Misri:Viongozi wakataza unenguaji viuno
WEKA TANGAZO
Ni densi ambayo isingekosekana kwenye sherehe muhimu. Harusi au burudani nyenginezo.
WEKA TANGAZO
Bodi ya kidini ya misri, imetoa
fatwa kukataza uonyeshaji wa kipindi kilichoanzishwa kwenye televesheni
nchini humo kuonyesha densi ya jadi ya wanawake wa misri ya kunengua
viuno almaarufu 'belly dance'.
Ngoma hiyo inayofanana na chakacha ya waswahili
imechezwa tangu zama za kale na imenakiliwa hata katika enzi za
ma-pharoah katika nchi hiyo ya Misri.
Maelfu ya watalii wanaoitembelea Misri hupenda
kwenda kuona inavyochezwa lakini mnamo siku za hivi karibuni wasichana
kutoka sehemu nyingi duniani hasa ulaya na hata uchina wameripotiwa
kwenda Misri kujifundisha jinsi ya kucheza densi hiyo.
Ni ajabu kuwa sasa imekuwa maarufu katika mataifa ya kigeni kuliko Misri kwenyewe ambako haichezwi ovyo ovyo hadharani.
Misri ni nchi ya waislamu wengi hivyo burudani
zina miiko yake- densi kama hizo hazichezwi hadharani hasa kwenye
mikusanyiko ya umma ya mchanganyiko wa wake kwa waume.
Hivi wale wanaozishabikia ni wachache kiasi kuwa
sasa kuna hofu kuwa huenda utamaduni au ustadi huo wa belly dancing
unakufa polepole Misri.
Pengine ni kwa kutambua hilo ndio waandalizi wa
vipindi wakaona bora walete shindano la ngoma hiyo kwenye televisheni ya
kitaifa kuhifadhi na kuipa umaarufu kama kitu cha asili ya Misri.
Lakini bila shaka hilo haliswihi machoni pa bodi ya kidini nchini humo na wametoa amri kipindi hicho kiondolewe mara moja .
Bodi hiyo Dar al-Ifta imesema kuonyesha watu
wakinengua viono kwenye televisheni kutazorotesha maadili ya jamii na
kutapelekea mwenye itikadi kali kupata visababu vya kuipaka matope Misri
ili kutia doa imani ya kiislamu ya taifa hilo.
Kutokana na kauli hiyo sasa kipindi kilichoikuwa kipeperushwe hewani juzi usiku kimeahirishwa.
Ni makala moja tu ya kipindi hiyo ndiyo
iliyooneshwa - Mojawapo wa waliokuwa majaji wa kupendekeza washindi
kwenye kipindi hicho ni mchezaji maarufu wa densi hiyo aitwae Dina na
wengi wa washindani katika mchuano huo wa belly dancing wala si raia wa
Misri .
0 maoni: