JE WAJUA WANAFUNZI 111 WAPATA MIMBA LINDI
WEKA TANGAZO
WEKA TANGAZO
Jumla
ya wanafunzi 111 wamepata mimba kwa kipindi cha mwaka 2012/13 katika
shule za msingi na sekondari mkoani Lindi na 1405 kati ya 8399
waliochaguliwa kujiunga elimu ya sekondari mwaka huu mkaoni Lindi
hawajafika kwenye shule hizo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo
utoro,
Hayo yamebainishwa na afisa elimu mkoa Silas Semaluku alipokuwa anazungumza na wadau wa elimu kwenye mkutano wa wadau wa Elimu mkoani Lindi.
Semaluku
alisema mkoa una kabiliwa na changamoto kubwa za watoto kupata mimba
kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo tamaa kwa watoto wakike kuwa na
vitu vya thamani ambazo zimeanza kufanyiwa kazi , na idara ya elimu
pamoja na wazazi,
Alisema
wilaya Lindi inaongoza kwa kuwa na watoto wengi waliopata ujauzito
ambao 48 ikifuatia wilaya Kilwa 23, Nachingwea 18, Ruangwa 14, Liwale 6
na manispaa ya Lindi 2.
Semaluku
alisema kuwa mkoa ulipangiwa wanafunzi 8,399 kati yao wasichana 4,078
na wavulana 4,321 lakini waliofika shuleni hadi sasa ni 6,994 pia
wanafunzi 1,405 hawajafika shule hadi sasa kati yao wavulana 720 na
wasichana 685.
Alifanunua
kuwa wanafunzi halmashauri ya wilaya Lindi kuna wanafunzi 327
wahajafiki shule hadi sasa, Liwale wanafunzi 230, Kilwa 200 Ruangwa 351
wilaya ya Nachingwea 226 huku Manispaa ya Lindi ikiwa na wanafunzi 69.
CREDIT - LINDI YETU
Mobhai.blogspot.com
0 maoni: