MAJANGA! NAY WA MITEGO ATOA VITISHO VYA KUUA, ASAKWA USIKU NA MCHANA.

WEKA TANGAZO KIMENUKA! RB namba KT/RB/1178/2014-KUTISHIA KUUA KWA NJIA YA MTANDAO inamsaka staa wa Ngoma ya Nakula Ujana, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kwa tuhuma ya kutishia kumuua mdogo wake aliyetajwa kwa jina la Amani Shija.

Kwa mujibu wa chanzo makini, Nay alikuwa akiishi na Shija kwa zaidi ya miaka mitano nyumbani kwake, Manzese jijini Dar. 
Habari zilitonya kuwa ugomvi wa Nay na Shija ulianza zaidi ya miezi mitatu iliyopita ambapo hivi karibuni walikuwa maeneo ya Kijitonyama, Dar, wakipata chakula cha usiku na marafiki zao wengine ndipo ghafla dogo akajichanganya na kujikuta akiropoka neno lililomuudhi Nay, akapaniki. 
Ilisemekana kwamba baada ya kupaniki, Nay alianza kumfokea Shija na kutishia kumuua, ambaye alishindwa kujizuia na kujikuta akimwaga chozi. Akaendelea kueleza kuwa hata baada ya siku hiyo, Nay aliendelea kumtumia SMS za kutishia kumuua ambazo bado anazo kama ushahidi Baada ya kudaka mchongo huo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Shija ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva na kumuuliza juu ya malalamiko hayo, akakiri kugombana na kaka yake huyo.
Alikwenda mbele zaidi na kudai kuwa Nay amekuwa akiendelea kumtishia kumuua jambo linalomfanya aishi kwa shaka mjini.
Alisema ili kujilinda ndipo alipoamua kulifikisha suala hilo kwenye Kituo cha Polisi Kitunda, Dar anakoishi kwa sasa kisha kufunguliwa jalada la kesi namba KT/RB/1178/2014 KUTISHIA KUUA KWA NJIA YA MTANDAO.
Gazeti hili lilimtafuta Nay bila mafanikio lakini kwa mujibu wa mtu wake wa karibu, baada ya kujua msala huo ametorokea nchini China.

-GPL WEKA TANGAZO

0 maoni: