Wanaume mnajua hili: Mfanyie mwanamke akuzidishie raha
WEKA TANGAZO
MAMBO vipi ndugu zangu? Ni furaha yangu kwa mara nyingine tena kukutana
nanyi wapendwa wasomaji wa safu yetu hii. Tumshukuru Muumba wetu kwa
kutujaalia uhai na afya njema, lakini zaidi ya hapo tumshukuru pia kwa
kutuumbia kitu mapenzi au siyo jamani?
Siku zote hatutaacha kuzungumza juu ya mapenzi kwani ni ukweli usiopingika kwamba mapenzi ndiyo maisha yetu.
Tunafanya
kazi usiku na mchana, tunahangaika huku na huko, lakini mwisho wa siku
tunafikiria jinsi gani tutapata kuboresha na kufurahia maisha na wapenzi
wetu.
Tunafikiria pia ni jinsi gani tunaweza tukapata utulivu na
amani katika maisha ya kimapenzi na wapenzi wetu, waume zetu au wake
zetu katika siku zote za maisha yetu.
Ndugu zangu, Mungu ametuwekea mapenzi ili tupate raha na amani katika maisha yetu.
Kwa
maana hiyo, wale wanaoyachezea na kuyavuruga mapenzi kwa makusudi kwa
kuumiza hisia za wenzao kisha kuwasababishia vilio si watu wa kupendeza
mbele ya macho ya wale wanaojua hasa nini maana ya mapenzi.
Wanawake
ni watu wa kuheshimika na kupewa furaha wanayohitaji. Unapompata
mwanamke anayekupenda na kukuheshimu, huna sababu ya kumfanya ajute kuwa
na wewe.
MPENDE NA MTHAMINI!
Yawapasa wanaume mfahamu kuwa,
wanawake ni zawadi kwenu, pumziko na tulizo la mioyo yenu. Wanawake
ndiyo raha na amani kubwa ya maisha yenu.
Kosa kubwa mnalofanya
wanaume ni kuutumia vibaya mfumo dume hasa katika suala nyeti kama
mapenzi. Mapenzi si ubabe, mapenzi ni upole na ukarimu.
Pamoja na
kwamba mmebarikiwa kwa kupewa nafasi ya kuwa kichwa katika nyumba lakini
linapokuja suala la kurekebisha tofauti zinazojitokeza katika uhusiano
wenu, si vyema kutumia njia za kibabe.
Niwaambie kitu, wanawake ni wa
hisia zaidi na waliobarikiwa kuwa na upendo wa hali ya juu na ndiyo
maana wakapewa dhamana ya kubeba mtoto tumboni kwa miezi tisa na pia
kumnyonyesha na kumlea kwa miaka kadhaa, wewe mwanaume ungeweza?
Nasema
ni watu wa hisia kwa sababu, hivi uliwahi kufikiri ni kwa nini wanawake
huridhika na kujisikia poa kweli wanapopewa zawadi kama ya maua na kadi
zenye ujumbe wa mapenzi ukilinganisha na wanaume?
Unafikiri ni kwa
nini wana machozi ya haraka wanapotendwa? Au unafikiri ni kwa nini
wanapenda kutumiwa ‘love sms’ zaidi kuliko kupigiwa simu? Jiulize.
Mimi
nawaona wanawake kama watu wa kuheshimiwa na kupendwa kwa dhati.
Mkumbuke wanawake ndiyo mama zetu, walezi wetu na ndiyo nyumba zetu.
Jaribuni pia kujicontroo na huo mnaouita ukijogoo kwamba eti ninyi ni
watu msioridhika na mpenzi mmoja.
Jaribuni kufanya kila mnaloweza
kuifuta ile dhana ya kwamba wanaume hawaaminiki hata kidogo. Ridhika na
mpenzi uliyenaye, heshimu hisia zake na thamini mapenzi yake kwako na
mpe ile kitu roho inapenda!
Ni hayo tu kwa leo.
WEKA TANGAZO
0 maoni: