IMEFAHAMIKA KUMBE ADAM KUAMBIANA AMEJIUA MWENYEWE, JIONEE HAPA
WEKA TANGAZO
WEKA TANGAZO
IMEVUJA! Siku
chache baada ya kifo cha mwongozaji na mwigizaji wa filamu Bongo, Adam
Philip Kuambiana, daktari mkubwa wa mastaa ameibuka na kudai marehemu
alijiua mwenyewe.
Waombolezaji wakiaga mwili wa marehemu Adam Kuambiana.
Kwa mujibu
wa daktari huyo ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini kutokana na
maadili ya taaluma yao kuficha siri ya mgonjwa, siku moja kabla ya kifo
(Ijumaa ya Mei 16, mwaka huu), marehemu alimpigia simu na kumwambia
amekunywa dawa za malaria aina ya Fansidar lakini pia amekunywa pombe.
ILIVYOKUWA
Daktari huyo alieleza kuwa, marehemu alimpigia simu kumuomba ushauri juu ya nini cha kufanya na kama kuna madhara yoyote juu ya pombe hizo na dawa alizokunywa.
Daktari huyo alieleza kuwa, marehemu alimpigia simu kumuomba ushauri juu ya nini cha kufanya na kama kuna madhara yoyote juu ya pombe hizo na dawa alizokunywa.
“Aliniuliza
kama kuna madhara yoyote ambayo anaweza kuyapata kwa kuwa alikuwa
amekunywa fansidar kwa ajili ya malaria kisha akapata kiu ya bia na
kuamua kunywa,” alisema daktari huyo.
AMSHAURI KWENDA HOSPITALI
Akizidi kuzungumzia tukio hilo, daktari alikwenda mbele kwa kusema licha ya msanii huyo kuwa na ‘masikhala’ mara kwa mara, lakini kwa kuwa alimwambia jambo ambalo linahusu uhai wake, alimshauri kwenda hospitali iliyo karibu ili akaonane na daktari kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kutoa sumu kwani kitaalam mtu anapokunywa pombe akiwa amemeza dawa za aina hiyo vyote hugeuka kuwa sumu.

Alisema
kutokana na jinsi alivyozidi kumsimulia hali aliyonayo, aliamini kwamba
marehemu alikuwa anamaanisha alichokuwa akikisema hivyo ikabidi
amsisitize kuwahi hospitali haraka.
“Nilimwambia
awahi hospitalini haraka kwani nilijua fansidar ni kali na si dawa ya
kufanyia mchezo. Lakini kesho yake nilipopata taarifa za kifo chake
niliumia sana japokuwa nilijua amejiua kwa kuchangaya fansidar na bia
maana mchanganyiko wa sumu yake mwilini ni mkali sana,” alisema daktari
huyo huku akisisitiza kusitiriwa kwa jina lake.
MAZINGIRA YA KIFO
Kwa mujibu wa mtu ambaye alikuwa karibu na Kuambiana siku ya tukio ambaye naye hakutaka kutajwa jina gazetini, marehemu asingekufa ghafla kama tatizo alilokuwa nalo lingekuwa la vidonda vya tumbo ambavyo vilikuwa vikimsumbua kwa muda mrefu.

“Siku ile
marehemu alikuwa na pesa, alikunywa sana pombe kutoka asubuhi mpaka
usiku mwingi, alikuwa anakula kila anapojisikia sasa hatuelewi ni kitu
gani kilitokea maana haiwezekani mtu akutwe anaendesha na kutapika damu
pasipo kuwa na sumu mwilini,” alisema mtu huyo.
DAKTARI AWAASA MASTAA
Katika hatua nyingine, daktari huyo aliwashauri mastaa wengine kuwa makini kwani mara kadhaa amepata kesi za namna hiyo ambapo wanakunywa pombe vilabuni usiku huku wakiwa katika dozi ya ugonjwa fulani.

“Mimi
nawaambia ndugu zangu, hasa mastaa waache tabia ya kunywa pombe wakiwa
katika dozi, starehe zipo tu. Ni vyema wakawa wanauliza kwa wataalam wa
afya pindi wanapokuwa wamemeza dawa za aina yoyote, nguvu ya dawa
inatofautiana kulingana na ugonjwa husika na muda wa kukaa mwilini,”
alisema daktari huyo.
DAKTARI MUHIMBILI ANENA
Ili kuzidi kupata undani wa mazingira ya kifo cha Kuambiana, Amani lilimtafuta daktari mwingine mtaalam wa magonjwa ya binadamu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Naye kwa sharti la kutotaja jina alieleza madhara ya mtu kunywa pombe akiwa kwenye dozi.

Mke wa marehemu Janeth Rithe ambaye ni Diwani Kata ya Kunduchi (Chadema), akiweka shada la maua kwenye kaburi la mumewe.
“Unapokunywa
dawa hususan hiyo fansidar, inakaa katika mwili kwa takriban siku saba
hivyo mgonjwa anapokunywa pombe ndani ya siku hizo, pombe
inapochanganyika na dawa katika mzunguko wa damu hugeuka kuwa sumu na
mgonjwa ana uwezekano wa kupoteza maisha endapo asipowahishwa
hospitalini,” alisema daktari huyo na kuongeza:
“Wengi huwa
wanajisahau na kunywa pombe kabla ya siku saba lakini wengine huwa
wanakunywa pombe makusudi pale tu wanapoanza kupata ahueni ya ugonjwa
pasipo kutambua nguvu ya dawa bado ipo mwilini mwake na madhara yake
ndiyo hayo.”
JB AANGUKA GHAFLA, AZUA HOFU
Wakati shughuli za kuaga mwili zikiendelea juzi, Jumanne katika Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar, nguli wa filamu nchini ambaye alikatisha ziara yake ya kikazi nchini Uturuki kwa ajili ya kuja kumzika Kuambiana, Jacob Steven ‘JB’, alipewa kipaza sauti ili amzungumzie marehemu ambapo akiwa katikati ya kuongea alianguka ghafla.

Umati wa
watu uliokusanyika viwanjani hapo uliingia hofu na kushindwa kuelewa
amepatwa na nini lakini haikuchukua muda mrefu akasaidiwa na watu na
kuendelea na shughuli nyingine.
MASTAA WAONGOZA KWA VILIO
Mastaa mbalimbali wa Bongo Movies wakiongozwa na Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’, Aunt Ezekiel, Blandina Chagula ‘Johari’, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ waliongoza kwa kulia viwanjani hapo hadi walipofika makaburini, Kinondoni.

Mbali na
mastaa hao kuangusha vilio, Mkurugenzi wa Aset, Asha Baraka alijikuta
akishindwa kuaga kwa kuhofia kuuona mwili wa marehemu na kudai huwa
akitazama maiti anamuota kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Marehemu
Kuambiana ambaye alikuwa nguzo muhimu katika ‘ku-dairekti’ filamu,
alipatwa na mauti katika Gesti ya Silvarado, Sinza- Kwaremmy jijini Dar.
Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina.
-GPL
0 maoni: