India kutambua waliobadilisha jinsia
WEKA TANGAZO
mobhai.blogspot.com
Mfano wa watu kama hao ni mtu
anayezaliwa kama mwanamke lakini anahisi kisaokolojia kuwa yeye ni
mwanaume na hivyo hubadilisha jinsia yake na kuwa mwanamume kwa hata
kufanyiwa upasuaji.
Uamuzi huu wa mahakama bila shaka ni wa kihistoria na unasema watu hao wasio jitambua kama wanaume au wanawake wanaruhisiwe na kutambulika kama wanavyotaka
Katika kitambulisho chao hawatajulikana kama wanaume au wanawake bali 'Transgender' kama jinsia ya tatu, sio wanaume wala wanawake.
Takwimu zinasema kuwa watu milioni mbili nchini India wamebadilisha jinsia yao.
Wanaharakati wanasema kwamba, watu hao wanatengwa na kuishi katika umaskini mkubwa na pia wanachukiwa kwa sababu ya kubadilisha jinsia yao.
Wengi hujikimu kimaisha kwa kuwa waimbaji , kuombaomba barabarani na kujihusisha na biashara ya ngono.
Kadhalika wanaharakati wanasema kuwa watu hao hunyimwa huduma za matibabu hospitalini.
''Watu hawa ni raia wa India na lazima waheshimiwe na kupewa nafasi ya kunawiri maishani,'' alisema jaji katika uamuzi wake.
"lengo la katiba ni kuhakikisha kila mtu wa India anapewa nafasi ya kuishi vyema na kujiendeleza maishani, licha ya jinsia , dini na jamii anakotoka''
WEKA TANGAZO
Mahakama ya juu zaidi nchini
India imetoa uamuzi wa kihistoria unaotambua watu waliobadilisha jinsia
yao kama watu wa kawaida katika jamii.
Kawaida kuna jinsia mbili, mke au mume lakini
mahakama hiyo imesema kuwa watu wanaoamua kubadilisha jinsia yao
kuambatana na hisia zao pia ni lazima watambuliwe na jamii na walio
katika aina ya jinsia kivyao.Uamuzi huu wa mahakama bila shaka ni wa kihistoria na unasema watu hao wasio jitambua kama wanaume au wanawake wanaruhisiwe na kutambulika kama wanavyotaka
Katika kitambulisho chao hawatajulikana kama wanaume au wanawake bali 'Transgender' kama jinsia ya tatu, sio wanaume wala wanawake.
"ni haki ya kila binadamu, kuchagua jinsia wanayoitaka,'' alisema jaji katika uamuzi huo ambao unawapa watu hao haki ya kujitambulisha kama wanaume au wanawake
Iliamuru serikali kuwapa watu hao nafasi za kazi na elimu kama jamii ya watu waliotengwa. Mahakama pia imeitaka serikali kuwapa huduma muhimu watu hao wanaochagua kujitambulisha watakavyo.Takwimu zinasema kuwa watu milioni mbili nchini India wamebadilisha jinsia yao.

0 maoni: