MAPENZI; KULA CHAKULA CHA USIKU WAKATI WA GIZA KUNAPONGUZA UTAMU WA MCHEZO..CHEKI HAPA

WEKA TANGAZO
MMH jamani ndiyo nini kuninunia kwa kusema ukweli? Siku zote dawa ya jipu ni kulitumbua kwani ukilionea huruma utamuongezea maumivu mgonjwa.
Nataka kukwambia kitu kimoja kwamba chuki nichukie roho yangu niachie, wee sema wee na upige mayowe lakini ukweli utabaki palepale, kaniki haiwezi kubadilika rangi na kuwa nyeupe, ujumbe umefika au siyo?
Natamani kucheka kwa jicho unalonikata na huku ukijisemea moyoni mwako kuwa siku ukinitia mikononi utanipasha nipashike, wapiiii, wan’kula huu na hasara juu.
Hivi wee mung’unya jeuri ya kutaka kunipasha umeipata wapi? Kwa taarifa yako tu, hicho ni  kiburi cha nazi kutaka kushindana na jiwe.
Jamani leo nataka nizungumzie raha ya kusafiri, siku zote, wanaume kwa wanawake wanapenda kusafiri usiku, tena kukiwa na giza totoro, kweli si kweli?
Basi nawaambia raha ya safari ni mchana au hata kama ni usiku mwangaza uwepo babuuu…shurti mtu upate fursa ya kuona kule uendako.
Utaujua mji, utaona mandhari yake na kufaidi kuliko kusafiri usiku au kukiwa na giza.
Ndiyo, watu wanalipenda giza hawajui kuwa giza ni la mwizi, maana hata kama kuna taa wanazima na kuamua kusafiri gizani mpaka wanafika mwisho.
Jamani hakuna raha katika safari ya giza hata kidogo, kwani ukisafiri kweupe utaiona safari mwanzo hadi mwisho pia, mtu unapata fursa ya kuujua mji vizuri.
Umenielewa au nimekuacha umelewa? Kama haitoshi nataka nikwambie kwamba utamu wa chakula ukione kwa macho yako kikiwa kwenye sahani safi.
Hapo hata kijiko cha kulia nacho ukikishika kinatulia mkononi. Utayaona maandalizi yaliyofanywa mezani na kukufanya uwe na hamu ya chakula ambacho machoni kitaonekana kuwa ni kitamu na kitakupa hamu ya kula, bado upo?
Hata ukila chakula huku unakiona ukisindikizwa na chombezo la maneno matamu hakika hutachoka kukitafuna kwa madaha huku utamu ukinoga na chenyewe kikikata kona katika mwili wako.
Eeeeeeeeeehe! Acha nisema miye kwani  nisiposema leo nitasema lini?  Unadhani nitasema nikiwa ndani ya kaburi?
Kawaida ya wanawake huwa tuna milio yetu wakati wa safari, huwa tunahema kwa mihemo yenye kuongeza mahanjamu pale safari inapokolea.
Jamani kuhema au kuzungumza kwa raha hutuongezea raha na kutufanya tuione safari kuwa ni fupi hata kama ni ndefu.
Umeshanipata ninaposema kusafiri kweupe kuna raha yake?  Kama hujanipata baki na ubozi wako.
Wanawake tumeshazoea kuzungumza tukiwa safarini lakini wengine tuna aibu utatujua kwamba tunafurahia safari kwa kututazama katika midomo au kwenye macho yetu.
Safari ikikolea utatuona tunajilamba midomo ujue hapo raha iko chini na utamu uko juu, hapo jicho hupoteza kiini chake kile cheusi, mwanaume akiwa na moyo mwepesi atajua mtoto wa watu anataka kukata roho, kumbe mwenzako hadithi imekolea na raha zimeshinda kibaba.
Nia kubwa ya kuyasema maneno haya, kuna mtu alikuwa akisafiri na mpenzi wake gizani, jamani kumbe mpenzi wake alikuwa na pumu, kwa vile si muongeaji alikuwa akiogopa kusema kama alikuwa anaumia.
Mwishowe binti akazidiwa, jamaa bila kujua kama binti alikuwa amepoteza fahamu muda mrefu, alikuwa akiendelea na muziki wake.
Laiti kama wangekuwa wanasafiri kweupe mwanaume angejua mwenzake alikuwa katika hali gani.
Pia, mwanaume anapokuwa akicharaza gitaa lake akiona mnenguaji wake anakwenda ndivyo sivyo si atasimamisha muziki ili amuulize mnenguaji wake inakuwaje muziki umeshafika kwenye sebene halafu anashindwa kuchanganya?
Hapa mwanamke anaweza kusema kuwa kasi ya gitaa inampa matatizo, hivyo akakutaka upige muziki wako taratibu lakini kama mko gizani huwezi kujua mwenzako anafurahiaje au anaumiaje.
Tusipende kula vyakula vyetu gizani, raha ya kula ule ukiwa unakiona chakula na unamuona mwenzako kakaaje, ananenguaje, anafurahiaje tena hutaweza hata kumchezea rafu na kumuumiza.
Raha ya safari msafiri kukiwa kweupe ili ujue mandhari ya mji, upo? Kama haupo  kalagabhao.

-Shaddyclassic
WEKA TANGAZO

0 maoni: