Mwanamke mkongwe zaidi Marekani

WEKA TANGAZO
Jeralean Talley bado anaweza kutembea ingawa kwa kusaidiwa.
Mwanamke mkongwe zaidi nchini Marekani mmoja wa watu wachache waliozaliwa katika karne ya 19, amefikisha miaka 115.
Jeralean Talley alizaliwa tarehe 23 mwezi Mei mwaka 1899 na ni mtu wa pili mkongwe zaidi duniani kwa mujibu wa shirika moja la utafiti la Marekani la Gerontology
Mwanamke mkongwe zaidi duniani ni Misao Okawa anayeishi nchini Japan akiwa na umri wa miaka 116.
Misawa Okawa ndiye mkongwe zaidi duniani akiwa na umri wa miaka 116
Alipohojiwa kilichomfanya kusihi miaka mingi hvyo, , Bi Talley alisema , “Yote ni kwa ajili ya kazi ya Mungu. Na hakuna ninachoweza kufanya kuhusu hilo.”
Anajiandaa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa pamoja na familia yake na marafiki kanisani mjini Michigan siku ya Jumapili.
Alizaliwa katika jimbo la Georgia, na kuhamia Michigan mnamo mwaka 1935 na kufanikiwa kupata mtoto mmoja na mumewe ambaye alifariki mwaka 1988.
Bintiye kwa jina Thelma Holloway, ana umiri wa miaka 76.
Bi Holloway humchunga mamake na ingawa aliwahi kushiriki shughuli ya uvuvi ishara kuwa afya yake ni nzuri yeye hutembea kwa usaidizi. WEKA TANGAZO

0 maoni: