Wanawake Walioachika Wana Visingizio Vingi, Wanawadanganya Wasio Olewa-Shtuka
WEKA TANGAZO
Nimegundua ya kwamba wanawake wengi walio achika katika ndoa zao wana ushuhuda wa uwongo kwa wanawake wasio olewa.
Utamkuta mdada mzima amezalishwa halafu ameachwa kwa makosa yake
anawaambia wanawake wasio olewa kwamba kuolewa kitu gani, kwani wewe
huwezi kuendesha maisha bila mwanaume, kwani mwanaume nani bwana
asikunyanyase , watu tumeona wanaume sembuse magume gume, mwanaume kitu
gani bwana, wewe waza maendeleo yako ,usiwaze kuolewa ,kuolewa ni
kupoteza muda , kuolewa ni kutiana umaskini tu.
Katika hali isiyo ya kawaida wanawake hao wakipata tena waume wa kuwaoa
utaona wanaolewa,halafu cha ajabu hamna shughuri yoyote ya maendeleo
wanayofanya zaidi ya kutwa kujadili wanaume za wtu na kuendelea
kuzalishwa tu nyumbani.
Waacheni mabinti waolewe na si kuwaharibu kisaikolojia kwamba kuolewa
hakuna maana na maana zaidi kuzalia nyumbani kila mtoto na babake.
Waacheni kila mtu akaone yeye wenyewe. Kama wewe umeachika wacheni
wakajaribu maisha.
Kama una binti yako mzuie kuambatana na akina mama waliotendwa.
WEKA TANGAZO
0 maoni: