Simu ya mkononi yaathiri mbegu za kiume
WEKA TANGAZO
WEKA TANGAZO
Tathmini ya utafiti kutoka chuo
kikuu cha Exeter nchini Uingereza, inaonyesha kuwa kiwango cha mbegu za
uzazi za wanaume huathiriwa kwa kuweka simu za mkononi kwenye mifuko ya
suruali.
Hata hivyo ,mwanasayansi wa maswala ya uzazi na
shahawa,anasema kuwa ushahidi huo bado hauna uhakika wowote hivyo basi
simu yake bado inaendelea kukaa mfukoni mwako
Uchunguzi huo uliochapishwa katika
jarida la 'Environment International' ulilaumu mnunurisho wa
kielectromagnetiki kuwa chanzo kikuu kinachoathiri mbegu za wanaume.
Wataalamu walichanganua utafiti tofauti kuonyesha ubora wa shahawa wakihusisha wanaume 1,492.
Hii ilijumuisha kupimwa kwa shahawa zilizowekwa
wazi kwa mnunurisho wa simu za rununu, kwa maabara na udadisi wa wanaume
katika kliniki za uzazi
Kiongozi wa uchunguzi huo Dkt.Fiona Mathews
aliambia BBC kuwa kutokana na uchunguzi huo,mmoja tu ndio ulionyesha
uhusiano kati ya utumizi wa simu na kudidimia kwa ubora wa shahawa.
"Nafikiri kwa mwanamume wa makamu hakuna haja ya
kuingiwa na hofu,iwapo unajua una uwezekano wa kuwa na shida ya kizazi
basi itakuwa jambo la busara kutoweka simu mfukoni ,pia kugeuza mtindo
wako wa kula."
'Uchunguzi zaidi'
Alikubali kukosolewa na wanasayansi wengine huku akiunga mkono kuwa kuna umuhimu wa kufanya uchunguzi zaidi.
Dkt,Mathews alimaliza kwa kusema"hili ni jambo
la kusisimua lakini hatusemi kwa uhakika kuwa kila anayebeba simu
mfukoni atakuwa na shida ya kizazi."
Dkt.Allan Pacey kutoka chuo kikuu cha Sheffield
anasema kuwa wazo hilo la kudidimia kwa shahawa na kuharibu "DNA"
linatokana na mnunurisho wa kielectromagnetiki zinazopatikana kwenye
simu na pengine joto aidha moja kwa moja kutoka kwenye simu au
mnunurisho.
Dkt huyo anayefanya uchunguzi wa shahawa bado
hajashawishika akisema ushahidi huo hauna msingi na ataendelea kuweka
simu mfukoni.
Aliambia BBC,"kumekuwa na shauku kwa mda kama
kuweka rununu mfukoni kunaweza changia kudidimia kwa ubora wa shahawa na
nguvu za kiume kivyovyote.
"Kumekuwa na habari zisizokuwa na msingi lakini
kwa maoni yangu uchunguzi uliofanywa hadi kufika sasa haujakuwa wa
kutosha kwa sababu wachunguzi aidha hawakuhifadhi shahawa vile inavyofaa
ama wamedadisi matumizi ya simu kati ya wanaume bila kuzingatia mambo
mengine kama mitindo yao ya maisha.
"Tunayohitaji ni uchunguzi kufanywa ambapo utumizi wa simu unazingatiwa vile vile tabia zinazoathiri maisha yao.
Hadi pale tutakapo tafakari hayo,nitaendelea kuweka simu yangu katika mfuko wa mkono wa kulia wa suruali yangu!"
0 maoni: