Mambo yanayochangia kupoteza hisia za mapenzi

WEKA TANGAZO
Lipo jambo muhimu analopaswa kuzingatia kila aiye kwenye uhusiano ikiwa anataka kutosheka na penzi la mpenzi wake.
Kwanza ni lazima uitosheleze kwanza akili yako, lakini pili, unapaswa kuamini kwamba uliyenaye ni bora na hata ikiwa kuna kasoro, jambo la msingi ni kuzungumza kuondoa tatizo hilo, siyo zaidi.
Anachanganya mambo, hatosheki
Ukweli ni kuwa wengi wa watu wanaodai hawatosheki katika mapenzi ni wale wanaoziachia akili zao zitake tendo la ndoa zaidi, bila kuangalia uwezo, nafasi, hisia na afya yao ya kukutana kimwili.
Lakini pia wengine ni kwa sababu wanavuta hisia za wapenzi wao wa zamani, ambao labda walikuwa wana uwezo mkubwa zaidi katika tendo hilo kuliko sasa.
Hata hivyo, wakati mwingine wanashindwa kuelewa kuwa hata wale wanaofikiri ni wazuri, kama wangekuwa nao hadi leo, huenda wasingeweza kuendelea kuwa imara.
Hii ni kwa sababu, watu wengi baada ya kukaa pamoja kwa muda mrefu hupoteza nguvu au shauku ya tendo hilo.
Zipo sababu nyingi za hali hiyo, mojawapo ni kutobadilika kwa mazingira au wapenzi kuanza kutoelewa kwa sababu mbalimbali kama vile kutojaliana na kadhalika.
Nguvu za kijinsi
Kama hukuwa unafahamu; ni kwamba, idadi ya wanaume wasiyo na uwezo wa kufanya vyema tendo la ndoa inazidi kuongezeka. Tafiti zinabainisha kuwa wastani wa ndoa nne kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliwa na tatizo hilo.
Pia wanaume sita kati ya 10 wanasumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume, kwamba kama siyo kuwa na uwezo mdogo, basi hukosa kabisa nguvu za kuendelea.
Wengine wanaweza kuanza, lakini hawawezi kuendelea au wengine hata kuanza ni shida.
WEKA TANGAZO

0 maoni: