MSANII WA FILAMU MAINDA AGEUKIA KWENYE UIMBAJI AANZA NA INJILI
WEKA TANGAZO
MSANII wa
sinema Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ aliyewahi kutamba na filamu za
kidunia, sasa ameamua kuimba muziki wa Injili ikiwa ni kumtukuza Mungu
na kujiandalia maisha mema ya peponi.
Akipiga
stori na mwandishi wetu juzi, staa huyo aliyekuwa akiitwa Mwanaidi na
kubadili jina baada ya kuokoka, alisema: Vijana siku zote tuna nguvu,
tuna muda wa kutosha hivyo tunapaswa kumtumikia Mungu siyo mpaka
tuchoke, tuzeeke au tufanye kwanza dhambi ikifika omega (mwisho) ndiyo
unamkumbuka Mungu.
“Ninaimba kwaya tena sauti ya tatu, subirini muone ujio wangu mpya kwani nimeamua kumtukuza Mungu aliyeumba mbingu na nchi.”
WEKA TANGAZO
0 maoni: