STORY: THE WORLD IZ NOT FAIR MTUNZI: Chicolove NAMBA: 0765,0658,270133 SEHEMU : 3

WEKA TANGAZO Ebu nitolee hapa us*ng* utakujaje kazini huna ela ya kula?
"Nikamtazama yule dada kwa hasira kali sana nilitamani nimrukie na kumchapa makofi!
"Uku wale wafanya kazi wenzangu wakinicheka kwa dharau!!
Ha ha ha ha dogo ulidhani hapa nyumbani nini ule bure?
"Sikumjibu yeyote maana nilisha jisikia vibaya moyoni mwangu!!
Nikasogea nikaenda kukaa chini ya mtu uku nikiangalia wenzangu wakiwa wanakula!!
"Hakuna hata mmoja aliyenikaribisha nikajiuliza ivi kweli binadamu ndio tulivyo usoni tunaonekana wema ila moyoni hatuko ivyo!!
"Baada tu yakumaliza kula wakapewa muda mchache wakupumzika uku wenzangu wakiwa wanaendelea kuvuta sigara na wengine bangi kutafuta stimu ya kazi"
"Kutokana na majibu ya yule dada nikajikuta nainua macho yangu juu nakusema eeh Mungu nipe moyo safi sije nikaingia katika jaribu la kumpenda msichana yeyote hapa duniani!
"Nilichukia sana majibu ya yule binti moyo wangu ukajenga chuki kwa wadada wote nikaona wote watakua walewale tu!!
"Basi kazi ikaendelea tena kama kawaida nikiwa na njaa yangu, kiu cha maji nikajikaza ivyoivyo nikaendelea kubeba zege langu!
"Mpaka kufika saa kumi jioni tulikua bado atuja maliza kila nikijaribu kumwangalia fundi mkuu labda atafunga kazi aoneshi dalili zozote!
"Nikajikuta nasema kimoyo moyo Eeh Mungu nitie nguvu najua wewe unanijua kuliko nijijuavyo nipe ujasiri wa kushinda yote katika hii dunia!
"Ilipokua inakaribia saa kumi na moja mara gafla nikaona lile gari la yule boss wangu Mustapha likiwa linakuja taratibu akapaki na kushuka uku akiwa anakagua kagua kazi!!
"Fundi inatakiwa ujitaidi kumalizia hapo kueka huo msingi nataka mmalize leo leo kesho tujue tunaanza kazi ingine
"Baada ya tajiri kutoa maelezo yake kwa fundi akatuamuru tukakoroge zege tena upya ya kumalizia huo msingi!
"Dogo pole umechoka ebu ingia hapo store toa mifuko mitatu ya cement tukoroge zege mara moja!
"Sawa nikaingia store nakutoa hiyo mifuko mitatu ya cement kama nilivyo agizwa nikaenda kuchota maji uku wenzangu wakiwa wanachanganya kokoto, mchanga na cement!!
"Bosi akawa anatuangalia tu pale uku akiwa anabinya binya simu yake ivi kama anaandika sms kutazama kule kwenye gari lake mara naona mlango unafunguliwa anashuka binti mmoja mzuri sana!
"Nikabaki nimeduwaa na mtazama alivyo mzuri alafu ni binti mdogo sana nikamgeuki yule bosi na kujiuliza ni mwanae au mpenzi wake?
"Mara nikasikia kibao cha mgongo paaah dogo ebu koroga zege acha kushangaa vitu vya wakubwa!

"Nikashtuka nakujikuta nimeropoka kwa bosi wangu nakusema.............ITAENDELEAAA
WEKA TANGAZO

0 maoni: