WEMA NA DIAMOND WAPEANA MAHABA LIVE BARABARANI.
WEKA TANGAZO
MASUPASTAA
ambao ni wachumba (wanasema wenyewe), Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na
Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, walijikuta wakionesha upendo wao
mbele za watu kwa kudendeka barabarani.
Ishu hiyo
ambayo wapendanao wengi huifanya kwa faragha, ilijiri hivi karibuni
maeneo ya Bamaga- Mwenge jijini Dar es Salaam ambapo ni hatua chache
kutoka kwenye Ofisi za Global Publishers ambao ni wachapishaji wa
Magazeti Pendwa ya Amani, Risasi, Uwazi, Ijumaa, Championi na Ijumaa
Wikienda.
ILIVYOKUWA
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, Wema alikuwa kwenye shughuli zake za kila siku maeneo hayo ambapo alikuwa ameegesha pembeni gari lake la rangi ya pinki aina ya Toyota Lexus Harrier bila kujulikana alikokuwa ameelekea.

DIAMOND AIBUKA PEKE YAKE
Ikadaiwa kuwa, mara Diamond naye alitokea bila kujulikana alikotokea akiwa anaendesha gari lake aina ya Toyota Prado na kuegesha gari lake jirani na alipoegesha Wema.

SIMU YAPIGWA CHUMBA CHA HABARI GLOBAL
Mapaparazi wa Global wakiwa katika kazi za kila siku ndani ya ofisi, simu ilipigwa kwa mmoja wao na kutonywa kuhusu wawili hao kuwepo eneo hilo kimahabamahaba.

“Jamani
Global hapa jirani na ofisi zenu Diamond amekuja sasa hivi, lakini
inaonekana amemfuata Wema maana Wema alishakuwepo muda mrefu uliopita,
njooni mchukue picha si ndiyo zenu au bado mna bifu na Wema tangu siku
ile alipokuja kuwafanyia fujo?”
PAPARAZI AWAFIKIA
Haraka sana paparazi mmoja alibeba kamera yenye uwezo wa kupiga picha kwa umbali wa mita hata 250 bila mhusika kushtukia na kutoka nayo.

Kweli,
lilikuwa tukio lilionesha kushangaza kwani paparazi alikuta wapita njia
wakiwa wanapunguza mwendo ili kuwashuhudia wawili hao walichokuwa
wakikusudia kukifanya bila kuogopa watu.
WEMA NJE, DIAMOND NDANI
Kamera ya paparazi wetu iliweza kuwanasa wawili hao, Wema yeye alisimama nje ya gari la Diamond upande wa dirisha la dereva na kuongea na mwandani wake huyo jambo ambalo hakuna mpita njia aliyeonekana kushangaa.
Hata hivyo, mshangao ulianza pale Diamond alipotoa mkono nje na kumshika kiuno Wema huku wakiendelea kuongea ndipo baadhi ya wapita njia nao walipokoleza macho kodo, wengine wakihoji kama aliyesimama nje ya gari ni Wema, nani alikuwa ndani ya gari hilo!

Haikuwa
rahisi kupata majibu kwani wengi walikuwa wanashindwa kumwona Diamond.
Wengine waliamini kwamba, Wema alikuwa ameshikwa kiuno na mwanaume
mwingine ambaye huena akampindua Diamond kama na yeye alivyompindua yule
kigogo wa ikulu ‘CK’.
“Sasa mbona
Wema anakubali kushikwa kiuno hivihivi tu, haoni watu?” alihoji mpita
njia mmoja ambaye alijitambulisha kwa jina la Salome, mwanafunzi wa Chuo
cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar.
DENDA NJE NJE
Katika hali isiyotarajiwa, baada ya kushikwa kiuno, Wema alikwenda mbali zaidi pale alipomwinamia ‘baby’ wake huyo na kula naye denda ambapo naye mwanaume hakufanya ajizi hata kidogo.

“He! Jamani!
Naona wenzetu leo wameamua, hata barabarani? Huu ustaa nahisi
unawafanya watu wawe vichaa mbele za watu. Mimi siwezi kabisa kudendeka
mbele za watu,” alisema mrembo mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake
lakini naye ni denti wa Chuo cha Ustawi wa Jamii ambacho kipo jirani
kabisa na eneo la tukio.
DIAMOND ACHOMOKA KWA KASI
Baada ya denda hilo lililodumu kwa dakika moja, Diamond alimuaga Wema na kukanyaga mafuta kuondoka katika eneo hilo huku wananachi wakimfuatilia kwa macho yaliyojaa mshangao.

-GPL
WEKA TANGAZO
0 maoni: