Wazazi waliandamana kuishinikiza serikali kuongeza kasi ya kuwatafuta watoto wao
Wazazi wa wasichana 230,
waliotekwa nyara Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, wamefanya maandamano
kuiomba serikali ya Nigeria kuongeza juhudi na kasi ya kuwatafuta watoto
wao waliotekwa nyara na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Boko
Haram.
Wasichana hao walikuwa wanafunzi katika mji wa
Chibok na walitekwa nyara wakijiandaa kufanya mitihani yao zaidi ya wiki
mbili zilizopita.‘‘Tunataka kuona juhudi zaidi,’’ alisema mama huyo
Kundi la wapiganaji la Boko Haram, halijasema chochote kuhusu madai kwamba wapiganaji wake ndio waliowateka nyara wasichana hao usiku wa tarehe 14 mwezi Aprili.
Wazazi walijawa na majonzi wakati wa maandamano wakisema serikali inajikokota
Mnamo siku ya Jumatano, mamia ya wanawake waliandamana wakiwa wamevalia nguo nyekundu licha ya mvua kubwa kunyesha na kutembea hadi majengo ya bunge mjini Abuja kuwasilisha ujumbe.
Wanailalamikia serikali kwa kusema haifanyi juhudi za kutosha kuwanusuru wasichana hao.
"Tunawashukuru wanawake waliotuunga mkono,'' alisema mama huyo akiongeza kuwa maandamano huenda yakashinikiza serikali kuongeza kasi ya kuwatafuta watoto wao.
Tunawaomba na wale walio huko nje kuja kutusaidia kwa sababu huu ni msiba mkubwa kwa wazazi wetu.
Alipokuwa anaongea, kilio na mayowe yaliweza kusikika kutoka kwa akina mama wengine waliokuwa wanaandamana.
Awali waziri wa mambo ya ndani wa Nigeria aliambia BBC kuwa alielewa hisia za wanawake hao, lakini serikali haiwezi kufichua inachofanya kujaribu kuwanusuru watoto hao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni