawake wa nje kuliko wake zao hao.
USALITI
Tabia
ya usaliti kwa mwanamke ni chanzo kingine cha mwanaume kupata tatizo la
upungufu wa nguvu za kiume. Mwanaume anapoona, kuhisi au kubaini kuwa
anasalitiwa, huumia sana moyoni, maumivu ambayo hatimaye humfanya
muhusika kuwa na mawazo mengi ambayo humuondolea hamu ya tendo.
0 maoni: