Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MUVI. Onyesha machapisho yote

JE WAJUA MWIGIZAJI YUSUF MLELA "NATAKA MWANAMKE ALIYENIZIDI UMRI ILI MAPENZI YADUMU".. CHEKI HAPA

0 maoni
Mwigizaji wa filamu za Kibongo, Yusuf Mlela ametoa kioja cha aina yake baada ya kufunguka kuwa akifika hatua ya kuingia kwenye ndoa anataka mwanamke atakayemzidi umri.
Yusuf Mlela.
Tofauti na vijana wengine ambao wanapenda kuoa wake wadogo kwao, Mlela alisema anaamini mwanamke akimzidi umri ndoa itadumu na maisha yao yatakuwa mazuri kwani atakuwa tayari ameshakomaa kiakili na atakuwa na uwezo mkubwa wa kuiendesha familia.
“Nahitaji mwanamke anayenizidi umri na sitaki nimzidi mimi naamini huyo tutaelewana na ndoa itadumu, sitaki mwanamke ninayemzidi umri mimi maana itakuwa shida kwani sijapangilia hivyo,” alisema Mlela.

MSANII WA FILAMU MAINDA AGEUKIA KWENYE UIMBAJI AANZA NA INJILI

0 maoni
MSANII wa sinema Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’  aliyewahi kutamba na filamu za kidunia, sasa ameamua kuimba muziki wa Injili ikiwa ni kumtukuza Mungu na kujiandalia maisha mema ya peponi.
Msanii wa sinema Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’
Akipiga stori na mwandishi wetu juzi, staa huyo aliyekuwa akiitwa Mwanaidi na kubadili jina baada ya kuokoka, alisema: Vijana siku zote tuna nguvu, tuna muda wa kutosha hivyo tunapaswa kumtumikia Mungu siyo mpaka tuchoke, tuzeeke au tufanye kwanza dhambi ikifika omega (mwisho) ndiyo unamkumbuka Mungu.
“Ninaimba kwaya tena sauti ya tatu, subirini muone ujio wangu mpya kwani nimeamua kumtukuza Mungu aliyeumba mbingu na nchi.”