Mradi wa reli mpya watiwa saini Nairobi

WEKA TANGAZO
Waziri mkuu wa Uchina Li Keqiang
Waziri Mkuu wa Uchina, Li Keqiang, na viongozi wa Afrika Mashariki wametia saini rasmi makubaliano ya kujenga njia mpya ya reli itayounganisha mji wa Kenya wenye bandari, Mombasa, hadi Nairobi, Rwanda na Sudan Kusini.
Waziri Mkuu wa Uchina yuko mjini Nairobi akiwa katika ziara ya Afrika.
Njia hiyo ya reli ya upana unaotumika kawaida duniani itagharimu mabilioni ya dola, na itachukua nafasi ya njia ya reli ya sasa ambayo ni nyembamba na ilijengwa zama za ukoloni wa Uingereza.
Sehemu ya kwanza ya reli itajengwa na kampuni za Uchina - jambo lilozusha malalamiko kwamba kampuni nyengine hazikuruhusiwa kushiriki
WEKA TANGAZO

0 maoni: