Jana tulikua na kamjadala karefu kidogo kuhusu hawa wandugu kitu gani
wanataka ili watulie ndoani. Nami nimeyachuja, nikaongeza na tu chumvi
kidogo ili kunogesha. haya si maneno yangu. Ni yakwao wenyewe. Mwenye
macho na asome na mwenye kusikia asikilize sauti yake mwenyewe
ikisoma....... Usione mwanaume katulia na mkewe ukaanza kuuliza mke
kamwendea kwa mganga yupi,uganga tunao wenyewe wanawake shutu
kuwajibika;
1. Kumjali mumeo kadri uwezavyo. Usipo mjali wengine wataja saidia
kumjali. Mfano …..kuna watu hapa hata hawajui leo mume wake kava nini!!
Wengine hata soksi za waume zao haawajui ziko ngapi. Mume anaenda kazini
hata hukumbuki kava shati rangi gani. Akipita na kimada mbele yako
unaanza kujiuliza, sijui ndo Yule……. Mbona shati ka lake??? Hivi leo
alivaa shati ile eh……! Jipange mwanamke
2. Jifunze kuhusu mapenzi na mbinu mpya…. Hii nadhani wanasema ubunifi
uwe mara dufu hasa chumbani. Sio mbaya hata mkizungumza na wanawake
wenzenu mkapata maujuzi mapya. Style zile apendazo mumeo ndo mwake. Basi
hata japo uliza mume wangu vipi hii… nah ii je!! Na Msijisahau, yale
masham sham ya uchumba yaendelee mpaka kwenye ndoa.
3. Tuwaelewe waume zetu kutokana na hali zao. Mfano kachoka,
anamatatizo. Usiwe wakati wa sisi kuanza lawama. Mume kapata msiba, wewe
ndo unapeleka shida zako. Atakuona hovyooo kabisa.
4. Usafi wa nyumba, mwili mzima bila kusahau kinywani. Na uvae vizuri
uvutie. Hapa hasa ni usafi na kujipenda. Usione uvivu kujipamba ukiwa
kwako na mumeo. Shurti bi mdachi unukie vizuri. Chmba chako sio kinanuka
mikojo ya mtoto. Na wanao pia wawe wasafi jamani.Mume anazidi kupata
hamasa ya kuwa karibu na familia. Mjitunze vizuri kipindi cha uzazi….
Sio mnanuka maziwaaaa. Yani mazingira yooote yawe ya kushawishi.
Nyumbanyingine ukikanyaga tu sakafu, mchaka kama upon je.
5. Jikoni pia uwe mbunifu. Na upate nafasi ya kumpikia mumeo chakula
wewe mwenyewe sio kila siku dada wa kazi ndo mpishi. Mume asipate hamu
ya kula baa. Kama ni mpenzi wa pombe basi aishie kunywa tu, msosi
ataupata kwa mkewe.
6. Kelele majumbani. Hapa wanawake tuache midomo. Kitu kidogo maneno
kibao. Kila saa wewe tu ndo unaekerwa. Huishi lawama. Mara nyingine
tuchague kukaa kimya, au hata kama tunasema basi kwa sauti ya chini. Si
vizuri kumpandishia mumeo sauti hata kama kakosea sema nae tara tara. Na
tone zetu ziwe zile za mahaba. Sio umekaza sauti ka unaamrisha gwaride
mweh!!!
7. Mnapokosa mkubali makosa na muombe msamaha. Wanaume wanapendaga
kuonekana wao ndo kichwa na wanaheshika. Sio unarekebishwa tabia na
mumeo, unaishia kununa siku tatu ndani hapaeleweki. Umenunaaaaa hatari.
8. Msijibweteke. Maisha ya sasa ni kusaidiana. So jishughulishe mtoto wa
kike. Ukiwa na kakitega uchumi kako si mbaya. Hata mume anakuheshim.
9. Mnapokuwa na watoto mjitahidi kugawa muda kwa ajili ya mtoto na kwa
ajili ya mumeo pia. Na msiwe wavivu kutoa unyumba kisa una watoto
kama kunanililo sahau ongezea.......
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni