JINSI YA KUTONGOZA MSICHANA KWENYE MTANDAO WA FACEBOOK...

WEKA TANGAZO


Facebook ndio habari ya mjini..., kila mtu yupo na kila msichana mzuri au mbaya, hata yule wa kwenye ndoto zako anaitumia, na ni sehemu iliyo na wasichana wengi zaidi waliounganisha na mtandao mmoja kuliko mtaani, mashuleni na maofisini. 

Na kizuri zaidi kupita yote hayo, hata kama uwe na aibu ya kutongoza kiasi gani, face buku huwezi kutetemeka hata ukucha, unachotakiwa kujua ni mpangilio kwanza ili uweze kuwavutia wasichana wa kila aina.


Facebook ni msitu wa wasichana, kwa hio inakupasa kuwa na subira japo kuwa unaham kubwa, angalia usije haribu na usimtongoze msichana papo hapo, kinachotakiwa ni kufuata masharti kidogo na uwezo mkubwa wa kuangalia na kutafakari...


  • Safisha picha zako...
Futa picha zako zote zile mbaya na ambazo haziitajiki, kwa mfano zile ulizopiga baa na vimada tofauti tofauti, na sidhani kama ulitakiwa uziweke intaneti kila mtu hazione!, hakikisha umetoa picha zote za wanawake wakiwa watupu hata kama ulikua umezishea tu, maana zinaleta muuonekano mbaya kihisia na zinamwonyesha msichana kwamba wewe sio mtu mzuri wa kuanzisha mahusiano naye, zifute na zile ambazo umejipiga mwenyewe, kwa vyovyote vile hazikuonyeshi ukiwa mtanashati, hakikisha zimebaki za kwako peke yako na hata kama za marafiki zisiwe na hisia zozote ambazo zinaweza kumfanya msichana hahisi hujatulia.

  • Tengeneza marafiki zaidi...
Ukiweza kupata marafiki wengi zaidi, ndivyo utakavyo kuwa unaongeza wigo mpana zaidi wa kumpata na kumchambua yule mwenye mvuto zaidi uliokua ukimwota kwenye ndoto zako, kwa hio hakikisha unajiunga na marafiki wengi zaidi uwezavyo, tafuta hata wale uliosoma nao zamani na jiunge kwenye magrupu ya facebook ili upate marafiki zaidi.

  • Marafiki wa marafiki...
Kama ukiwa umeweza kujiunga na marafiki wengi, utakua na nafasi kubwa ya kumchambua yupi unaemtaka, angalia komenti zote zinazopita pamoja na picha mbali mbali zinazopita, ukimwona yule aliyekushika macho na hisia kakomenti, hata kama kakomenti kwenye komenti ya rafiki yako, na wewe komenti hapo hapo na hakikisha umeweka na komenti tata juu yake ili apate sababu ya kukujibu wewe, na kama hajakomenti, tafuta rafiki unayemjua aweze kukutambulisha kwake, muulize rafiki yako kiungwana kwa mfano... "Mambo, nimemwona msichana mrembo rafiki yako Angel, unaweza kunitambulisha kwake?", hili swali lipo moja kwa moja na sidhani kama anaweza kataa kukutambulisha.yeye atakachofanya ni kukusagesti urafiki kwake ili atakapokuadd mkubalie urafiki na hapo ndipo unaanza swaga.

  • Mtumie mwaliko wa kuwa marafiki...
Kwa hio kama mmeweza kukomenti hapa na pale pamoja, sasa hivi atakua ameshakujua, mtumie mwaliko wa kuwa marafiki, kuna asilimia kubwa sana lazima akubali, na mkisha kuwa marafiki sasa unaweza kuanza kukomenti kwenye maandiko yake na picha zake, pia mnaweza piga stori za hapa na pale kwa kuchati, baada ya maendeleo kwenda vizuri na mazoea yamekua ya kutosha, unaweza mwomba siku moja muweze kutoka wote mtoko!.
  • Vuta subira na kuwa jasiri...

Iwapo ikitokea asipokujibu, japo ni mara chache sana iwapo umefuata maelezo vizuri, usije chukulia haraka na kukurupuka, usimuulize chochote kuhusu hilo, endelea na stori, mpe muda na subiri tena wakati mwingine mwafaka wa kumba mtoko tena.

Ili kuongeza mafanikio unaweza fanya kwa msichana zaidi ya mmoja, maana samaki ni wengi sana baharini na wavuvi pia ni wengi xo ni ushindani.
WEKA TANGAZO

0 maoni: