FURSA ZA NDOA NA UMRI WA WANAWAKE
WEKA TANGAZO
Poleni Sana madada wa zama hizi wenye umri wa kuanzia miaka 30 na kuendelea. Mliochezea fursa.
1. Ulivyokuwa una miaka18 mpaka 22 walikuja waposaji ukasema bado unasoma. Au Wazazi wako walikwambia huwezi kuolewa bado unasoma na hujapata msingi wa maisha. Ulisahau kama ambavyo walivyosahau kuwa maisha anapanga Allah na rizki haina mahusiano na elimu. Mkasahau kuwa unaweza ukaolewa na masomo yakaendelea.
Pole Sana Dada yetu.
2. Kweli ukaendelea na masomo lakini ulivyofika form four au six ulifeli mtihani. Au ulifaulu lakini sio kwa kiwango ambacho ulitarajia ukalazimika urudie mtihani au usomee kitu ambacho hukukitaka. Au ukafika chuo kabisa lakini ukafeli. Au ukafanikiwa kumaliza chuo. Kwakuwa ni binti unapendeza na ndoa ilikataliwa walikuja wachumba wasio rasmi (maboy friend). Na ulikuwakubalia maskini. Wakachill sana mkachat sana na mkatoka out. Kumbe walikuwa wanakupotezea muda tu.
Poleni Sana Dada zetu.
3. Ukafika chuo kikuu ukaanzisha mahusiano na kijana mkawa na ndoto za ndoa. Na wakaja watu wengine kuposa. Ukajibu una mtu wako. Tena kwa mbwembwe ukasema una mpenda sana (mahaba niue). Ukabaki kila siku unabadilisha profile yako kutilia mkazo kuwa umezama kimahaba. Ukasahau kuwa uchumba ni mwanamume kuja nyumbani na akakubaliwa. Kumbe alikutamani tu moyoni ulikuwa haumo ndio maana hakuona haja ya kuleta posa.
Poleni Sana Dada zetu.
4. Uliwakatalia wengi wenye sifa nzuri za kukuoa kwasababu yake. Una maliza chuo ukiwa na miaka 27 au 28. Wale wote waliokuja kutaka kukuoa washaoa. Matokeo yake unapoteza imani na wanaume wote. Hali ya kuwa kosa ni lako.
Pole sana Dada yetu.
5. Walikuja wenye kukuposa ukasema hawana hadhi kama yako. Unataka msomi mwenzio. Au awe na mali. Ukasahau kuwa mwanaume mwenye mafanikio huwa nyuma yake kuna mwanamke makini sana. Na hukutaka umakini huo ukitaka uzikute tu hizo mali.
Pole Sana Dada yetu.
6. Upo kazini mwaka wa tatu hajaja mchumba. Una miaka 30. Wote Wanaokuja wanataka wakate matamanio yao ya kimwili tu. Na ukikumbuka ulitoa mimba kadhaa wakati unasoma kwa kuwa hukutaka mimba hiyo. Itakuharibia malengo yako ya kielemu.
Pole sana Dada yetu.
7. Walikuja watu wakitaka kukuoa ndoa ya uke wenza ukasema hutaki kusikia upuuzi huo. Ni bora usiolewe lakini kuolewa mitala ni nuksi Kwako. Unataka mume wa peke yako. Kuolewa Mitala ni mambo ya kizamani ukasahau kuwa hata bibi yako mzaa babu yako alikuwa ni mke wa nne kama si watano wa babu yako.
Jambo ambalo ulishindwa kulifahamu Dada yetu, ni kuwa huu ulimwengu waoaji ni wachache sana. Wengi ni mafukara sana, wengi ni wazinzi sana sio waoaji, wako mashoga sio waoaji, Wapo walioathirika sio waoaji, Wapo ambao ni wagonjwa wasio weza kuhimimili ndoa………….. Na waolewaji mko wengi Sana.
Maskini Dada yetu ulishindwa kufahamu kuwa ulimwengu wa Leo Waume ni kushare kama sio kwa njia ya Halali basi itakuwa kwa njia ya haramu.
Pole sana Dada yetu.
8. Sasa Leo umri umeenda huna kazi hata pesa ya kununua mahitaji ya kike huna. Wachumba uliokuwa unawaona wa nini Leo unajiuliza utawapata vipi. Masomo Umemaliza kazi hakuna. Ndoa za wake wengi ulizozikataa Leo unazitamani lakini hakuna hata anaekuuliza hali.
Umeamua ujiachie mitandaoni labda kutapatikana mchumba. Kila ajae anataka akuchezee tu.
Au kazi unayo nzuri lakini hakuna mume wa ndoto zako wote wajao wanaitaka mali yako tu. Sasa unaamua ujitafutie mtoto wa Zinaa kwa hoja kuwa una mali zako. Maskini Dada pole sana. Maamuzi ya mtu yalipoteza muelekeo wa maisha yako.
Umebaki umejiinamia hujui Unafanyaje pole sana Dada yetu. Ulisahau kuwa ujana ni maji ya moto. Lakini ujana wa mwanamke ni maji ya moto yaliyomo kwenye chumba cha barafu. Au mlisahau usichana ni biashara ya nyanya.
Wale wote ambao uliona washamba kwa kukubali ndoa mapema wamo ndani ya Ndoa zao. Wanaitwa mama mwenye watoto wanaofahamika baba zao. Maisha yanawaendea. Na wako vizuri tu kimaisha.
Pole sana dada yetu
WEKA TANGAZO
0 maoni: