JE WAJUA WALE WAUMINI WALIOLISHWA NYASI NA MCHUNGAJI WAO SASA WAANZAKULA MITI, CHEKI HAPA
WEKA TANGAZO
Dada aliyepona jino kwakutafuna majani akiendelea na lishe yake kwa furaha huku wenzake wakiwa wamelala. |
Ikiwa
ni miezi miwili imepita toka huduma ya mtume Lesego Daniel wa nchini
Afrika ya kusini ya Rabboni Ministries Centre kuwa maarufu duniani baada
ya waumini wake kula manyasi ikiwa moja ya namna ambavyo roho mtakatifu
alivyowaongoza, bado waumini wa huduma hiyo wanaendelea kula manyasi na
kufanya njia moja wapo ya kupata uponyaji licha ya watu wengi kupinga
ufunuo wa namna hiyo.
Kupitia
picha zilizotolewa na huduma hiyo kupitia ukurasa wake wa facebook,
umeonyesha waumini wakikimbilia matawi ya miti na kuanza kula majani
yake, huku mmoja wa waumini aliyefika kanisani hapo kwa mara ya kwanza
amesema amepona jino lililokuwa likimuuma mara baada ya kula majani,
amesema kwamba alifika kanisani hapo kwa mara ya kwanza siku ya ijumaa
akiwa na dawa za kutuliza maumivu pamoja na panado lakini hazikumsaidia
ila majani yalimponya na kwamba akirudi nyumbani mumewe (ambaye pia
mtumishi) atafurahi sana kwa uponyaji huo.
Huduma
hiyo ambayo inaongozwa na mtume msomi Lesego Daniel imekuwa ikipingwa
na watu wengi hasa baada ya tukio la waumini kula nyasi huku pia mtume
huyo mda mwingine huwafanyia maombi waumini wake huku akiwa amewakanyaga
migongoni. Licha ya kelele kutoka kwa viongozi wa dini na makanisa
mbalimbali kuwakataza waumini wao na wakristo kuwa makini na huduma ya
mtumishi huyo, ndio kama wamewaruhusu kwenda huko kwakuwa inasemekana
huduma hiyo imeendelea kujikusanyia waumini kila kukicha. Huduma hiyo
ilikuwa ikifanya huduma zake katika majengo ya chuo kikuu cha teknolojia
cha Tshwane kwasasa wamepata enero lao ambalo wameliita shamba la
Rabboni ambalo wanatarajia kuhamia huko jumapili ijayo ya tarehe 4
http://googleads.g.doubleclick.net/aclk?sa=L&ai=CVqEm71RhU4CVGKvi7gaz7IEw0YWs1AS5u47PgwHAjbcBEAEg6cqvI1CttMa__f____8BYMMGyAEBqAMByAOfBKoErAFP0NurYRSSdahC8lKRDyb52Lub59S1V64sMoLnnBCB3czSgLYDZvVq68uAundnFITqj_oIFkGnlQId0ZcEGQAGJR_dEvIRGhtm57oecKK857rb9p4WcO8gIZMe5Gjrmlr4rn8fz9ho-ZmMJk4gy-FpgHH9uv80t9rjJUKapHzjo5d7JSLG4BTj3Swb1GIzOax8jddnfjeIM-rulCwvPVuAnNYV6pt4is1iboSxoAYayAbJhabZgwGAB4vckhQ&num=1&sig=AOD64_0jPBxErVokBl0qJygGSzMlJOwkXA&ctype=21&video_id=mlGtnG1yzPM&client=ca-pub-3642407196773375&adurl=http://www.youtube.com/watch%3Fv%3DmlGtnG1yzPM&nm=123&nx=112&ny=135&mb=2&nb=0&clkt=25087&jca=447
WEKA TANGAZO
0 maoni: