BOYFREND KANITUPA BILA HURUMA

WEKA TANGAZO
Doctor, mimi ni binti mwenye umri wa miaka 24 na nimekuwa na uhusiano na kaka mwenye umri wa miaka 27U. Uhusiano wetu hadi leo ulikuwa na umri wa miaka 2. Kwa kweli nilimpenda sana Alex kutokana na tabia zake na muonekano wake pia.

Kutokana na mambo aliyokuwa ananifanyia na kuniambia niliamini kabisa kuwa yeye ndiye mume ambaye Mungu alinipangia .Nilishangaa wiki iliyopita alivyoanza kubadilika na nilipomuuliza alisema “Hisia zangu juu yako zimebadilika na sijui ni kwanini” niliumia sana kusikia hilo na siku mbili baadae aliniambia wazi kuwa hatuwezi kuendelea kuwa wapenzi tena. Doctor, inakuwaje mtu kuweza kubadilika haraka sana kiasi hicho? Naumia sana hadi nashindwa kulala na kula chakula na najikuta nalia mara kwa mara na nashindwa kufanya kazi. Leo nimeangalia kwenye facebook nimegundua kuwa sasa ana msichana mwingine. Doctor nifanyeje?.

JIBU:  Pole sana dada yangu na napenda kukuambia kuwa hauko peke yako katika mtego uliokunasa na kukujeruhi ukweli ni kwamba mchakato wa wewe kuachwa ulianza muda mrefu na kwa bahati mbaya hukuwa na utaalamu wa kuona dalili zake.

Naamini kuwa nia yako ya kuniandikia barua pepe ni kutafuta njia ya kuweza kumrudisha aendelee kuwa mpenzi wako kwani tayari umegundua kupitia facebook kuwa amepata  mwanamke mwingine.

Kabla sijakupa njia ya kupita kumrudisha mpenzi wako ni muhimu uangalie kwa makini sababu kuu za wewe kutetea arudi je ni kweli kwa maneno, matendo na mwenendo wake alikuletea furaha na hali ya kujivunia kutokana na sifa alizonazo? Labda alikuwa ni mwenye hasira au alikuwa na wivu mchafu, au alikusaliti na kutembea na mtu mwingine au alikuwa sio mkweli mara kwa mara au alikuwa hajali hisia zako na maoni yako?. Au jiulize swali linguine gumu, je unao uhakika kuwa ulikuwa unampa sababu za kutosha kabisa kufurahia maisha yake kutokana na wewe kuwa katika maisha yake?.




(1)        Angalia makosa
Kuachana kwa wapenzi huwa hakutokei bila sababu yoyote na hivyo iwapo unataka mpenzi wako akurudie ni muhimu sana kwanza uangalie kosa linalowatenganisha ni nini.Angalia ni jinsi gani mwenzio anaoliona kosa kama ni la kwako,upo uwezekano kuwa amelikuza zana na ikamfanya asiyaone mazuri yako yote.Kama kosa ni lake je angalini jinsi gani umelipokea najinsi gani limekuumiza na mwisho angalia je hukumu ulioitoa na kumwambia katika maongezi yenu ya mwisho ni sahihi au je ulitoa hukumu kubwa zaidi ya kosa lenyewe?

(2)        Kwepa wanaume au wanawake
Iwapo mtu uliempenda amekuacha na hujui kwamba huenda akatamani mrudiane ni muhimu sana kwako ukwepe kujenga ukaribu na watu wa jinsia tofauti na wewe ili kumfanya mwenzio aendelee kuona kuwa nafasi yake bado ipo wazi. Kujaribu kujihusisha na watu wa jinsia tofauti na yako kwa nia ya kumtia wivu ni sawa na kumfukuza kabisa mtu huyo.HIVYO epuka ukaribu wowote na wanaume au wanawake katika kipindi chote cha kuokoa uhusiano wenu.

Ili kuweza kumrudisha na aweze kukung’ang’ania fuata hatua zifuatazo:-
(1)        Usimpe faida ya yeye kuona kuwa amefanikiwa kukuumiza na kukutoa machozi. Jifanye kama vile hukuumia kabisa. Akiona kuwa hajafanikiwa kukuumiza ataanza kujiuliza maswali mengi na moja kati ya jibu atakalolipata ni kuangalia hasara aliyoipata kutokana na wewe kutokuwepo maishani mwake (hii itafanya kazi vizuri kama una uhakika kuwa ulikuwa na mchango mkubwa katika kumletea furaha katika mazungumzo na mwenendo wako, ufundi wako katika tendo la ndoa na usafi kwa ujumla).

(2)        Endelea kumpigia simu na kwa uchangamfu mkubwa mweleze matukio mbalimbali yanayoendelea katika maisha yako. Kwa kufanya hivi ataona kwa hakika jinsi gani ulivyo na nguvu katika nafsi yako ya kupambana na kufanikiwa katika maisha. Jambo  LA KUONYESHA KUWA UNAWEZA KUANGUKA NA KUINUKA NA KUENDELEA NA MAISHA YAKO  ni jambo ambalo huwavuta wanaume japo hawatakuambia. Jitahidi kujizuia usimpigie simu kila siku, panga siku mbili katika wiki ambapo utampigia simu kwa mtindo ulioeleza hapo juu, yaani uchangamfu uwe kiungo kikubwa. Tafadhali kabla hujampigia mtumie SMS isamayo, “samahani naweza kukupigia sasa?” kwa kufanya hivyo utamwonyesha kuwa unaheshimu uhuru wake na usingependa mpenzi wake mpya aanzishe ugomvi kwa sababu yako wewe.

(3)        Kwa kufanya mambo hayo mawili utakuwa umesababisha maswali mengi nafsini mwake na yeye mwenyewe ataanza kukuchokoza kwa SMS au kwa kukupigia simu. Aanzapo hilo hapo jitahidi kujibu SMS zake katika hali ionyeshayo uchangamfu na pia akupigiapo simu jitahidi kuwa mchangamfu vya kutosha. Katika mazungumzo yenu kwa SMS au kwa simu jitahidi kutaja  jina lake mara kwa mara kwa kufanya hivyo unajiunganisha upya katika nafsi yake hali ambayo itaendelea kumsumbua moyoni mwake.

(4)        Hatua hizo zitamfanya apate hamu ya kukuona na pale mtakapopanga kuonana hakikisha kuwa uchangamfu wako unaambatana na tabasamu lenye nguvu ya kuyeyusha barafu iliomo moyoni mwake. Kumbuka tabasamu lako ndilo ambalo lina nguvu ya kumkumbusha mema yote aliyopata toka kwako na utamu wa penzi lako.Nguvu ya uchangamfu wako na mazungumzo yako yataanza kumsumbua pale atakapoachana nawe kwenda kwake. Wakati unapokuwa nae jitahidi kumshikashika kwa mkono aidha mapajani au eneo toka kwenye bega hadi kiwiko cha mkono. Sayansi inathibitisha kuwa njia hii inasababisha mtu kukuthamini zaidi na atapata shida kusahau mazuri yako na hivyo kutafuta njia ya kuunganishwa nawe kwa  upya.

ANGALIZO
 Ni muhimu uzingatie kuwa japokuwa mmetengana huenda bado anakupenda na kwamba huenda kuna jambo ambalo limemchanganya na kwa kipindi hicho akakuona kuwa hufai lakini baadae atazinduka na kutaka kukurudia. Aonapo kuwa bado mlango uko wazi atakuwa mwepesi kurudi. Umuhimu wa jambo hili utauona vizuri iwapo kuachana kwenu kulitokea katika hali ya ghafla au baada ya kutupiana maneno makali

Ni muhimu ujichunguze iwapo kabla hamjatengana hukuwa na wivu wa kupita kiasi, ulishindwa kutimiza ahadi zako mara kadhaa, angalia kama kuna mambo ambayo ulimkatalia bila sababu ya kimsingi, tathmini iwapo una ufundi wa kutosha kumfanya mwanaume afurahie tendo la ndoa kikamilifu na hasa uwezo wa kumsaidia mwanaume aweze kusimamisha uume wake mara nyingine na nyingine na zaidi ya hayo. Kwa kuwa tendo la ndoa ni chakula muhimu sana kwa mwanaume aliyekamilika iwapo atakuhitaji katika eneo hilo basi hakikisha kuwa huwi mvivu na una nyenzo za kutosha kumpagawisha
WEKA TANGAZO

0 maoni: