JE WAJUA MAPENZI; HUWEZI KUTONGOZA ? BASI USIJALI SIMU YAKO INAWEZA KUKUSAIDIA SANA..CHEKI HAPA
WEKA TANGAZO
Ni siku
nyingine nzuri tunapokutana mambo mbalimbali yanayohusu uhusiano wa
kimapenzi na leo, napenda kujadili na wewe msomaji wangu juu ya hili
suala nililolitambulisha hapo juu.
Maendeleo
ya teknolojia yamebadilisha mambo mengi katika maisha yetu ya kila
siku. Zamani ilikuwa kama kuna mwanamke au mwanaume unampenda, basi
lazima ‘umfukuzie’ kwa kumvizia vichochoroni mpaka utakapopata nafasi ya
kuzungumza naye, na kama huna ujasiri wa kumtongoza ana kwa ana basi
ndiyo umemkosa.
Lakini siku
hizi mambo yanamalizwa kidijitali. Hata kama wewe ni ‘domo zege’, simu
yako ya mkononi inaweza kukusaidia kumpata mwanamke au mwanaume wa
maisha yako. Lakini je, hivi ni wote wanaojua namna ya kutumia simu
kuanzisha uhusiano wa kimapenzi?
Ni matumaini
yangu kuwa mada hii itakusaidia wewe ambaye muda wa kuoa umefika lakini
kwa sababu moja au nyingine, huwezi kumwambia ana kwa ana mtu
umpendaye. Kumbuka kuwa penzi bora ni lile ambalo wawili huanza kwa kuwa
marafiki, ni makosa kukurupuka kumtongoza mtu kwenye simu bila kumvuta
kwanza karibu.
Hatua ya
kwanza, ukishapata namba ya simu ya huyo umpendaye, tafuta muda ambao
utakuwa umetulia kisha mpigie na jitambulishe. Mweleze kwamba umempigia
simu kumjulia hali, kama akikuuliza mahali ulikoipata namba yake,
unaweza kumjibu vyovyote lakini inashauriwa kuwa siyo vizuri kumtajia
aliyekupa namba yake kwa sababu unaweza kuwagombanisha.
Usiwe na
papara, mtakie siku njema na endelea na shughuli zako nyingine. Unaweza
pia kuendelea kumtumia meseji za kawaida (siyo za mapenzi), ukimjulia
hali, ukimuuliza kama ameshakula au amekula chakula gani, anafanya nini
kwa muda huo na vitu anavyovipenda sambamba na vile asivyovipenda.
Endelea
hivyo kwa muda, siri kubwa ambayo huijui ni kwamba watu wengi, hasa
wanawake huwa wanapenda kujua kuwa mtu fulani anamjali kwa kumuuliza
mambo mbalimbali yanayohusu maisha yake ya kawaida.
Jitahidi
kuwa mcheshi lakini usizidishe masihara. Ukishafanikiwa kumvuta karibu
yako na kumfanya aamini kwamba huwa unamfikiria mara kwa mara, sasa
unaweza kupiga hatua moja mbele kwa kufanya yafuatayo:
MBINU ZA KUMTEKA
Tumia sauti ya utulivu yenye hisia ndani yake, utazidi kumvuta karibu yako. Usipende kuzungumza kwa sauti ya juu au kupayuka au kupiga simu ukiwa kwenye kelele. Akipokea tu simu yako, mjulie hali yake kisha msifie kidogo kuhusu sauti yake na namna anavyozungumza.
Tumia sauti ya utulivu yenye hisia ndani yake, utazidi kumvuta karibu yako. Usipende kuzungumza kwa sauti ya juu au kupayuka au kupiga simu ukiwa kwenye kelele. Akipokea tu simu yako, mjulie hali yake kisha msifie kidogo kuhusu sauti yake na namna anavyozungumza.
Msimulie
kidogo kuhusu siku yako inavyokwenda, tumia maneno machache lakini
yatakayomfanya asiboreke kukusikiliza. Ifanye stori yako iwe ya kuvutia
kwa kutumia maneno matamu yatakayomfurahisha na kumfanya aache kila
anachokifanya na kukusikiliza.
Badili
mazungumzo, muulize kama anajua kwamba yeye ni mzuri sana na hujawahi
kukutana na mtu anayevutia kama yeye. Kama wewe ni mwanaume na
unayezungumza naye ni mwanamke, utakuwa katika nafasi nzuri ya ‘kum-win’
kwa sababu wanawake wengi wanapenda sana kusifiwa.
Akiwa
amekolea na sifa unazomwagia, mweleze kwamba unavutiwa naye na unatamani
kuwa na mpenzi anayefanana naye. Zungumza naye kwamba atakapokubali
kuwa na wewe, utamtunza na kumlea kama malkia, mweleze malengo yako ya
baadaye katika uhusiano wenu endapo atakukubalia.
Usimpe
nafasi ya kukwambia kama amekubali au amekataa bali hitimisha mazungumzo
yenu kwa kumtakia siku njema au kazi njema. Bila shaka utamuacha akiwa
na shauku kubwa ya kuendelea kusikiliza ‘mistari’ yako.
Endelea
kuwasiliana naye kwa mambo ya kawaida huku ukimpima kama yale
uliyomwambia anayachukuliaje. Kama naye amekupenda, utaanza kuona
mabadiliko kuanzia meseji atakazokuwa anakutumia, namna anavyopokea simu
yako na uchangamfu anaokuonesha.
Kama bado
haoneshi dalili zozote za kukuelewa, basi jua hajavutiwa na wewe na
ukiendelea kuzungumzia mambo ya mapenzi, huenda ukaanza kumboa lakini
kama ana dalili za kuingia kwenye kumi na nane zako, endeleza
mawasiliano naye,
omba
kukutana naye sehemu tulivu kama ufukweni au popote ambapo mtakuwa
wawili na hapo utakuwa na nafasi nzuri ya kueleza kwa kina juu ya hisia
zako, utafikia wakati mtaelewana na kuoana.
-GPL
WEKA TANGAZO
0 maoni: